Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Mwingira amlaani mchungaji Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:32 0diggsdigg

Elizabeth Suleyman
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. “Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.

“Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,”alisema Mwingira.

Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. “Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.
Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka,” alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.

Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.
“Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,”alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

“Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira. Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara."

Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.

Pengo alisema: “Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion’ na baadae watu wakapata madhara makubwa.

“Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,”alisema. Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao


wakati yeye mwenyewe anawatoza waumini sadaka
 
Another confusion in my mind....

Kumbe wachungaji wanalaani na kutata mtu afe! duu....
 
Bila kusahau ukatende mema, nafikiri hii haina shida kama kule kwa kakobe ambako anathubutu kusema kuwa wakati wa yesu umepita na sasa ni wakati wa kakobe, je inamaana yeye ni sawa ya yesu?

Ukweli ni kwamba hii ni dawa aliyooteshwa awape watu na si kuwahubiria.yeye hana sababu ya kukiuka yale aliyoambiwa.na ni lazima kama wewe ni mkristo ujue si kanisa,mchungaji,nabii,papa au katekista atakayekupa uzima wa milele.aanachofanya babu ni kutoa dawa na angekua na ulafi kama wa mwingira na kakobe angeweza sana kuwasumbua watu kwa kujikweza na kuringaa sana na hii dawa.cha msingi kama una shida na unaamini dawa inaponyesha basi unaweza kwenda maana hakuna anayelazimishwa au kuambiwa ajiunge na kanisa la mchungaji.jamani tuone tofauti hapa na makanisa haya ya mazingaumbwe na madaha.
 
Hana lolote...sadaka zimepungua kanisani kwake ndomana amepagawa....kama namwona vile alivokua anatoka jasho na mishipa kumtoka....ile benki ndo itafulia kwa jina halisi la yesu mnazarethi....ile dhamana ya b.o.t ya billion 5 aliitoa wapi??? Ashindweeeeeeeeeeeeee
 
mahubiri haya yako very light kwa mtu anayejipachika vyeo vingi kuwa ni nabii na mtume. Mbona yeye huchangisha fedha na kumkabidhi mkewe?
 
Mwingira amekosa wagonjwa wa kuwaombea ili apate sadaka, wote wametimkia LOLIONDO kwa BABU na wamepona teh teh teh pole sana Mwingira teh teh teh:lol::lol::lol::lol:
 
hawana lolote wanaona ni tishio kwao kukosa waumini na sadaka.
"Naogopa kwenda kanisani kwakuwa sina sadaka":shock:
 
Mimi sijategemea kabisa kama Ambilikile angepata upinzani kutoka kwa viongozi wa dini ya Kikristo.
 
Tanzania imegeuka uwanja wa vita! CCM Vs CDM, na sasa Mwingira Vs Loliondo!!
Nijuavyo mimi hakuna wachungaji wezi wa pesa za waumini kama Mwingira, Kakobe na Mama Lwakatare! sasa wateja wao wamekimbilia Loliondo, kelele zimeanza!!
 
Yaani Mwingira anaweza kuthubutu kusema babu ni Mwizi???????? Ama kweli Mwingira hana haya! Hivi kuna mwizi kama yeye anayeendesha magari ya kifahari, mashamba, kafungua benki kwa kuchakachua sadaka maana analazimisha fungu la kumi amejenga majumba ya kifahari maana inasemekana ukifika kwake hutaamini kwa jinsi alivyo jenge mijumba ya kifahari.... je kama kweli yeye ni nabii amesaidia watanzania wangapi wenye shida....??? Mimi naona Mwingira na mwenzie Kakobe wasiwasi wao mkubwa ni kukimbiwa na wateja!!!!!
Babu wa Loliondo Mungu akutie nguvu uendelee kuwasaidia wa tanzania na ulimwengu wote!!!!
Kwanza huo unabii kapewa na nani kajipachika two kwa kifupi hizo laana zitamrudia yeye mwenyewe!!!!!

Nimechekeshwa sana na mchangiaji hapo juu aliyesema Mwingira na Kakobe wapigwe Radi!!! teh teh teh teh
 
Tanzania imegeuka uwanja wa vita! CCM Vs CDM, na sasa Mwingira Vs Loliondo!!
Nijuavyo mimi hakuna wachungaji wezi wa pesa za waumini kama Mwingira, Kakobe na Mama Lwakatare! sasa wateja wao wamekimbilia Loliondo, kelele zimeanza!!

umeona eeeeeeeeeeeh?

lakini hata mimi babu simkubali na wala sijawahi kuhisi kwenda huko.

only those desperate and unfaithful will go there.
 
Tanzania imegeuka uwanja wa vita! CCM Vs CDM, na sasa Mwingira Vs Loliondo!!
Nijuavyo mimi hakuna wachungaji wezi wa pesa za waumini kama Mwingira, Kakobe na Mama Lwakatare! sasa wateja wao wamekimbilia Loliondo, kelele zimeanza!!

point of collection kwenye red:ccm,cuf,nccr,tlp,udp Vs CDM
 
umeona eeeeeeeeeeeh?

lakini hata mimi babu simkubali na wala sijawahi kuhisi kwenda huko.

only those desperate and unfaithful will go there.


Bora wewe kama humkubali lakini haujamkashifu Babu. Na ujue kwa vile huna imani hata ukienda wewe hatakusaidia chochote kinachokuponya ni imani.
Ni vizuri kusema unayoyasema lakini nakushangaa kidogo unaposema "only those desperate and unfaithful wataenda huko.... ndugu yangu hujafa hujaumbika.

Wanasema ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu mpe Mungu.......................
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
umeona eeeeeeeeeeeh?

lakini hata mimi babu simkubali na wala sijawahi kuhisi kwenda huko.

only those desperate and unfaithful will go there.


Bora wewe kama humkubali lakini haujamkashifu Babu. Na ujue kwa vile huna imani hata ukienda wewe hatakusaidia chochote kinachokuponya ni imani.
Ni vizuri kusema unayoyasema lakini nakushangaa kidogo unaposema "only those desperate and unfaithful wataenda huko.... ndugu yangu hujafa hujaumbika.

Wanasema ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu mpe Mungu.......................
 
jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

tusaidiane please

Glory to God

Unaweza kuwa na point Miss, lakini hebu fikiria kwa nini idadi ya wanaokwenda huko inongezeka kila siku? Pamoja na mashaka juu ya uponyaji huo lakini ukweli utabaki kuwa watanzania wengi wanaamini katika majibu rahisi kwa kila tatizo pasipokuweka juhudi za kutosha.

Ndio maana tuliposikia ukiweka mbegu DECI hela yako inazaa haraka na tukaamini!
 
Hawa wahubiri hasa ambao wanang'ang'ania kuhubiri injili dar es salaam tu wana mambo ya ajabu sana na wanajiona wao wako sahihi kwa kila kitu kumbe ni kutaka sadaka na changizo tu.

Yesu hakuwa na taahira ya akili aliposema watatenda miujiza,watatoa mapepo,watahubiri,wataponya magonjwa n.k lakiani yesu atasema siwajui ninyi mtendao maovu...mantiki hapa ni kwamba kukubalika na Mungu hakutategemea miujiza na hata kutoza zaka au changizo, hawa wanaojiita mitume na manabii wanadhani sisi hatujui mwisho wa yote nao wanaweza kukataliwa na yesu kristo.


Na kuhusu babu wa loliondo ni kama wao tu anaweza akahukimiwa bila kujali kwamba hiyo huduma amepewa na Mungu au laa sasa Mwingira yeye ni nani aanze kutoa hukumu kwa babu...tumewajua wezi wa pesa zetu hao na hata kakobe naye aliropoka hivyohivyo tena bora yababu anaonyesha mgawanyo wa pesa zake je,wao zinaenda wapi?



kipimo utakachotumia katika kutoa hukumu nawe utahukumiwa kwacho
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom