Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba, amesema jambo hilo tayari limefika kwa viongozi wakuu wa nchi na tayari Majaliwa ameitisha kikao na wizara ya fedha na Ile ya mawasiliano kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi.

Dk. Nchemba amesema kikao hicho kitafanyika kesho na hivyo ameowaomba Watanzania kuendelea kuwa watulivu na kuisikiliza serikali yao na siyo kusikiliza maneno ya watu ambao wamekua wakifanya upotoshaji mitandaoni.

"Niwaombe Watanzania muwe watulivu, jambo hili limeshafika kwa viongozi wetu wakuu na Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameguswa nalo na amesikia maoni ya Watanzania, hivyo tayari ameshatoa maelekezo kwetu ya kufanyia kazi hoja zote zinazotolewa na wananchi," amesema.

"Tunaamini kupitia kikao na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho tutatoka tukiwa na muelekeo wa pamoja, kwa hatua ya Sasa niwasihi Watanzania kuendelea kuwa na imani na serikali yao na kumuunga mkono Rais Samia katika utekelezaji wa majukumu ya kuijenga Nchi yetu," amesema Dk. Nchemba.

Ametoa rai kwa wale wote wenye nia ovu kuacha kufanya upotoshaji kwa wananchi na badala yake amewaomba Watanzania kusikiliza maelekezo yote yanayotolewa na viongozi na kuahidi kuyatolea ufafanuzi na maelekezo mambo yote ya kikanuni.
"Rais Samia ana nia njema ya kuijenga Nchi yetu, ni jukumu letu kama wananchi kuendelea kumuunga mkono na siyo kusikiliza wababaishaji wanaofanya upotoshaji," amesema.

Waziri wa Habari na Mawasiliano, Dk. Faustine Ndugulile, amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na wizara ya fedha katika kutolea ufafanuzi sheria hiyo, huku akiwaondoa hofu wananchi na kuwahakikishia kuwa serikali yao ni sikivu na inajali wananchi.
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Nilisema haijawahi kutokea waziri wa Fedha kutokea mkoa wa singida tangu nchi ipate uhuru. Sasa yameonekana. Jiuzulu babu
 
kama kawaida ya ccm

tengeneza tatizo, litatue, uonekane shujaa
Na si ajabu kama zitafanyiwa marekebisho kidogo, wale UVCCM, waliokuwa wamepongeza tozo hizo, watajitokeza tena kumpongeza Rais!!kuwa ni msikivu!!hii mijitu huwa hata siielewi, ina simamia wapi?bali ni kufuata upepo tu!!tatizo wameshatuona wananchi mabwege tu, yaani tatizo wanalitengeneza wao, huko wanalileta kwetu kwa makusudi , tukilalamika wanasema ngoja tukaliangalie upya, wanakuja na ufumbuzi watu tunaanza kushukuru tena, na kuwaona wanatupenda!!
 
Na bado! Tumsaidie Mama kuondoa uozo wote:


Nchi ni yetu waliyo nayo ni dhamana tu.
 
Back
Top Bottom