Mzee Kawawa afariki dunia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Kawawa afariki dunia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshirazi, Dec 31, 2009.

 1. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wanabaraza, habari nilizozipata muda huu ni kwamba Mzee wetu RASHID M KAWAWA hatunae tena...

  Soma habari iliyohaririwa kwa kiasi:


  Waziri Mkuu wa Tanganyika na mpigania huru wa Tanganyika na Muasisi wa Muungano mzee Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia. Habari ambazo zinatiririka taratibu kutoka vyanzo mbalimbali zinadokeza kuwa mzee Kawawa amefariki dunia leo na mpango wa kulitangazia taifa msiba huu mkubwa uko mbioni na wakati wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atalihabarisha taifa juu ya msiba huu wa kitaifa wa mmoja wa viongozi waliopendwa na waliolitumikia taifa kwa muda mrefu. Mzee Kawawa alikuwa ni swahiba wa karibu zaidi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere.

  [​IMG]

  Mzee Kawawa alizaliwa Mei 27 , 1926 huko Songea kijiji cha Matepwende mkoani Ruvuma. Alianza elimu ya msingi huko Liwale Lindi. Aliendelea na elimu ya kati (middle school) hapo Dar-es-Salaam school ambapo mmojawapo wa wanafunzi wengine ni marehemu mzee Kanyama Chiume mpigania uhuru toka Malawi aliyeishi uhamishoni nchini Tanzania kwa muda mrefu. Wengine katika shule hiyo wakati huo ni pamoja na kina Abdul Sykes, Ali Sykes, Hamza Aziz na Faraji Kilumanga.

  Aliendelea na masomo yake huko Tabora Boys kati ya 1951-1956. Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanganyika mwaka 1962 wakati Mwalimu Nyerere alipoamua kwenda mikoani kujenga chama na kufanya shughuli za kisiasa. Baadaye aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu mwaka 1972-1977 na akawa miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wakati wa vita ya kumng'oa nduli Idi Amin ambapo alitembelea wapiganaji wetu waliokuwa mstari wa mbele kule Uganda. Hii ilimpatia jina la "Simba wa Vita" jina ambalo lilimkaa vyema kwa muda mrefu.

  Kabla ya kuingia katika harakati za kupigania Uhuru Mzee Kawawa alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa Shirikisho la Wafanyakazi mwaka 1955 ambapo alichaguliwa kuwa Katibu wake Mkuu wa kwanza. Ni katika nafasi hii ndiyo aliweza kuanza kushiriki kwa nguvu zaidi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika akihamasisha wafanyakazi. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Serikali.

  Februari 1956 Mzee Kawawa aliacha kazi yake ya Shirikisho la Wafanyakazi kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali kitu ambacho kilimkataza kuhusisha na siasa na kuamua kuingia katika harakati za kudai uhuru kupitia TANU. Alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU mwaka 1957, Makamu mwenyekiti wa TANU mwaka 1960.

  Mwaka 1964 baada ya Muungano Mzee Kawawa alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais akiwa ni msaidizi wa Rais wa Muungano kwa upande wa mambo ya Bara.

  Katika siasa amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo ile ya Ukatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM na amekuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM.

  Mzee Kawawa alikuwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto nane na mojawapo ya kazi zake za awali ilikuwa ni uchezaji wa filamu za uhamasishaji na akawa ndiye mcheza filamu wa kwanza kiongozi mweusi (lead actor).

  Mzee Kawawa alikimbizwa hospitali hapo jana kutokana na hali yake kuwa mbaya na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi; ambapo mapema leo asubuhi alifariki dunia. Mipango ya mazishi inaandaliwa.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu Pema Peponi, Amina.

  Imeandikwa na: Mwanakijiji
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kumaliza mwaka ni jambo ZITO sana. MUNGU ashukuriwe, maana ndiye mwenye uwezo wa kupanga na kupangua. Sote tuombe Mungu.. Mengine zaidi baadaye... INASIKITISHA
   
 3. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nimepata mshtuko, tafadhali mwenye habari za uhakika atujuze!!
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Taarifa zitatolewa IKULU muda si mrefu.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Sina uhakika ngoja niwasiliane na waliopo Dar watuhakikishie hii habari. nilimwona ktk news akiwa ICU mhimbili
   
 6. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jamani haya yanayoenea mtaani ni sahihi?
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Inna Lilah
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Habari zilizonifikia kupitia luninga ya ITV ni kuwa Mzee wetu Simba wa Vita amefariki Leo Hosipitalini alikokuwa amelazwa!

  RIP Mzee Kawawa!
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Dec 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Yes confirmed, RIP mzee wetu!
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  R.I.P Mzee K!!! u will be remebered!!!
   
 11. D

  Dotori JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  RIP Mzee. Utakumbukwa kwa mchango wako katika mapambano ya uhuru wa nchi hii.
   
 12. Brutus

  Brutus Senior Member

  #12
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Duh! Mungu amlaze mahali pema peponi!
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  RIP Mzee Kawawa. One of the few leaders God had given, go well.

  We hope your death is not related to JK's "ushindi wa Sunami" in 2010!!
   
 14. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  R.I.P mzee wetu, Poleni wanafamilia wote wa Kawawa.
   
 15. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  R.I.P utakumbukwa
   
 16. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  R.I.P Simba wa Vita. Poleni Watanzania wenzetu.
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  R.I.P mzee!
  utakumbukwa daima
   
 18. Mnyonywaji

  Mnyonywaji Member

  #18
  Dec 31, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R.I.P. Simba wa Vita
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ni kweli amefariki wala si udaku..
   
 20. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Simba wa Vita na kiongozi wa ukweli kwa heri! R.I.P. Kawawa
   
Loading...