jamani rafiki etu
Paula Paul kafiwa na Mama yetu embu tuzidi kumuombea kwa Mungu aendelee kuwafariji yeye na familia yake binafsi nimesikitika sana ngoja tuwasiliane tujue msiba uko wapi
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ameumaliza mwendo tutaonana asubuhi ile njema iwapo amelala upande wa Bwana. Mungu aijuaye huzuni awafariji familia nzima katika kipindi hiki cha majonzi. Neno la faraja kutoka 1 Wathesolanike 4
13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo