Mwingira amlaani mchungaji Loliondo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by PayGod, Mar 16, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

  Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. "Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.


  "Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,"alisema Mwingira.


  Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. "Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.


  Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka," alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.

  Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.


  "Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,"alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

  "Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira.


  Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion' na baade ikaleta madhara."

  Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.


  Pengo alisema: "Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion' na baadae watu wakapata madhara makubwa.


  "Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,"alisema.

  Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.
   
 2. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Aache wizi nae Mwingira, basi na yeye asingekusanya michango kanisani. Tena kwa kupanga watu kwa mafungu ili wanaotoa sana waonekane! Haya makanisa mengine biashara tupu.

  Wale vijana wa babu wanaoenda kumtafutia dawa wataishije? Umeona nyumba anayoishi babu? Yeye yake ni 100 kati ya 500 bado mnaona anapata nyingi?

  Kweli mashetani ni wengi humu duniani,tutaishi na kuona mwisho wenu..
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mwingira aache upumbavu wake hapa. Atoe bure akale wapi kama mtu kutwa nzima anashinda anatoa dawa. Mbona yeye waumini wake wanatoa sadaka zinazomfanya awe na nguvu hata kubwabwaja hivyo! Kwa nini asitoe hiyo huduma yake ya kiroho bure?! Mtu wa Mungu kumshambulia mwenzie ni ukosefu wa imani na hekima.

  Mtu gani anayejiita nabii halafu anamtusi mwenzie kuwa ni sawa na DECI. Tatizo la viongozi wa kidini wa aina ya kina mwingira ni kiburi cha imani. Wanajifanya wao ndiyo wao na ndiyo maana ukimsikia askofu kakobe utashangaa mahubiri yake yanalenga kumsema mzee wa upako, ukimsikia mwingira naye utaona anamsema askofu kakobe, ukimsikia mzee wa upako naye utashangaa anampiga vijembe askofu kakobe.

  Kwa ujumla, viongozi wengi wa dini kama akina mwingira ni wasanii tu. Mimi narudia maoni ya mwingira ni upuuzi na wivu wa kijinga.
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mwingira ni mfanya biashara kwa kutumia nguvukazi ya waumini wake. Hana jipya na ni myonyaji mamboleo.

  Anashauriwa aendelee na biashara yake ya Efatha Bank na mashamba ya kule Rukwa ili apate fedha zaidi.

  Aache watu wa Mungu wanaofanya kazi waliyotumwa kuifanya hapa duniani.

  Yeye amejituma kutafuta fedha, na azitafute mpaka aridhike nazo.

  Watu wengi wamechomoka pale kwake Mwenge baada ya kutumika kwa muda mrefu kama nguvukazi ya bure.

  Kwa hilo atahukumiwa.
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Lazima hao viongozi wa Dini wamwogope BABU!! Anawamalizia waumini wao, as a result SADAKA makanisani mwao zinapungua!!
   
 6. v

  valour Senior Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hayo ni maneno makali sana kutoka kwa mtumishi wa Mungu. Hata kama hakubaliani na Mchungaji Ambikile Mwasapile kuna jinsi ya kusema. Biblia inatufundisha tuwaombee na kuwabariki adui zetu. Sasa hata kama adui ni wakuombewa, yeye iweje amlaani? Jamani tutawajua watumishi hawa kwa matendo yao. Ee Mungu wa neema kikombe chako cha rehema kamwe kisikauke
   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  ... Very very intersting!!
   
 8. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  mwingira,kakobe etc biashara yao imewekwa matatani na babu. Kaona mia tano ni nyingii. Yy anawachukulia waumini wake kiasi gani mpaka akawa tajiri hivyo. Mpaka kafungua benki du! Hapo lazima waumini wanalazimishwa kuweka na kukopa.
   
 9. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli Mwangira,Kakobe na wengine wanaofanana na hawa wanaojiita manabii,inatakiwa wakati wakifikiria mawazo ya kw Babu wapigwe na radi
   
 10. e

  ejogo JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asilimia kubwa ya watu wanakwenda kwenye makanisa kama ya Mwingira kwakuwa wanamatatizo na tatizo kubwa ni la kiafya. Wanakwenda huko kwa matumaini kwamba wataponywa kimwili. Babu amejitokeza na kuweza kuyaponya hayo magonjwa sugu ya kimwili na wale watu wengi waliokimbilia kwenye makanisa hayo kwaajili ya kuponywa kimwili sasa wanayakimbia na kwenda kwa babu. Mwingira sasa woga umemwingia kwani amekuwa akiishi kwa kuwategemea hao watu wanaokimbia.
   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wajinga ndio waliwao, ni kuwakamuwa tu! huyu mtume, huyu nabii huyu mganga, wenyewe kwa wenyewe wanaanza kugombana:ballchain: kwa jina la Bwana.
   
 12. Salathiel m.

  Salathiel m. JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwingila apo umekosa cha kusema,naamin ata usemeje babu atapiga kazi kama kawa! Sio kila kitu ukiskia lazma useme!
   
 13. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kuna matukio mengi sana ambayo tutayaona hasa katika hizi nyakati za mwisho
   
 14. L

  Leonard Mwanja Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mbona ww mwingira unaona mia tano mtu kutoa sadaka ndogo?Babu kakupiga bao ww endelea kufungua mabenki wivu wa nn?Ww na kakobe ni wezi kuliko babu na mnapenda kutukuzwa sana sijui nani kawapa huo utume na unabii.Nyie ndio Deci haswa
   
 15. I

  Igembe Nsabo Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu bwana amepungukiwa na Wateja wake ambao wengi walikuwa ni Wagonjwa wa malazi SUGU na kwa sasa wanakwenda kupata dawa kwa BABU, yeye anataka kubakia yeye tu akitengeneza pesa ili anunue Mashamba na kujenga Shule pekee! (awe Mch./Nabii na pia Mfanyabiashara/ Mwekezaji pekee??!). Aache UNAFIKI pale anapoona amezidiwa kete atafute njia nyingine ya kujiimalisha na si kumshambulia Mch. Mwasapile (BABU).
  Yeye ndie tunaye muona kama shetani kwanini amushambulie mwezeka! yeye halazimishi watu waende kwake watu wanakwenda na matatizo yao na wala hajitangazi kwenye TV kama yeye, ila watu wanapata promo kutoka kwa watu wanao pata huduma hiyo, kama akina MREMA wanapopata Tiba na kwenda kwenye TV na kutoa ushuhuda!
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

  hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ ni uchungaji gani huu?

  Mungu anapewaje utukufu hapo?

  tusaidiane please

  Glory to God
   
 17. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hawa kina mwingira na kakobe wake mi nawaona majizi tu kudadadeki.
   
 18. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135

  kwa staili hii vilaza hawatakaa waishe.
   
 19. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  mwingira, kakobe, rwakatare, mzee wa upako (wa giza) and co. wote ni wezi na wanyang'anyi
   
 20. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwingira anatimiza lile andiko la enzi za Ayubu kipenzi cha Mungu. Ayubu naye alisemewa mengi mabaya na marafiki zake ambao nao walikuwa wanapiga vifua vyao kwamba wanamjua Mungu sana kuliko hata Ayubu hao ni Eliphaz, Bildad na Zophar. Kumsema Ayubu walikuwa wanaegemea Jina la Mungu pia. Lakini mabishano yao hatimaye Mungu mwenyewe akajatoa hitimisho kwa kwaambia live watu hao kwamba wao ndio wamekosea na Ayubu ndiye aliyesema kweli kuhusu Mungu, akawarudi na kumpandisha juu sana chati Ayubu (Ayub 41:8-9) unaweza kusoma mlango mzima ukipata nafasi. Biblia Takatifu ambayo Mwingira anapata upofu kuiona inasema hivi: "Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwainua wanyenyekevu wa moyo"

  Anayo haki kuongea Mwingira anayejiita Nabii na Mtume mfanya biashara maarufu nchini anayetumia nguvu kazi ya wale wanaomwendea kumsikiliza kwenye viunga vyake alivyowekeza, ambaye naambiwa anatembelea gari lenye zaidi ya milioni 200 katikati ya waumini wake masikini kabisa, akikusanya kila senti kutoka mifukoni mwao kwa jina la sadaka kwa Mungu na kujinufaisha yeye mwenyewe, akiwachukia wote wanaoinukia kutumiwa na Mungu kwa kuwa hawatoki kanisani kwake, akikandamiza uelewa wa walio chini yake wasijenyenyuka wakampita yeye. Anatafuta umaarufu huyo, anahofia watu watamkimbia naye atamasikinika haraka. Roho za namna hiyo zipo nyingi na zitaendelea kuja tu, kama Kakobe naye anavyolinganisha tiba ya Loliondo na DECI. Wanafiki hao wala hawafai kusikilizwa. Roho ya Mungu hijipiganishi yenyewe. Kama kweli watu hao ni watumishi waaminifu wa BWANA, wangekuwa na hekima angalau kidogo tu kukwepa kuingia kwenye mtego wa kutafuta na kujilimbikizia sifa. Sio sahihi kkwao kumhukumu babu na kumpangia adhabu ya kifo kwa kusema roho inayodaiwa na Ambilikile kutoka kwa Mungu ikimtuma afanye anachofanya kutibu watu ni ya kishetani. Wamekuwa kama panya wamenaswa kwenye mtego ilhali walidhani wao peke yao ndio wanatumiwa na Mungu kupeleka habari za kheri kwa viumbe vya Mungu. Si ajabu kama Mungu atakuwa amewakataa hao kama Sauli alivyokataliwa na Daudi asiyetegemewa akapakwa mafuta na kuwa mfalme wa Israel. Sauli hakutulia kimya akatafuta kila njia amwue Daudi, lakini kwa kuwa MUNGU alitoa kibali kwa Daudi akafa Sauli mwenyewe baada ya kuingia mkenge kumwinua Nabii Samwel kutoka kuzimu na kusemezana naye, akapata maneno asiyotarajia. Ndivyo Mwingira na Kakobe wanavyofuata nyayo za kale pasipo wao wenyewe kufahamu.

  Kama kweli MUNGU ndiye aliyemruhusu Ambilikile Mwaisapila kufanya afanyayo, HAKIKA hatawaacha wamneneayo mabaya wadumu, bali atajilipiza kisasi kumtetea mja wake, kwa maana kisasi ni chake BWANA. Dhambi zote zinaweza kusamehewa, lakini kumkufuru Roho Mtakatifu KAMWE hasamehewi mtu, ndivyo KRISTO mwenyewe alivyoonya. Ikiwa Mwingira anamwamini KRISTO basi na ajitambue kwamba amepotea upeo, ajiangalie na kauli zake. Babu sijamsikia akihubiri watu waende kwake na wala hajitangazi ili watu wengi wamfuate. Wanaokwenda kutoa shukrani anawaambia waende kanisani kwao wanakosali wakatoe sadaka huko. Mwingira sasa naanza kuamini kwamba yanayosemwa kuwa jamii ya mateka wa kiroho inawezekana kuwa, kwa sababu kila anayemwamini Mungu anaweza kutenda dhambi sana tu lakini wanaogopa kumsema Mungu vibaya hata kwa utani. Jazba anayoitumia kumdhalilisha babu sio ya kawaida. Babu wala hajibu mapigo, anajua anachokifanya, yupo mtetezi wake atakayewashukia wabaya wake kama nyuki.

  Tumwachie Mungu anayejua kujitetea. Mwingira na Kakobe wana maisha ya peponi wangali duniani, wanawazuia wengine waione baraka za Mungu kwa vitisho vingi, waumini wao masikiniiiiiii wanaonuka kwa umasikini huo, lakini wamekusanya kila kilicho cha thamani na kuwapelekea watu hawa ambao chai ya rangi ni historia kwao, wakati waumini wao hata hiyo chai ya rangi wakiipata wanadhani ni muujiza. Jamani, mimi sijui tunapelekana wapi. DECI wanayodai waliiombea kufa na ikafa wanakosea, it was a situational circumstance. Miongoni mwa walionufaika na DECI ni waumini wao na labda hata wao wenyewe hao waropokaji. Hawataki wengine waone paradiso wakingali duniani kama wanavyoifaidi wenyewe. Lakini ole wao, maana wataangukia pua wasipojichunguza na kumlilia Mungu awasafishe nia zao mbaya na kuachana na kiburi cha rohoni, wakajivisha nafasi ya Uungu kama Shetani alivyofanya na akatelemshwa kuzimu. Wanapohubiri wasisahau kujihubiri na wao wenyewe, hata Paulo Mtume wa Kweli alijisemea asijewahubiri wengine wakaenda mbinguni na yeye akakataliwa. Paulo aliliona hilo ambalo Mwingira na Kakobe bado wamepofushwa. Utamwombeaje mtu kufa wakati anachokifanya hata wapagani wanakiri kwamba Mungu yumo kwenye huduma hiyo? Watajitenganisha vipi na wayahudi waliobobea kidini waliomsaliti Yesu na kumwua? Hao ndio aina ya Mwingira na Kakobe. Ona Pengo anavyotoa maoni kwa mashaka, anajua ubaya wa kupingana na Mungu, anatoa maoni yake kwamba hana cha kusema ila anabaki kushangaa, kwani akili yake inapingana na imani yake na kwa hekima aliyopewa na Mungu anasita kusema vibaya juu ya huduma hiyo hadi Mungu atakapomdhihirishia ukweli.

  Yatosha. Vipofu na waendelee kuwa vipofu, wenye macho na waendelee kuona, wanaomtafuta Mungu waongeze bidii na kumuuliza ukweli wa jambo hili naye atawajibu. ZIjaribuni kila roho.
   
Loading...