Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Bwana Yesu asifiwe,

Kwa kweli, Babu wa Loliondo na ndoto zake na dawa yake hakuna utukufu wowote anaopata Mungu aliye hai ambaye alijifunua kupitia neno lake Yesu Kristo. Kwa hiyo, watumishi wa Mungu kama Kakobe, Mwingira na wengine kupinga ni sahihi tu wala hawana kosa. Tatizo ni kwamba watu wamezama katika udunia na kusahau kabisa maisha ya utakatifu ndiyo maana wanatafuta ufumbuzi laini kwa matatizo magumu kitu ambacho hakiwezekani.

Cha kufanya ni kama mtu unaumwa dawa ni kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu; kama ukipona sawa na kama usipopona si unakufa na kwenda mbinguni. tusidanganyane hata ukinywa kikombe na kupona mwili je kesho ukifa utakwenda wapi? Na hata kama huumwi ugonjwa wowote kama mimi dawa ni kuishi maisha ya utakatifu wa kweli ndani ya Yesu tu.

Pia naomba tuwe wastaarabu tuache kuwatukana watumishi wa Mungu kwani tutavuna laana. Wao wanafanya kazi yao kwa kuangalia kila jambo kama linapingana na maandiko matakatifu ya biblia lazima walipinge tu kwani linatoka kwa yule mwovu.

Mwingira, Kakobe na wengine wanaopinga mambo ya Babu wa Loliondo mbarikiwe sana.

Nawasilisha.

Kuna kitu sijaelewa, watu humu mnapinga nini? kwamba dawa ya babu inatibu v/s haitibu?, au whether babu ni mtumishi wa Mungu v/s mtumishi wa shetani? watu wanachohitaji ni kupona, mbona hamuwapingi madaktari wanaotengeneza dawa kila siku? na zenyewe si zinatoka kwenye mitishamba? as long as mtu anamjua anayemuabudu mi sioni shida iko wapi, maana akipona siku zote sifa na utukufu atarudisha kwa Mungu alie hai, so long as hata Ambikile mwenyewe kakiri kwa jina la Yesu kuwa anatibu kwa jina hilo, na anamtumikia Mungu alie hai, hiyo inatosha kwa muumini wa kawaida hana hatia, msim underestimate Mungu kwa uelewa wenu wa kibinadamu. Pingeni na dawa za hospitali kwanza kwa spidi hii hii.
 
Waseme yote, walaani sana, wafundishe sana. Lakini mimi nitabaki nikisema hivi WAKATI UTAAMUA MAMBO.Tena mi noinavyoona waache wale wanaoiamini hiyo dawa ya babu wanywe na kama wanapona na wapone kabisa.

Hawa/sisi ambao tunamashaka nayo, basi tumuombee ulinzi wa Mungu uwe pamoja naye, na Mkono wa Mungu uhusike katika huduma nzima. Kama ni huduma ya uongo haitadumu!!

Kama ni ya Ukweli hata mkeshe na kufunga siku arobaini mchana na usiku haitakufa ng'o!!! Kwa sababu cha Mungu kinadumu. Kwa mtu anayemwamini Mungu na kumjua huyo Mungu anayemwamudu hapaswi kulaani wala kulumbana kwa sababu ya kitu ambacho kinamhusisha Mungu ndani yake.

Tunadhani Mungu ameshindwa kazi kiasi hicho? Tunadhani Mungu anahitaji wewe na mimi mtetee ktk kazi zile zifanywazo kwa jina lake kiasi hicho?
Tunadhani Mungu haoni uongo au ukweli wa mambo yafanywayo na mwanadamu chini ya jua hili?

Hapana Mungu hajafilisika kiasi hicho, wala hatuwezi kumsaidia kazi hata kidogo. Mwenye ufahamu na amuombee Babu tu, uwepo wa Mungu umzingire. Palipo na nguvu ya Mungu uongo lazima udhihirike tu!!! Na ukweli unadumu daima.

Ndivyo moyo wangu unavyonambia mimi. TIME WILL TELL!!!!

Very useful post, tusimsaidie Mungu kwa werevu wetu wa kidunia. Anaona, na anajua kila kinachoendelea, its just a matter of time for us to know mchele na pumba.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Its is difficult to tell who is right and who is a liar, bt believe it or not! some of these RIDICULOUS GOOD FOR NOTHING SHAMELESS PASTORS use satanic power to perform miracles in churches and in turn they are given money and fame by satan thats why u cn see them driving Hammers and other luxurious expensive cars worth up to 500,000,000mill. Open ur eyes guys that has nothing to do with ur SADAKAS, they are given that 2prepare u to accept the ant-christ and 'Mark of the beast 666' you'll realise the truth when it's too late and taken straight to hell when u die! Damn them all. ELIMRINGI MOSHI, +255 714-112-062,Ellystrick87@rocketmail.com
 
Back
Top Bottom