Mzigua90
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 38,405
- 88,870
Pole Paula, mie sio mchangiaji sana ila kwa uzi huu nimeshawishika, hali unayopitia ilinikuta pia 05.01.2019 Daktari aliponijuza kuwa mgonjwa wangu ambaye ni mama mzazi hana zaidi ya masaa 24 atafariki kwa saratani ya kongosho(pancreatic cancer), hapo nilikuwa Nina miezi 4 na muuguza nipo nae, na nikiona dalili kuwa yupo ukingoni, nilijitia moyo nikamuondoa hospital , tulipofika nyumbani tuliomba na kumkabidhi kwa Mungu, tarehe Saba usiku saa 4 tuliimba wimbo wa Usinipite mwokozi na chakutumaini Sina, Kisha tukaomba na kumwombea, nusu saa baadae akakata Roho, nikipata uchungu maana alikata roho nikiwa namuona, lakini nilijitia moyo kuwa Kapumzika kwa AMANI. Ushauri wangu Kila Aina ya cancer ina life span yake, nyingine miezi 24, nyingine miezi 4 tu. Hivyo muwekeni mkononi mwa Mungu na mumkabidhi Mungu yeye ndio mwanzilishi na muhitimishi wa Safari yetu.
Uwezo wa binaadamu unapofika kikomo ndio Uwezo wa Mungu hujitokeza ili kuonyesha kua yeye yupo na anaweza tenda miujiza katika hali yoyote ile..
I believe maneno ya daktari sio tiketi ya kifo cha mama..Mungu yupo ndio anayetambua hatima yake.
Mungu yupo nae naamini atalishinda hili.
Poleni sana..
Salini na kuomba bila kuchoka..
Mungu ni mwema wakati wote
Hon, Ni ngumu sana kwetu kulipokea hili.Paula Paul, Dah Serious nimelia mimi naliaga sana nmevaa viatu vyako Paula Paul mimi nikiwa nasafiri napokuwa namuaga mama uwaga nalia sana ngoja nmpigie simu nimefikiria siku akiondoka nmewaza Mbali sana Mungu Wa mbinguni mcheck huyu dada Paula kwa jicho lingine yeye na Mama mgonjwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Ms mol, Asante sana.
Hon, Ni ngumu sana kwetu kulipokea hili.
Naumia, nikimfikiria yeye. Vile anakuwa anaweza kwenye akili yake jee ni mawazo gani yanamjia.
Najua ana huzuni sana moyoni akifikiria ijumaa hatoiona.
Na kinachoumiza zaidi yupo kutoa maelekezo tuu like "kitu Fulani nimekiweka sehemu Fulani msije mkakitafuta sana" , "uende kwa Fulani niliacha mzigo wa mdogo wenu kwa ajili ya shule". Leo palivyopambazuka tuu ametuambia tukamtafute fundi wa kurekebisha sink la jikoni (nyumbani) kwamba linavujisha maji.
Ni vitu ambavo vinauma na unaona ni namna gani anatamani angeendelea kuwa hai.
Asante hon
Natamani hata nisingejua. Tuendelee kupambana hadi mwisho.Daktari, daktari , angenyamaza tu bila kuwaambia lakini kusibiri kifo aaah, inatia huzuni nyingi sana, poleni sana kwa kuuguza na poleni kwa kuwa stressed kuliko hata mgonjwa mwenyewe!
Asante Karunzi.Poleni sana, Mungu atawapa faraja yake halafu Kifo kina siri kubwa wakati mwingine Madaktari wanakosea
Daash...Hon, Ni ngumu sana kwetu kulipokea hili.
Naumia, nikimfikiria yeye. Vile anakuwa anaweza kwenye akili yake jee ni mawazo gani yanamjia.
Najua ana huzuni sana moyoni akifikiria ijumaa hatoiona.
Na kinachoumiza zaidi yupo kutoa maelekezo tuu like "kitu Fulani nimekiweka sehemu Fulani msije mkakitafuta sana" , "uende kwa Fulani niliacha mzigo wa mdogo wenu kwa ajili ya shule". Leo palivyopambazuka tuu ametuambia tukamtafute fundi wa kurekebisha sink la jikoni (nyumbani) kwamba linavujisha maji.
Ni vitu ambavo vinauma na unaona ni namna gani anatamani angeendelea kuwa hai.
Asante hon
Dear,Paula Paul,
dear Paula,
Poleni sana mama angu, Nimejaribu kuvaa viatu vyako nimeshindwa mumie vinanipwaya hasa, nimepita kwenye hii thread nimelia sana Leo, how can you be this strong?
Mungu akawatie faraja ya kipekee itokayo kwake, akawape amani yake na damu ya Yesu ikawafunike, baraka na furaha vikawe mioyoni mwenu daima!
Nitawaweka kwenye maombi yangu, Mungu akawatetee katika kipindi hiki kigumu! Nilikuwa na mawazo yangu ila nilipokutana na huu uzi wako Paula, nikamuambia Mungu anisamehe sababu kumbe jambo langu ni dogo watu wanapitia nyakati ngumu sana!
Kila nikiwaza siku nipitie wakati mgumu kama huu, nijue kabisa namuhesabia yule mwanamke masaa ya kuishi, Eeh' Mungu wangu sitaki hata kufikiri hili!
Pole sana Paula, Pole sana jamani Mungu pekee akakufariji kwa namna ya ajabu, Wewe ni jasiri sana!
Ipo siku yule Mfariji Mkuu atatufuta machozi na haya mateso na maumivu yote yatafikia kikomo!!
Inatosha. Usiendelee kusimulia pleaseDear,
Asante sana kwa maneno ya faraja na kwa pole.
It sucks. Kumuona tuu kwenye kitanda, kakonda kabaki mifupa. She was cute back then na mnene. Lakini sasa amekuwa mifupa tuu. Hii inaumiza zaidi.
Baada ya kupata taarifa kwamba hatopona, alitaka wamrahisishie kwa kumwondoa duniani mapema ili asituone tunavyo umia.
Tukamwomba kwamba we still need her..aache wakati wake ufike. Akakubali.
Sasa hivi anatuchagulia tuu picha ambayo itatumika kwenye funeral, ungemwona anavyochambua hizo picha anajisemea "hii nilicheka sana haifai, hii nguo ilikuwa mbaya" ndio zoezi analolifanya. Na pia anadondosha machozi kwenye macho yake ambayo yamedumbukia ndani. Najua anawaza alivyokuwa na afya , nzima na kwenye furaha na sasa mambo yamebadilika.
Sasa hivi tunapeana shift za kwenda nje, ukitoka nje unalia hadi unatosheka unarudi ndani tunaendelea kufurahia. Lakini mama anajua anasema tunalia lakini tunamdanganya hatulii.
Leo anataka aende nyumbani. Hapa kwenye care centre wameshadhibitisha amebakiza masaa kadhaa. Anataka kama ni umauti umkute kwenye kitanda chake anacholala na baba. Tunamsubiri Baba, aje ila anachelewa , tunajua ni kwa sababu hana ujasiri wa kumtizama mama na pengine analia hadi machozi yaishe ili akimwona asilie.
Kwa sisi watoto hamna anayetaka kucheza mbali zaidi ya huyu mdogo wetu ambaye amesema hawezi kamwe kumshughudia mama yake akiondoka.
Huyu ameshatafutiwa phycologist kwa sababu unaonekana kutokupokea matokeo vizuri.
Asante kwa kuwa hapa, nina unafuu na Nina ujasiri sasa wa kusema namruhusu mama apumzike baada ya kuumaliza mwendo.
Dear,

Natamani hata nisingejua. Tuendelee kupambana hadi mwisho.
But now, tunahesabu masaa.
Natamani niweze kusimamisha masaa.
Ila mpaka sasa hamna mwenye wazo la kuandaa Mazishi, kila mtu anaona kama ni ndoto na ataamka ndotoni.
Asante Sana
Pole sana mpendwa. Mungu awape ujasiri wewe na familia yako wote katika kukabiliana na wakati mgumu mlionao wa kumfariji mama yenu anapongoja dakika zake za mwisho. Viatu vyenu ni vikubwa mno wengine hatuwezi kuvivaa, yaani daaah!Pancreatic cancer. Thank you Beca.