Tamko kuhusu JamiiForums kuendelea kuzuiliwa kupatikana nchini Tanzania

Tamko kuhusu JamiiForums kuendelea kuzuiliwa kupatikana nchini Tanzania

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,247
Reaction score
5,731

TAARIFA KWA UMMA

Mnamo Septemba 6, 2025, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilisitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums na kuzuia upatikanaji wa jukwaa kwa siku 90, kwa madai ya ukiukwaji wa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta. Pamoja na kutambua athari kwa haki ya wananchi kupata taarifa na kutoa maoni, tulitii agizo hilo hadi huduma ziliporejeshwa Desemba 06, 2025.

Tangu kurejeshwa, tumepokea taarifa kutoka kwa watumiaji wetu wa Tanzania kuwa kuanzia Desemba 7, 2025 hawawezi kufikia jukwaa bila kutumia mbinu au nyenzo za ziada.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa hatuhusiki na hali hii, na tunalaani vikali kitendo cha kuzuia upatikanaji wa jukwaa bila taarifa rasmi kwa umma, kwani ni kinyume na ukiukwaji mkubwa wa haki ya kutafuta, kupokea na kutoa taarifa.

Tunatoa wito kwa yeyote au mamlaka yoyote inayohusika kuondoa mara moja vizuizi hivi na kuruhusu wananchi kupata huduma bila vikwazo.

Tutaendelea kusimamia haki za kidijitali na uhuru wa watu kujumuika mtandaoni, kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, na kuhimiza uwajibikaji katika jamii.

Desemba 12, 2025

20251212_213632.jpg
 
Mambo kama haya ndio maana watu wanagoma nakufanya maandamano!

Hili taifa lina viongozi washamba sijapata kuona sijui hata wanaogopa nini kusemwa kwenye uongozi kupo tu hata baba anasemwa kwenye familia sasa nyinyi ni kina nani...?

Kama hivi ndivyo mnavyoendesha mambo basi tarajieni migomo na maandamano zaidi na zaidi maana sikio la kufa halisikii dawa!.
 
Msikate tamaa, msivunjwe moyo uongozi na wafanyakazi wote wa JF.
Yatapita haya, Yana mwisho.

Nawafikiria wadogo zangu walioajiriwa na JF.
Revenue ikishuka na wao Wanaathirika.
Hakuna matangazo ya ndani (local) ya kulipia bills.

Uongozi ukiomba msaada wa wahisani watapewa kesi ya uhujumu uchumi, kutakatisha pesa.
Au uhaini wanatumiwa na wahisani toka nje.
 
Dah inasikitisha lakini ndio hivyo.Hili lilikuwa wazi toka mwanzo walipofungia.

Kwa watumiaji ambao hampendi kutumia VPN(kosa kisheria).Tumia JF web version pia tumia operamini kama browser(ukiingia usifute browsing history au ku-clear cache) ndio salama yako na utaipata JF wakati wowote
 
Ko basi tu ila machawa wao wote wangepigwa pini wasiingie kuibrand serikali yao dhalimu humu.

There's no point kucheka na machawa wa ccm humu wakati serikali yao katili imefungia watu kujumuika kidijitali.

Mods acheni ujinga, ban them fvckers!!
 
Back
Top Bottom