Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Believe me, hakuna mtaalamu wa uchumi ambaye anaweza kuweka tozo na kodi 7,250/- kwenye mwamala wa elf 50........chukulia mfano makato kwenye ATM shilingi 500, na hapo ume withdraw milioni moja cash.......eti mtaalamu mwenzangu!
ATM ya kwenu huko ndio inatoza 500? Hizo ATM unatumia mwenyewe? Kwa mfano CRDB na NMB hazina makato ya jero zako hizo.

Pili pesa ikienda huko ndio afya ya mabenki sasa lakini unfortunately ATM ni chache kuliko network ya mitandao ya simu na mawakala kwa hiyo huwezi kwepa kirahisi ku transacts unless uwe kwenye shorter distance
 
Jibu swali la msingi 7,000 kwenye 50,000 kuna shida gani?

Ukienda dukani huwa unadai risiti? Ukiuza huwa unatoa risiti?

Tangu tozo zimepanda umeona wakala hata 1 kafunga kibanda kwa kukosa wateja? Au Bar na vilabu huko Vijijini watu hawaendi kunywa pombe?

Lipa kodi wewe Acha utoto wa ulalamishi kama watoto wa tumbili
Ahaaa 7,000 hakuna shida, vipi ikiwa 500 kuna shida gani, ndugu mtaalamu wa uchumi...
 
Rais akiibatilisha tozo na yeye atahamia Burundi?

Anaelewa kwamba kwa kuitaja Burundi kama nchi ya Watanzania kukimbilia anaweza kuanzisha mgogoro wa kidiplomasia wa kimataifa?
 
Kwakweli sijui Mwigulu angekuwa Baba yangu ningepitaje mtaani.

Yaani anajua kabisa wananchi wana stress alafu yeye kama kiongozi mwenye dhamana anaamua kuongezea machungu kwa kauli za kukebehi namna ile!?!

Amezingua
 
ATM ya kwenu huko ndio inatoza 500? Hizo ATM unatumia mwenyewe? Kwa mfano CRDB na NMB hazina makato ya jero zako hizo.

Pili pesa ikienda huko ndio afya ya mabenki sasa lakini unfortunately ATM ni chache kuliko network ya mitandao ya simu na mawakala kwa hiyo huwezi kwepa kirahisi ku transacts unless uwe kwenye shorter distance
Hata kama ATM ni 2,500 kwa kutoa milioni moja, huoni kuna unafuu zaidi ya mara 50 ukilinganisha na wizi mnaotaka kufanya kwenye miamala ya wanyonge....
 
Hata kama ATM ni 2,500 kwa kutoa milioni moja, huoni kuna unafuu zaidi ya mara 50 ukilinganisha na wizi mnaotaka kufanya kwenye miamala ya wanyonge....
Haipo hiyo wewe usikute hata acc.huna..ATM ya baba yako ndio utatozwa 2,500 kwa milioni moja?

Hujui kitu unahemka na sikujibu tena
 
Haipo hiyo wewe usikute hata acc.huna..ATM ya baba yako ndio utatozwa 2,500 kwa milioni moja?

Hujui kitu unahemka na sikujibu tena
Kama withdrawal moja ya laki nne makato ya ATM si zaidi ya buku, zidisha mara tatu hapo kutoa milioni halafu ujione ulivyo zwazwa kukata 7,250/- kwenye elf 50......huwezi kuendelea kunjibu maana huna hiyo akili na PhD yako ya kwenye chibuku...
 
Wewe uwezi fananisha Magufuri na takataka, Magufuri alipoingia madarakani alifuta tozo zote zilizokuwa kero kwa watu wa chini, service charge za luku ya umeme,ushuru wa mazao kwenye mifugo,mpaka kwenye masoko mengine aliwambia wasilipe ushuru mpaka waboreshewe mazingira, baada ya kufa kila kitu kimerudi kama zamani,mpaka mpangaji analipa kodi ya nyumba wakati nyumba sio yako,eti mtadaiana na mwenye nyumba, kipindi cha Magufuri akukuwa na kodi za kipumbavu,na kazi zilifanyika zinaonekana, kipindi cha Magufuri akukuwa na misamaa ya kodi kwa matajiri, sasahivi wamerudisha ndio maana wanakosa ela wanaanza kurundikia kodi watu wa chini.
Service charge na wale wenye matumizi chini ya 75 units ya umeme ilikuwepo kabla ya magufuri cc tuliojenga zamani tunajua pia magufuri aliongeza tozo ktk bank ilikuwa kabla yake ukienda na check unakatwa si zaidi ya 2,600/ alipoingia yy akapandisha Hadi elf 6 na points lakini pia akaweka na Kodi nyingine ktk bank.
 
Hayati Magufuli amewaachia nchi ambayo aliyowajengea misingi mizuri ya ulipaji kodi na kupigana na ufisadi na wizi wa mali za wote. Wao wangeiboresha tu.Mama Samia kaingia madarakani kayavuruga yote ya Hayati Magufuli na kurudisha fedha kwa mafisadi.

Dr Mpango ndiye aliyekuwa Waziri wa fedha. Kuna watu walikuwa wakipiga tenda hewa na serikali na kulipwa mabilioni bila ya kufanya chochote. Serikali ikafanya kazi yake na kuokowa mabilioni kutoka kwa wezi. Mama Samia kasema hataki dhuluma. Wezi warudishiwe fedha zao! Kweli ni fedha zao? Na kuwafanya wote waliokuwa wakifanya kazi na Hayati Magufuli , waliopigana na wakwepa kodi na mafisadi mpaka Tanzania ikafika uchumi wa kati Sasa wanaitwa wadhulumaji.

Sasa Wanasema kodi zikusanywe kutoka kwa walala hoi. Kila senti moja wakipokea misaada kutoka kwa ndugu zao ambao wameisha katwa kodi, zinakatwa kodi tena. Sasa Wawekezaji fake na mafisadi wanasema wamefurahi na kupumuwa tangu Hayati Magufuli kutuacha. Hawa ni wachache tu waliokuwa wakiwalalia ndiyo wengi. Serikali lazima itafute kodi kutoka kwa wanyonge. Hiyo Rais Magufuli asingeruhusu, na wala isingetokea.

Serikali sasa inataka kodi kwa nguvu kutoka kwa walala hoi. ambao ni wengi. Kwa Hayati Magufuli haya yasingetokea. Mafisadi na wadanganyifu wasingerudiishiwa fedha walizowaibia Watanzania. Kungekuwa hakuna haja ya kuweka kodi kwenye huduma inayotumiwa na wanyonge wengi.
We chawa wa jiwe.
 
Kwenye nchi zenye press iliyoenda shule sawa sawa, hapo mwandishi asingemwacha kiongozi atoe kauli ya kibaladhuli namna hiyo halafu apete...

I can imagine mwandishi kama wa BBC World angejibiwa hivyo angemtemesha nyongo na ma follow up questions na kuhakikisha skendo la kufa mtu linaanzia hapo hapo studio....
 
Back
Top Bottom