Paula Paul,
dear Paula,
Poleni sana mama angu, Nimejaribu kuvaa viatu vyako nimeshindwa mumie vinanipwaya hasa, nimepita kwenye hii thread nimelia sana Leo, how can you be this strong?
Mungu akawatie faraja ya kipekee itokayo kwake, akawape amani yake na damu ya Yesu ikawafunike, baraka na furaha vikawe mioyoni mwenu daima!
Nitawaweka kwenye maombi yangu, Mungu akawatetee katika kipindi hiki kigumu! Nilikuwa na mawazo yangu ila nilipokutana na huu uzi wako Paula, nikamuambia Mungu anisamehe sababu kumbe jambo langu ni dogo watu wanapitia nyakati ngumu sana!
Kila nikiwaza siku nipitie wakati mgumu kama huu, nijue kabisa namuhesabia yule mwanamke masaa ya kuishi, Eeh' Mungu wangu sitaki hata kufikiri hili!
Pole sana Paula, Pole sana jamani Mungu pekee akakufariji kwa namna ya ajabu, Wewe ni jasiri sana!
Ipo siku yule Mfariji Mkuu atatufuta machozi na haya mateso na maumivu yote yatafikia kikomo!!