My mother is dying of Cancer

My mother is dying of Cancer

Status
Not open for further replies.
Kasie,
Dear Kassie.
Hii msg imeniliza. Nimelia sana sikutegemea kupata upendo wa namna hii hapa ndani.
Sikutegemea kama ungekumbuka kuna siku niliandika kwenye Uzi wako kuhusu mama. Kitendo cha wewe kukumbuka pamenifanya macho yangu kutiririsha machozi kama bomba.

Ndani ya ID fake lakini kuna mtu ambaye ana upendo wa dhati.Nashindwa kujizuia. How I real wish tungekuwa siblings. Nahisi hata maumivu niliyoyapata nisinge yapata.

Mama yupo nje ya Tanzania. Asante kwa kuonesha nia na upendo dear.
Thanks for these hugs, nimemsomea hadi mama amefurahi sana. Amefurahi kwamba ataondoka lakini kuna watu wema ambao bado watakuwa wananifariji.

Ni kweli anapitia maumivu mahali, ila anajikaza sana. Mpaka sasa anaweza kutumia simu yake kuchat na kuongea kwenye simu ambapo hauwezi kuamini kama ni mgonjwa.

Mpaka sasa hali yake imebadilika na unaonekana mwenye nguvu sana, anaimba Gospel na anacheza (kujitikisa ile). Anaweza kusoma pia Biblia. Unaweza hizi anapona ila hapa doctor anasema mgonjwa wa cancer kwenye hatua za mwisho huwa anapata nguvu.

Ila kwa Mara ya kwanza ameshindwa kunitofautisha mimi na twin sister. Na sisi hatutaki kumtesa kuanza kumfundisha kutofautisha. Baba yetu ameshindwa kuvumilia kumwona mama kwenye hiyo hali, tunaomba Mungu pia tusije tukampoteza na yeye pia.

Pia kwa sasa hapendi watu wamshangae usoni. Sisi anatuangalia tukiwa hatumwangalii, tukimwangalia anatazama pembeni, hivyo tumeacha kumwangalia direct ili tumpe nafasi ya kutuangalia yeye hadi aridhike.

Ameniambia Leo nilale pembeni yake nimkumbatie. Nimelala nae kidogo ndipo nilipogundua mama amekonda sana hata uti wa mgongo umetokeza juu hamna nyama. Ninasubiri kwanza asinzie maana hataki nimshangae nilale nae tena.

Kwenye hiki chumba tupo wote tunalala na mama, kasoro baba ambaye madaktari wameshauri aondoke hadi masaa ya mwisho ndio aje. Wakionana wote wanalia inafanya mama achoke zaidi.

Mdogo wangu wa kiume kaleta maua ya Christmas na happy new year. Tumeyapamba hapa ndani. Mama kafurahi anatamani angetupikia chakula cha sikukuu. Sikukuu huwa anapika vyakula vingi na mdogo wetu wa kiume huwa anadeka anakaa na mama jikoni ili aonje. Mama anataka sikukuu wote tuwe nyumbani tumpikie mdogo wetu. Hatujui kama tutampa furaha anayoipataga kwa mama. Ila tutajitahidi.

Kasie Nakupenda. Asante sana.
Paula Paul Mimi binafsi Nashindwa cha kusema......... ila pokea hii video Dear...

So sorry Paula Paul i can feel you, and i know how it feels, i lost my grandma 3 yrs ago, it was breast cancer. May Almighty God gives you comfort kwenye kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana mama yetu kwa maumivu
Paula Paul kipenzi pole sana kwa kuuguza mama
Mungu wetu ni mwema na wa miujiza, anatuwazia mema hata katika nyakati ngumu
Mungu awape faraja na imani kuu sasa na siku zote
Mama D Asante. Asante kwa Faraja.
I needed this.
 
Pole Paula, mie sio mchangiaji sana ila kwa uzi huu nimeshawishika, hali unayopitia ilinikuta pia 05.01.2019 Daktari aliponijuza kuwa mgonjwa wangu ambaye ni mama mzazi hana zaidi ya masaa 24 atafariki kwa saratani ya kongosho(pancreatic cancer), hapo nilikuwa Nina miezi 4 na muuguza nipo nae, na nikiona dalili kuwa yupo ukingoni, nilijitia moyo nikamuondoa hospital , tulipofika nyumbani tuliomba na kumkabidhi kwa Mungu, tarehe Saba usiku saa 4 tuliimba wimbo wa Usinipite mwokozi na chakutumaini Sina, Kisha tukaomba na kumwombea, nusu saa baadae akakata Roho, nikipata uchungu maana alikata roho nikiwa namuona, lakini nilijitia moyo kuwa Kapumzika kwa AMANI. Ushauri wangu Kila Aina ya cancer ina life span yake, nyingine miezi 24, nyingine miezi 4 tu. Hivyo muwekeni mkononi mwa Mungu na mumkabidhi Mungu yeye ndio mwanzilishi na muhitimishi wa Safari yetu.
 
Pole sana Paula.
Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu kwenu.
Cancer is very stupid, last month one of my friends( twin brother's) lost their lovely mom, was there at the last moment yule mama anamaliza pumzi yake... Haielezeki.
I feel your pain Paula, Mungu akupe ujasiri .
Tell mom you love her so much!

Sent using Jamii Forums mobile app
Avriel, thank you.
It's comforting to know that I am not alone.
Thank you for being here. I am deeply thankful and blessed.
 
Pole sana dada Paula Paul kwa maumivu anayopitia mama!

Madaktari wanatibu lakini Mungu ndio anaponya. Afya, uhai na uzima unatoka kwa Mungu!

Kwa uwezo wa Mungu mama anaweza kuishi zaidi ya siku walizotaja madaktari! Mungu wetu ni mwaminifu. Nitaomba kwa ajili ya afya ya mama yetu!
How we wish angeuona mwaka ujao.
Angesherekea sikukuu nasi.
Najua anaumia sana, ila pia wote tuna imani kwamba Mungu atatenda.
Amen, Usifemoyo. Asante sana.
 
Pole Paula, mie sio mchangiaji sana ila kwa uzi huu nimeshawishika, hali unayopitia ilinikuta pia 05.01.2019 Daktari aliponijuza kuwa mgonjwa wangu ambaye ni mama mzazi hana zaidi ya masaa 24 atafariki kwa saratani ya kongosho(pancreatic cancer), hapo nilikuwa Nina miezi 4 na muuguza nipo nae, na nikiona dalili kuwa yupo ukingoni, nilijitia moyo nikamuondoa hospital , tulipofika nyumbani tuliomba na kumkabidhi kwa Mungu, tarehe Saba usiku saa 4 tuliimba wimbo wa Usinipite mwokozi na chakutumaini Sina, Kisha tukaomba na kumwombea, nusu saa baadae akakata Roho, nikipata uchungu maana alikata roho nikiwa namuona, lakini nilijitia moyo kuwa Kapumzika kwa AMANI. Ushauri wangu Kila Aina ya cancer ina life span yake, nyingine miezi 24, nyingine miezi 4 tu. Hivyo muwekeni mkononi mwa Mungu na mumkabidhi Mungu yeye ndio mwanzilishi na muhitimishi wa Safari yetu.

Nimeuguza wagonjwa lakini Cancer hapana ni kitu kingine jamani.
I lost my uncle 2017 and now my aunt yuko na third dose ya chemo first dose8, second 8 na wameongeza😢😢😢 kwa kweli niseme tuu ni Mungu mwenyewe anajua njia zake na hatma ya kila mtu
 
Uwezo wa binaadamu unapofika kikomo ndio Uwezo wa Mungu hujitokeza ili kuonyesha kua yeye yupo na anaweza tenda miujiza katika hali yoyote ile..
I believe maneno ya daktari sio tiketi ya kifo cha mama..Mungu yupo ndio anayetambua hatima yake.
Mungu yupo nae naamini atalishinda hili.
Poleni sana..
Salini na kuomba bila kuchoka..
Mungu ni mwema wakati wote
 
Back
Top Bottom