Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,792
- 4,448
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia Suluhu Hassan amepunguza tozo za miamala ya simu ili zisiwaathiri vijana wengi waliojiajiri kwenye huduma za fedha kwa njia ya simu. Amewataka Watanzania kutochukulia tozo kama uhasama, bali njia ya kuboresha maisha yao.
Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zote zitakazokusanywa kwenye tozo za miamala ya simu kuanzia leo Septemba Mosi zielekezwe kwenye sekta ya elimu (kujenga/kukarabati madarasa na madawati) ili kupanua fursa ya elimu kwa watoto wengi zaidi.