Mwezi wa RAMADHANI ndio umefika ila please tuvumiliane

Lete ushahidi unaoonyesha kama ni waislamu!!!!!. Maana mkishakaririshwa na mabeberu nanyi mko fasta kuamini. Na mavazi wanayotumia ndio kabisaa mnaamini.

Na kama kweli ni waislamu, tambua kuwa uislamu unakataza yote hayo, kwa maana wako nje ya mafundisho ya dini/uislamu.
ISIS
BOKO HARAM
MUSLM BROTHERHOOD
niendelee........................
 
Alichokileta mleta mada kwako ni sahihi?? Naomba unijibu!
Amesema msimpangie cha kupost, na biashara yake ya kitimoto msiisumbue iendelee kama kawaida. Sasa wewe umedhalilishwa nini hapo?
Mimi nahisi Kuna mambo ya muhimu zaidi ya kufanya kipindi hiki cha ramadhan kuliko kulia lia unadhalilishwa na hii mada ya mtu anayejifurahisha nafsi yake.
Nilichomuelewa ni kwamba mfungo wako wa ramadhan usiathiri maisha ya mtu mwingine ambae hausiki na mfungo.
 
Kama ujanja huo mnao jaribuni kumla mbele ya waislamu, humu mnaongea kwa kujigamba, sasa jaribuni kufanya kweli muone kitakachowapata 😀
Mbona tunakula vizuri,lets say tupo kazini au sehemu ya biashara niache kula kwasababu wewe muislamu upo?
Haipo hiyo. Tunakula vzr kila siku...hayo unayoyasema labda yapo huko zenji.

Wakristu walivyofunga mlikula kwa kujificha? Au nyie ndo mna haki zaidi?
 
Wakristu walivyofunga mlikula kwa kujificha? Au nyie ndo mna haki zaidi?

Demi hujambo? Habari za siku rafiki?
Ok, ipo hivi:
Nimefuatilia kwa ukaribu zaidi swala hili na nimegundua kifuatacho.
Sio wengi wa waislam wanaojua/kufuatilia kipindi cha Kwaresma inapoanza, hivyo ni wajibu wenu pia kuwajuza ili kuweza kuepusha udhia au kutokuona na nyie mnapokuwa kwenye kwaresma wao kula mbele zenu huwa kama wanawafanyia dhihaka au kutokustahi mfungo wenu, je huwa mnawajulisha juu ya hilo?

Pili kuna madhehebu mengine ya Kikristo ikiwemo walokole, (sina uhakika kama ndio SDA) wao ile kitendo cha kusema kuwa wamefunga kwao ni shida na wala huwa hawataki wajulikane kuwa wamefunga, je unaliongeleaje hilo?

Sisi waislam mtu akiwa amefunga anakwambia moja kwa moja hata akiwa amefunga Sunna, je mnaonaje na nyie mtu akiwa amefunga kwa upande wenu hata makazini mkawa mnawajuulisha na upande wa Waislam pia ili kuondosha udhia, na msione wanawafanyia dhihaka au kukebehi imani yenu?
 
Demi hujambo? Habari za siku rafiki?
Ok, ipo hivi:
Nimefuatilia kwa ukaribu zaidi swala hili na nimegundua kifuatacho....
Mnatakiwa mkifunga muweze pia kuvumilia kishawishi cha kutamani kula, wakristu wanafunga sana tu sio kwaresma pekee bali unakuta mtu ana maombi yake binafsi anafunga na ukimkaribisha chakula anakwambia asante nimefunga.

Sasa nyie mkifunga why mnataka kila mtu afate matakwa yenu? Yaani nisile mbele ya muislam kwanini hasa? Vumilia matamanio na kama kweli umefunga kwa dhati hutatamani utaendelea na shughuli zako.

Mnawakwaza dini nyingine..wakati wao hawajawahi kuwakwaza. Mna tabia za kibinafsi (am sorry to say this) kulazimisha mambo ambayo wengine haituhusu. Mlitakiwa muwe na nchi yenu mkae wenyewe huko maana hamna uvumilivu wa kuheshimu imani za watu wengine.

Mkristu hakereki wewe ukila kama yeye amefunga.
 
Mnawakwaza dini nyingine..wakati wao hawajawahi kuwakwaza. Mna tabia za kibinafsi (am sorry to say this) kulazimisha mambo ambayo wengine haituhusu.
Mlitakiwa muwe na nchi yenu mkae wenyewe huko maana hamna uvumilivu wa kuheshimu imani za watu wengine.

Mkristu hakereki wewe ukila kama yeye amefunga.

Nimekuelewa vyema, sasa nijibu na hili
Sidhani kama una uhakika na hiki unachoongea, kumkwaza mtu sio kwenye kufunga tu, bali hata kuanzisha biashara ya vinywaji (bar) kwenye eneo lililozungukwa na Waislam pia ni kukwazana.

Kwa asilimia 99% wakazi wa Zanzibar ni waislam na kila ifikapo kipindi cha Ramadhan hukuti mtu kuwa anakula njiani ama huku anatembea, sasa je kwa wale wanaotoka Tanzania bara ndani ndani huko akifika Zanzibar na akaambiwa utaratibu wanaotumia wenyeji wake alikofikia lakini kwa kibri chake akasema asipangiwe unalizungumziaje hili kama sio ushari?

Umeshawahi kuskia maeneo kama Dar, Kigoma, Morogoro, Lindi, Mbeya, Songwe, Singida ama maeneo mengine yenye Wakristo wengi Waislam walioko maeneo hayo wakalalamika kuwa wanakwazwa?
 
Back
Top Bottom