Mwigulu na madereva wamaliza mgomo

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,200
Reaction score
6,949
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Madereva wa mabasi na malori Nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Ostabay Jijini Dar es salaam.

Pamoja na mambo mengine, Viongozi wamekubali kusitisha mgomo uliodumu kwa siku mbili, ili huduma za usafiri ziendelee kama kawaida huku Serikali ikiwa tayari kusikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva.

FB_IMG_1790781541281.jpg
 
Kimejadiliwa nini..?

Changamoto gani serikali itakazozipatia ufumbuzi..?

Tatizo lilikuwa nini mpaka linafikia hatua hii ya kuumiza watu (wasafiri/abiria) wasiohusika na mgogoro...?

Abiria waliocheleweshwa safari zao, walioingizwa gharama zingine na kuteseka stendi kwa siku mbili na wale waliokata tamaa na kuamua kusafiri kwa njia nyingine huku kampuni za mabasi/usafirishaji abiria zikiwa zimechukua fedha zao za nauli wanafidiwaje?

Hili halipaswi Kwisha hivi hivi kwa uzembe wa serikali kushindwa kushughulikia matatizo ya wananchi kwa wakati mpaka yanageuka kuwa majanga..!!
 
Tulisema haya mambo watu
Wakae chini wazungumze angalau watafikia muafaka
Mambo ya kutunishiana msuli kungoleana plate namba hazifai
Huko kwenye kukatana point inatakiwa elimu zaidi wapewe,kama kuna madereva waendawazimu
Wajiandae na huo mfumo
Mambo ya rushwa nk nayo
Yakomeshwe
Trafic wawe yasteyaste basi

Ova
 
Kimejadiliwa nini..?

Changamoto gani serikali itakazozipatia ufumbuzi..?

Tatizo lilikuwa nini mpaka linafikia hatua hii ya kuumiza watu (wasafiri/abiria) wasiohusika na mgogoro...?

Abiria waliocheleweshwa safari zao, walioingizwa gharama zingine na kuteseka stendi kwa siku mbili na wale waliokata tamaa na kuamua kusafiri kwa njia nyingine huku kampuni za mabasi/usafirishaji abiria zikiwa zimechukua fedha zao za nauli wanafidiwaje?

Hili halipaswi Kwisha hivi hivi kwa uzembe wa serikali kushindwa kushughulikia matatizo ya wananchi kwa wakati mpaka yanageuka kuwa majanga..!!
Hapo hao viongozi wakifika 2027 wameenea nipo pale njooni niwanunulie kahawa wote wana jf isipokuwa machawa kina tlAa tlaa na mazwazwa wengine. Hao watapotezwa one after another.
 
Hii move ili kuwa like cumbersome yaan madreva nchi nzima wanapanga mgomo[maana si swala la siku1] mpka wanautekeleza , the all interagency resources zote ni kama zimepararaizi, haya tuseme walikuwa wanajua je waliangalia athari wakaona hazina mashiko? Na mamlaka zote mpka ziingizwe kazini?

Au watu know days wanavipaumbele vyao? Something is incomplete
 
𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗪𝗜𝗚𝗨𝗟𝗨 𝗔𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗩𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗗𝗘𝗥𝗘𝗩𝗔, 𝗠𝗚𝗢𝗠𝗢 𝗪𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗪𝗔

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubali kusitisha mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili, hatua inayowezesha huduma za usafiri kuendelea kama kawaida.

Aidha, Serikali imeeleza utayari wake wa kusikiliza na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva, kwa lengo la kupata suluhisho la masuala yaliyosababisha mgomo huo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha huduma za usafiri zinaendelea kutolewa huku majadiliano kuhusu changamoto za madereva yakiendelea kati ya Serikali na wadau husika.
 

Attachments

  • IMG-20260930-WA0061.jpg
    IMG-20260930-WA0061.jpg
    250.8 KB · Views: 2
  • IMG-20260930-WA0054.jpg
    IMG-20260930-WA0054.jpg
    265.4 KB · Views: 1
  • IMG-20260930-WA0062.jpg
    IMG-20260930-WA0062.jpg
    221.4 KB · Views: 1
  • IMG-20260930-WA0051.jpg
    IMG-20260930-WA0051.jpg
    218.2 KB · Views: 1
  • IMG-20260930-WA0058.jpg
    IMG-20260930-WA0058.jpg
    242.5 KB · Views: 1
  • IMG-20260930-WA0056(1).jpg
    IMG-20260930-WA0056(1).jpg
    287.6 KB · Views: 1
  • IMG-20260930-WA0053.jpg
    IMG-20260930-WA0053.jpg
    244.8 KB · Views: 1
  • IMG-20260930-WA0052.jpg
    IMG-20260930-WA0052.jpg
    251.9 KB · Views: 2
  • IMG-20260930-WA0056.jpg
    IMG-20260930-WA0056.jpg
    287.6 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom