Mwigulu: Watanzania msikimbie nchi tutarekebisha makosa

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,661
2,000
“Wewe Mtanzania usiikimbie nchi yako, tutarekebisha matatizo, lakini kama umepata fursa ya kuwekeza huko, wekeza!

Lakini usiikimbie nchi yako kwa sababu ya matatizo”. Waziri Nchemba

Pia soma > Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

E7J0rFGXIAEmz33.jpeg


Source : Radio 1
===
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wafanyabiashara waliokimbilia Nakonde nchini Zambia, kwa maelezo ya kuwa huko kuna unafuu wa kodi kuliko Tunduma nchini Tanzania warejee na malalamiko yao yatafanyiwa kazi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ameitoa kauli hiyo Mjini Tunduma wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji huo wakiwemo wafanyabiashara katika mpaka huo wa Tanzania na Zambia walioeleza kero zao mbalimbali.

"Wewe Mtanzania wala usiikimbie nchi yako tutarekebisha yale yaliyomatatizo lakini kama umepata fursa ya kuwekeza wekeza inaruhusiwa, lakini usiikimbie nchi yako sababu ya matatizo hayo tutayarekebisha," amesema Waziri Dkt. Nchemba.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,003
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom