Imani ni kitu kipana sana, Waislam wala tusikasirike wala tusishawishike wala tusiwe watamanifu na wala tusiwe wepesi wa kuchukua hatua mikononi mwetu tunapojaribiwa na watu kwa makusudi, cha kufanya ni kujizuia tu. Binafsi mtu hata akila usoni kwangu wala siwezi kutamani.
Hii pia haiwapi fursa wasio waislam kuwafanyia fujo, mizaha au majaribu waislam pale wanapokuwa wamefunga. Kiufupi ni kwamba tuheshimiane na tustahiane kama Watanzania.
Leo hii mimi Muislam nikienda Mbeya siwezi kukataza watu wa Mbeya wasile kitimoto au wasile nje mchana wa Ramadhan bali nitawastahi na kuheshimu utamani wao nilioukuta, basi na iwe hivyo hivyo wewe nae usiekuwa Muislam siku ukienda Zanzibar au kwenye Mji wenye mkusanyiko mkubwa wa Waislam, wastahi wenyeji wako, lakini pia stahi na kuheshimu utamaduni wao uliowakuta nao. Sisi ni Watanzania bana, tusivunjiane staha wakati tukistahiana kila mmoja anaweza kufata imani yake bila kumkwaza wa imani nyingine kwa vile tu amestahi imani yake.
[emoji120][emoji120][emoji120]