Mzee Kawawa afariki dunia!

Mzee Kawawa afariki dunia!

It pains alot!!!!!!!!!!


Kweli imenigusa sana,
Nimedondosha Mchozi maana huyu Baba ndio kimbilio letu watu wa Kusini.
Sasa itakuwaje,
Mungu amemchukua sekunde chache kabla ya Mwaka mpya.
Yaani Taifa linaanza mwaka mpya kwa Msiba Mkubwa kama huu.
kweli Hujafa Hujaumbika.
Jamani tuwe waangalifu Kwa muda huu mfupi ulio baki.

Watakao uona mwaka huu jamani tutumiane hata sms tuu.

Ahsanteni wanandugu,

Benno
+255 713 092 952

GODBLESS ALL WHO WILL WISH ME A HAPPY NEW YEAR 2010
 
Kweli imeniguswa sana,
Nimedondosha Mchozi maana huyu Baba ndio kimbilio letu watu wa Kusini.
Sasa itakuwaje,
Mungu amemchukua sekunde chache kabla ya Mwaka mpya.
Yaani Taifa linaanza mwaka mpya kwa Msiba Mkubwa kama huu.
kweli Hujafa Hujaumbika.
Jamani tuwe waangalifu Kwa muda huu mfupi ulio baki.

Watakao uona mwaka huu jamani tutumiane hata sms tuu.

Ahsanteni wanandugu,

Benno
+255 713 092 952

GODBLESS ALL WHO WILL WISH ME A HAPPY NEW YEAR 2010
dah, leo nahisi nitakwenda home kwa MIGUU ili niweze kuona 2010, maana madreva wa daladala hawakawii kutuingiza mitaroni.
R.I.P kawawa
 
Rest In Peace Mzee Rashid Mfaume Kawawa.Utakumbukwa daima...
 
Jamani, give me a break. We already have too many holidays. Katika siku ya Kawawa tutafanya nini? Tutamkumbuka nini? Siku ya Nyerere watu wanafanyaga nini? Ya Karume je? Hata watoto wetu hatuwaambii tunakumbuka nini siku hizo, basi watu kazi yao ni kulewa na kulala tu. Jamani, itakuwa aibu tukifanya jambo hili. Mimi nadhani tungekuwa na siku moja tu ya waasisi wa taifa, tukawakumbuka wote kwa pamoja, tuache kuongeza siku za uvivu, tuchape kazi.


duuuuuh! imetulia hiii
 
MUNGU ailaze roho ya marehemu Kawawa mahali pema peponi AMEN
 
Wanabaraza, habari nilizozipata muda huu ni kwamba Mzee wetu RASHID M KAWAWA hatunae tena...

Waziri Mkuu wa Tanganyika na mpigania huru wa Tanganyika na Muasisi wa Muungano mzee Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia. Habari ambazo zinatiririka taratibu kutoka vyanzo mbalimbali zinadokeza kuwa mzee Kawawa amefariki dunia leo na mpango wa kulitangazia taifa msiba huu mkubwa uko mbioni na wakati wowote kuanzia sasa Rais Jakaya Kikwete atalihabarisha taifa juu ya msiba huu wa kitaifa wa mmoja wa viongozi waliopendwa na waliolitumikia taifa kwa muda mrefu. Mzee Kawawa alikuwa ni swahiba wa karibu zaidi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere.

kawawa_1.jpg


Mzee Kawawa alizaliwa Mei 27 , 1926 huko Songea kijiji cha Matepwende mkoani Ruvuma. Alianza elimu ya msingi huko Liwale Lindi. Aliendelea na elimu ya kati (middle school) hapo Dar-es-Salaam school ambapo mmojawapo wa wanafunzi wengine ni marehemu mzee Kanyama Chiume mpigania uhuru toka Malawi aliyeishi uhamishoni nchini Tanzania kwa muda mrefu. Wengine katika shule hiyo wakati huo ni pamoja na kina Abdul Sykes, Ali Sykes, Hamza Aziz na Faraji Kilumanga.

Aliendelea na masomo yake huko Tabora Boys kati ya 1951-1956. Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanganyika mwaka 1962 wakati Mwalimu Nyerere alipoamua kwenda mikoani kujenga chama na kufanya shughuli za kisiasa. Baadaye aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu mwaka 1972-1977 na akawa miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wakati wa vita ya kumng'oa nduli Idi Amin ambapo alitembelea wapiganaji wetu waliokuwa mstari wa mbele kule Uganda. Hii ilimpatia jina la "Simba wa Vita" jina ambalo lilimkaa vyema kwa muda mrefu.

Kabla ya kuingia katika harakati za kupigania Uhuru Mzee Kawawa alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa Shirikisho la Wafanyakazi mwaka 1955 ambapo alichaguliwa kuwa Katibu wake Mkuu wa kwanza. Ni katika nafasi hii ndiyo aliweza kuanza kushiriki kwa nguvu zaidi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika akihamasisha wafanyakazi. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Serikali.

Februari 1956 Mzee Kawawa aliacha kazi yake ya Shirikisho la Wafanyakazi kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali kitu ambacho kilimkataza kuhusisha na siasa na kuamua kuingia katika harakati za kudai uhuru kupitia TANU. Alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU mwaka 1957, Makamu mwenyekiti wa TANU mwaka 1960.

Mwaka 1964 baada ya Muungano Mzee Kawawa alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais akiwa ni msaidizi wa Rais wa Muungano kwa upande wa mambo ya Bara.

Katika siasa amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo ile ya Ukatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM na amekuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM.

Mzee Kawawa alikuwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto nane na mojawapo ya kazi zake za awali ilikuwa ni uchezaji wa filamu za uhamasishaji na akawa ndiye mcheza filamu wa kwanza kiongozi mweusi (lead actor).

Mzee Kawawa alikimbizwa hospitali hapo jana kutokana na hali yake kuwa mbaya na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi; ambapo mapema leo asubuhi alifariki dunia. Mipango ya mazishi inaandaliwa.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Pema Peponi, Amina.

Imeandikwa na: Mwanakijiji

Ni huzuni na masikitiko makubwa kwa Watanzania sote. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amim\na.
 
Tulikupenda sana lakini Mwenyezi Mungu ameamua kukupenda zaidi! Raha ya milele ikuangazie ewe Simba wa Vita. Wanamsimbazi tunakukumbuka kwamba ulikuwa ni mwenzetu wa UKWELI.....
 
Alikokwenda Kawawa ndiko sote tunakoelekea kwa zamu. Mungu atufungue akili za mioyo yetu tutambue hilo na kijiweka sawa tayari kwa safari ya mwisho isiyo na mawaa. Ameacha kumbukumbu nyingi zinazostahili kukumbukwa. Sisi tulimpenda sana, lakini Mungu alimpenda zaidi. Jina la Bwana libarikiwe, Amen.

Leka
 
Wana BOIZIA (Tabora School) tumepoteza mpiganaji Mzee wetu,Simba wa vita Mzee Rashid Mfaume Kawawa! Mzee Kawawa utaishi milele kwenye mioyo yetu japo umepumzika kimwili kwa sasa.Wana BOIZIA wenzangu mtakumbuka kuwa Mzee wetu Rashid Kawawa na Wenzake ndio waasisi wa ORCHARD enzi zile za Warsal na Berlin na hata tulipokuwa pale camp tulinong'onezwa kuwa Hayati Bibi yetu Sophia Kawawa walikutana kule.

Huyu alikuwa JABARI hata Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukiri katika Kitabu chake cha UONGOZI NA HATIMA YA NCHI YETU kuwa watu kama kina Kawawa HUZALIWA kwa nadra sana!

Poleni Watanzania wenzangu!! Poleni sana wana BOIZIA popote mlipo duniani !!!!
 
Ni huzuni na masikitiko makubwa kwa Watanzania sote. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amim\na.

RIP Simba wa yuda, uwasalimie ..Sokoine, Nyerere, Kreluu uwaambie mwenzao Kingunge siku hizi ni bilionea wa kutupwa na ameasi ukomunisti pia ukatuombee wadanganyika wote tubadilike akili zetu na zifanane na watu wa kikwelikweli, na ukawaombee mafisadi safari yao wafike haraka segerea, Mungu akulaze mahali pema peponi...Amina
icon3.gif
 
........................Nani kauona mwaka, kamaliza mwaka...... NI MAJALIWA YAKE MUNGU KUUONA MWAKA (Quoted from DDC Mlimani Park Song)!
 
TBC Wanarun program zake za zamani, hivi sasa anahojiwa na David Wakati. Natumaini pia tutapata fursa ya kuiona tena ile filamu ya 'Fimbo ya Mnyonge'. Mimi niliiona mwaka 79 pale Viwanja vya Tangamano, mjini Tanga wakati huo wakiita Sinema za Dezo.

Sasa Kawawa anaeleza Alipoingia Tanu, 1956, mwaka mmoja baada ya David Wakati kuajiriwa TBC ile ya Mkoloni.

RIP SIMBA WA VITA.
 
Back
Top Bottom