SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,906
Akileta cheti cha kuzaliwa hapa kinaweza ibua utata mwingine wa majina labda walete na kile kiapo chake cha kubadili majina!Mbona hapo kunaonekana kuna tatizo kwenye uchapaji tuu? Hivi vitu vinatokea sana! Nilitegemea MsandoAlberto atuwekee cheti cha kuzaliwa cha Mwingulu tuone huo udanganyifu anao jaribu kuonesha! Hapo kuna makosa ya uchapaji hakuna lingine! Ukienda kwenye website ya bunge utakuta kazaliwa 1975.
Wekeni hapa cheti cha kuzaliwa ndio tuone huo udanganyifu..hapo kunaonekana kuna tatizo kwenye uchapaji!
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, amekula kiapo batili kwa kutamka jina ambalo siyo la kwake.
Jana asubuhi kundi la wabunge ambao walikuwa hawajala kiapo wakifanya hivyo, Mwigulu alikuwa mmoja wao, lakini
alijitamka kuwa yeye ni Mwigulu Lameck Nchemba kinyume cha kiapo chake katika gazeti la Serikali la Julai 15, 2011 toleo namba 28.
Katika gazeti hilo taarifa ya kawaida namba 574, Mwigulu alibadilisha jina lake la Mwigulu Lameck Nchemba kwa kiapo kwamba ameliacha na kuanzia Oktoba 12, 2009 amechukua jina jipya la Mwigulu Lameck Nchemba Madelu.......
Pitia zaidi hii: Home
Lipo tatizo, sema tu vi nchi vyetu hivi matatizo ni mengi mno na haya ya kufoji majina/umri nk kuonekana ni madogo madogo tu na ya kupuuzwa. Tuliona kina Lulu, na karibuni binti wa Mtemvu....kote sheria haikufuatwa! Itakuwa kwa Mwigulu? Tunamwonea bure tu.