Sekta ya Mawasiliano Tanzania (Q4 2025)

Sekta ya Mawasiliano Tanzania (Q4 2025)

Bwege2030

Member
Joined
May 10, 2025
Posts
90
Reaction score
186
SEKTA YA MAWASILIANO TANZANIA (Q4 2025)

jumla ya usajili wa simu za mkononi ulifikia milioni 106.9 kufikia Desemba uku ongezeko la matumizi ya simu janja (smartphone) lilipanda hadi 41.82%,ufikiaji wa huduma ya 5G ulifikia 30.1% ya idadi ya watu, na wastani wa kasi ya mtandao wa simu ulikuwa Mbps 30.30.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa Takwimu za Mawasiliano kwa robo iliyoishia Desemba 2025.

Usajili wa simu iliongezeka kwa 7.7% kutoka milioni 99.3 mwishoni mwa Septemba 2025 hadi milioni 106.9 kufikia Desemba 2025.
Usajili wa Simu za Mkononi na Laini Maalum (Fixed)Q4 2025

Oktoba: 102,334,091
Novemba: 104,662,248
Desemba: 106,935,201
Vodacom inaongoza soko kwa 31.2%, ikifuatiwa na Yas ( 28.9% na Airtel 21.8%.


Mobile Network Coverage
Uwekezaji katika miundombinu umeongeza usambazaji wa huduma Kufikia Desemba 2025, ufikiaji wa teknolojia mbalimbali kwa idadi ya watu ulikuwa kama ifuatavyo
2G: 98.6%
3G: 93.9%
4G: 94.2%
5G: 30.1%
Idadi ya minara ya mawasiliano iliongezeka kutoka 9,745 Septemba 2025) hadi 10,029 mwishoni mwa mwaka.

Huduma za Pesa kwa Njia ya Simu,Mobile Money.
Usajili wa huduma za pesa kwa njia ya simu uliongezeka kwa 6.7%, kutoka akaunti milioni 71.7 mwezi Septemba hadi milioni 76.5 mwezi Desemba 2025.

M-Pesa (Vodacom) inaongoza soko kwa 41.18%.
Mixx (Yas) na Airtel Money kwa pamoja na M-Pesa zinamiliki 89% ya soko.
uku jumla ya miamala ya pesa kwa njia ya simu kwa mwaka 2025 ilikuwa bilioni 6.3, ongezeko la 68.7% ikilinganishwa na mwaka 2024.


Kukiwa na ongezeko la 3.2% ya usajili, kutoka milioni 56.3 Septemba 2025 hadi milioni 58.1 Desemba 2025.
99% ya watumiaji wanatumia mtandao wa simu za mkononi,mobile wireless,
Fiber - FTTH/FTTO bado ina watumiaji wachache takriban 140,000 kwa pamoja.
uku wastani wa kasi ya download ni 30.30 Mbps
 
Back
Top Bottom