Mzee Kawawa afariki dunia!

Mzee Kawawa afariki dunia!

Mwenyezi Mungu ilaze mlaze pema Simba Wa Vita.
 
Mshirazi au Mod:

Mzee Kawawa nadhani hakumaliza Tabora boys akiwa na miaka 30. Hivyo angalieni fact ya wakati akiwa huko.
 
RIP

Msalimie Nyerere, mweleze kuwa akina JK na wenzake wamegawana nchi, Kawawa usipomweleza wewe atamweleza nani? angekufa Chenge nina hakika angemkimbia Nyerere huko..
 
RIP kamanda wa vita. Tumempoteza mpiganaji wa kweli - poleni Watanzania wenzangu.
 
sinkala-albums-sinkala-picture813-flag4.gif
 
Kama kuna kiongozi ambaye jina lake limetumika kufafanua vitu, Kawawa ni mojawapo gear 4WD, bia, nk
Pumzika kwa amani Simba wa Vita!
 
Hii ni ratiba fupi iliotolewa muda si mrefu mzee wetu kawawa mfaume rashid anatarajjiwa kuagwa kesho saa sanane pale uwanja wa karimjee ;mwili utatolewa hospital ya lugalo saa saba na gari maalum la jeshi kupitia barabara ya ali hassana mwinyi;wananchi wote tunaombwa kuunganika na wanaafamilia pale karimjee wale watakaoshindwa mnaombwa kusimama njiana ama barabarani wakati akipitishwa kuelekea karimjee

Mwili utaagwa kuanzia saa nane mpaka kuminambili baadae unaelekea nyumbani ambapo tar 2 january 2010 mwili utazikwa nyumbani kwake madale saa saba kamili;mtabiri maarufu shikh yahya hussein anatarajiwa kuwa mmoja wa watakaofika mazikoni..Mungu amlaze pema peponi

KAMANDA KOVA

NDUGU WANANCHI KUTOKANA NA KIFO CHA MZEE WETU MH KAWAWA MFAUME RASHID SERIKALI IMEOMBA SI VYEMA WATU MKAPIGA TUMBATU ZENU AMA BARUTI ZENU KILA MTU AFURAHIE KIMYA KIMYA BILA FATAKI ZOZOTE,TUNAAMINI WOTE MTAITIKIA WITO HUU

TUNASHUKURU WENU

KAMANDA KOVA
 
From: Mwanakijiji.com

Waziri Mkuu wa Tanganyika na mpigania huru wa Tanganyika na Muasisi wa Muungano mzee Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia. Habari ambazo zinatiririka taratibu kutoka vyanzo mbalimbali zinadokeza kuwa mzee Kawawa amefariki dunia leo na mpango wa kulitangazia taifa msiba huu mkubwa uko mbioni na wakati wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atalihabarisha taifa juu ya msiba huu wa kitaifa wa mmoja wa viongozi waliopendwa na waliolitumikia taifa kwa muda mrefu. Mzee Kawawa alikuwa ni swahiba wa karibu zaidi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere.

kawawa_1.jpg


Mzee Kawawa alizaliwa Mei 27 , 1926 huko Songea kijiji cha Matepwende mkoani Ruvuma. Alianza elimu ya msingi huko Liwale Lindi. Aliendelea na elimu ya kati (middle school) hapo Dar-es-Salaam school ambapo mmojawapo wa wanafunzi wengine ni marehemu mzee Kanyama Chiume mpigania uhuru toka Malawi aliyeishi uhamishoni nchini Tanzania kwa muda mrefu. Wengine katika shule hiyo wakati huo ni pamoja na kina Abdul Sykes, Ali Sykes, Hamza Aziz na Faraji Kilumanga.

Aliendelea na masomo yake huko Tabora Boys kati ya 1951-1956. Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanganyika mwaka 1962 wakati Mwalimu Nyerere alipoamua kwenda mikoani kujenga chama na kufanya shughuli za kisiasa. Baadaye aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu mwaka 1972-1977 na akawa miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wakati wa vita ya kumng'oa nduli Idi Amin ambapo alitembelea wapiganaji wetu waliokuwa mstari wa mbele kule Uganda. Hii ilimpatia jina la "Simba wa Vita" jina ambalo lilimkaa vyema kwa muda mrefu.

Kabla ya kuingia katika harakati za kupigania Uhuru Mzee Kawawa alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa Shirikisho la Wafanyakazi mwaka 1955 ambapo alichaguliwa kuwa Katibu wake Mkuu wa kwanza. Ni katika nafasi hii ndiyo aliweza kuanza kushiriki kwa nguvu zaidi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika akihamasisha wafanyakazi. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Serikali.

Februari 1956 Mzee Kawawa aliacha kazi yake ya Shirikisho la Wafanyakazi kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali kitu ambacho kilimkataza kuhusisha na siasa na kuamua kuingia katika harakati za kudai uhuru kupitia TANU. Alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU mwaka 1957, Makamu mwenyekiti wa TANU mwaka 1960.

Mwaka 1964 baada ya Muungano Mzee Kawawa alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais akiwa ni msaidizi wa Rais wa Muungano kwa upande wa mambo ya Bara.
Katika siasa amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo ile ya Ukatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM na amekuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM.

Mzee Kawawa alikuwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto nane na mojawapo ya kazi zake za awali ilikuwa ni uchezaji wa filamu za uhamasishaji na akawa ndiye mcheza filamu wa kwanza kiongozi mweusi (lead actor).

Mzee Kawawa alikimbizwa hospitali hapo jana kutokana na hali yake kuwa mbaya na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi; ambapo mapema leo asubuhi alifariki dunia. Mipango ya mazishi inaandaliwa.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Pema Peponi, Amina.

- Mkuu MMJ hakuna la kupunguza wala kuongeza, Bwana alitoa Bwana ametwaa, lihimidiwe jina la Mungu!

Respect.

FMEs!
 
sala zetu kwa marehemu,ndugu ,jamaa ,marafiki na watanzania kwa ujumla....

MoD tunaomba ili tupate mtiririko mzuri thread zote za kawawa kufariki ziunganishwe....nadhani members si vema kuanzisha topic wakati tayari unaona ipo....najuwa mara nyingi tunakosea wote hili....na MoD huwa anaziunganisha...

ahsante!! na Poleni !!
 
Poleni sana wafiwa, poleni sana Watanzania........ulale pema peponi Mzee Kawawa
 
R.I.P. Mzee Kawawa. Amina.
Pole Modou na Wanafamilia Wote.

SteveD.
 
Ni msiba mzito sana, tutakukumbuka daima mpigania uhuru. Mwenyezi mungu akulaze mahali pema peponi
 
Back
Top Bottom