Kawawa anazungumzia kuanzishwa kwa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Operesheni Vijiji. Anakiri ilitumika nguvu kubwa, watu walikuwa hawataki kuhama, 'tulikuwa wakali', hatukuwa na mchezo mchezo, ilifikia mahali wakisikia Kawawa yuko kijiji fulani, vijiji vinavyofuata, walihama usikuusiku kabla hajawafikia.
Anazungumzia Ujamaa, anasema nia Ujamaa ni njema, kila kitu ni mali ya umma, hakuna matajiri na masikini, kila kitu ni bure, maji bure, elimu ure, hospitali bure. Hata hivyo anasikitikia kufikia mahali ujamaa umeshindwa, serikali aiwezi tena kutoa huduma za bure.
Anamalizia kwa kutoa wito kuishika sana elimu kama mkombozi wa kweli kwa Mtanzania, ni kusoma ili ujitegemee. Kosoma ni kuamsha elimu ili uweze kuona mbali, ujitegemee sio kusubiri kajiriwa.
Program inaendelea TBC.
RIP RASHIDI MFAUME KAWAWA.