Wananchi Iramba wamsubiri kwa hamu Rais Samia, wamshukuru kwa miradi mingi ya maendeleo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Kesho Jumanne Oktoba 17, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara kwenye wilaya ya Iramba mkoani Singida ambapo atakagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali yake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wilayani hapa wametoa ya moyoni na kusema wanamsubili kwa hamu kubwa sana Rais Samia ili wamshukuru kwa namna serikali yake ilivyotekeleza miradi mingi ya maendeleo kwenye nyanja za afya, elimu, umeme, miundombinu na mengine mengi.

Akizungumza kwenye daraja la Tutu na barabara unganishi ya inayounganisha mji wa Kiomboi na Tutu, Yohana Kessy mkazi wa Tutu amemshukuru sana Rais Samia kwa mradi huo kwani kabla ya ujenzi wa barabara na daraja hilo wananchi walikua wanapata shida sana kutumia barabara hiyo.

Nae mkazi wa kijiji cha Kisiriri Amani Yumbia amesema wanamshukuru sana mkuu wa wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Mwigulu Nchemba na viongozi wote kwa namna wanavyosimamia vyema miradi inayotekelezwa kwani kwenye kata ya Kisiriri mradi mkubwa wa umeme vijijini (REA) umefanya sasa vijana hawakai vijiweni na badala yake wamejiajiri kwa kufungua viwanda vidogo vya kuchomelea, saluni na mengine mengi.

Akiwa Iramba, Rais Samia atafungua mradi wa maji kutoka ziwa Victoria katika eneo la Shelui utakaohudumia maelfu ya wananchi wa eneo hilo huku hospitali ya wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi ndani ya miaka miwili ya Rais Samia ikisheheni vifaa tiba vya upasuaji, ujenzi wa ICU kubwa ya kisasa, vitanda vya kisasa, X-ray ambapo sasa wananchi wa Iramba hawawezi kwenda tena Singida kwa huduma za kibingwa badala yake wanazipatia ndani ya wilaya yao.

Wananchi kila eneo Iramba wameendelea kumshukuru Rais Samia kwa mvua ya miradi na ndiyo maana sasa wananchi wamekua na hamu kubwa ya kumpokea na kumshukuru kwa haya yaliyofanyika.

 
Kesho Jumanne Oktoba 17, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara kwenye wilaya ya Iramba mkoani Singida ambapo atakagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali yake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wilayani hapa wametoa ya moyoni na kusema wanamsubili kwa hamu
Tatizo la Tanzania ni moja, 99.99999% ya wananchi ni takataka! Unamshukuru nini wakati ni hela yako na mtumishi wako. To crown it all, hili la bandari hata kama hela ni zake, hilo tu linam-dicredit in all angles of her doings!
 
Tatizo la tanzania ni moja, 99.99999% ya wananchi ni takataka! Unamshukuru nini wakati ni hela yako na mtumishi wako. To crown it all, hili la bandari hata kama hela ni zake , hilo tu linam-dicredit in all angles of her doings!
Shida ni hata hao wanaotegemewa kuwa wamesoma pamoja na kuwa hawana nafasi yeyote serikalini ukisikia wasemayo au kuandika unaishia kujiuliza ni dawa gani imetumika kuliloga hili taifa?

Mbona wanawapotosha sana wale wasio elimika na kuwachanganya?

Mfano hata humu JF, yupo mwandishi mmoja ambaye na sasa ni wakili makala zake za siku hizi ni upotoshaji mtupu unaweza kudhani hakusoma kabisa au ni Katibu mwenezi wa chama Twawala.
 
Back
Top Bottom