Mzee Kawawa afariki dunia!

Mzee Kawawa afariki dunia!

Dah, basi tena. alisemwa sana jana kabla ya siku yake mwishowe imetimia.

Mungu amlaze pema peponi kiongozi huyu shujaa wa wafanyakazi wa nchi hii.
 
TBC Wanarun program zake za zamani, hivi sasa anahojiwa na David Wakati. Natumaini pia tutapata fursa ya kuiona tena ile filamu ya 'Fimbo ya Mnyonge'. Mimi niliiona mwaka 79 pale Viwanja vya Tangamano, mjini Tanga wakati huo wakiita Sinema za Dezo.

Sasa Kawawa anaeleza Alipoingia Tanu, 1956, mwaka mmoja baada ya David Wakati kuajiriwa TBC ile ya Mkoloni.

RIP SIMBA WA VITA.
Filam maalufu aliocheza Marehemu Mzee wetu inaitwa "Muhogo Mchungu"

Kawawa.jpg


 
R.I.P Mzee Kawawa lakini tuombee. Mjulishe mwl. Nyerere kuwa nchi sasa iko mikononi mwa wezi.
 
sasa amebaki mama nyerere tu mwenye heshima the rest sijui.
 
Dah, basi tena. alisemwa sana jana kabla ya siku yake mwishowe imetimia.

Mungu amlaze pema peponi kiongozi huyu shujaa wa wafanyakazi wa nchi hii.
Mkuu wangu kichuguu, yawezekana 'alisemwa sana' lakini ukiangalia wa kwanza kuanza kuchokonoa ni mimi haswa, chanzo changu kilionesha kuwa hali ya mzee haikuwa ya kawaida na kilisisitiza kuwa ni vema umma ukafahamishwa kuwa hali ya mzee inaelekea kubaya...

Ni vema tulishaandaliwa mazingira ya kujua kuwa mzee wetu alikuwa mgonjwa na hamjashtukizwa, nadhani niliandika pia kiungwana kabisa kuwa hali ya mzee si shwari na yupo ICU.
 
Hakika alikuwa Kiongozi mvumilivu sana, mabaya yote yalikuwa ya kwake na aliyavumilia na kuwa mtiifu kwa kiongozi wake na Taifa kwa ujumla, tumpate wapi kiongozi mvumilivu wa aina hii katika karne hii? Machozi ya Mwalimu ni ushahidi wa uvumilivu wa mzee Kawawa.

Mungu kampenda zaidi yetu. ulale kwa amani, Amin.
 
Hakika alikuwa Kiongozi mvumilivu sana, mabaya yote yalikuwa ya kwake na aliyavumilia na kuwa mtiifu kwa kiongozi wake na Taifa kwa ujumla, tumpate wapi kiongozi mvumilivu wa aina hii katika karne hii? Machozi ya Mwalimu ni ushahidi wa uvumilivu wa mzee Kawawa.

Mungu kampenda zaidi yetu. ulale kwa amani, Amin.

Wakuu,

Tujenge Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia kwa heshima yake.

Tumeweza DODOMA UNIVERSITY hatuwezi kushindwa kwa ajili ya heshima yake.-----KAWAWA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY.

Sijui tutamlipa nini mzee wetu kwa mema yote aliyoitendea nchi yetu???!!!!!

Kwa upande mwingine, JF tukae chini baada ya mazishi na kufikiria jinsi gani tunaweza kushirikiana na JKT ili kuibadilisha shule ya Sekondari ya Kawawa iliyoko pale Mafinga, Iringa ili ndani ya miaka minne iwe kati ya shule kumi bora za sekondari hapa nchini. Tunaweza kukiamua na kukubaliana.

Kheri ya mwaka mpya kwenu wote pamoja na familia zenu.
 
Roho ya marehemu Mzee Wetu KAWAWA ipate Rehema kwa MUNGU ipumzike kwa AMANI.
Poleni ndugu wa marehemu,Mungu awape uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu kwa familia na Watanzania kwa ujumla.
 
Kikawaida kulingana na maandiko umri wa binadamu kuishi ni miaka 70, kwa huyu Mzee wetu nadhani amefariki akiwa na 83, sio mbaya tumshukuru Mungu kwa kumuweka hadi leo hii, yeye ndiye mtoaji na ndiye anayetoa pale anapoamua. Sisi ni mavumbi tu

RIP

Kaizer; Sijui ni maandiko gani you're refering to....However life expectancy sehemu nyingi duniani sspecially zile ziliozendelea ni miaka 70.
Ambayo tukirudi kwenye pointi bado ni michache sana na ndio maana tuwe happy as much as we can for as life is too short.

Inasemekana kama ukiishi kwa miaka sabini basi minimally unalala kwa miaka 30,sasa miaka 70 uliyoishi ukiondoa 30 ya kulala unabakiwa na 40.

Kwenye hiyo miaka 40 unaambiwa utoe miaka 18 as a minor,kwani kwa miaka 18 ndani ya maisha yako wewe ni mtoto,na huwezi kujiamulia mambo yako wewe mwenyewe kwa uhuru,so kwenye 40-18,unabakiwa na miaka 22 tu.

Kwenye hiyo miaka 22,unaambiwa miaka 10 ni ya matatizo kama magonjwa nk....Hapo unabakiwa na miaka 12 tu.

Hiyo miaka 12,assume hujafungwa jela hata siku moja na kwamba hukulala kwa zaidi ya muda unaozidi miaka 30,na matatizo na magonjwa kwa kipindi chote hayakuzidi miaka 10 ilhali jela hujaonja hata siku moja.

Kwa kifupi life is too short,we as human beings are never perfect,and so therefore we should never strive for perfection.......We should strive for exellence rather than perfection....As they say "Hujafa Hujaumbika"

Sote tumo safarini,and not much.In this ceremonial,we should celebrate his life for he has strived for exellence during his life tenure!

Rest In Peace Ndugu Rashid Mfaume Kawawa and the Nation will remember you for what you have done for it and not what it has done for you.
 
Mungu wetu Mwema uliyemuumba Mpendwa wetu Rashidi hatimaye umemuita kwako.

Poleni sana Watanzania wote.

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen
 
Pumzika kwa amani ni safari yetu sote, naomba kuuliza hivi ni sahihi kupiga king'ora hospitali????
 
hapo ndipo ninapowakumbuka sikinde waliposema, "ni majaliwa yake Mungu ee kuuona mwaka" kila nafsi inastahili ilichopanda, na Mungu amstahilie kwa aliyoyatenda enzi za uhai wake
 
Back
Top Bottom