Mwezi wa RAMADHANI ndio umefika ila please tuvumiliane

Mwezi wa RAMADHANI ndio umefika ila please tuvumiliane

Asiruhusiwe kwa sababu gani?

Dini yake?
Mavazi yake?
Umri wake?
Au afya yake?

Na suppose dini yake inamkataza lkn yeye anafanya, so?

Ndio uta generalise kuwa waumini wote wanacheat kama anavyocheat huyo mzee?
Good question,

Dini yake...

We unasemaje?

Sent from my SM-C9000 using JamiiForums mobile app
 
Hamna izoo bhana.

Zenji imekuwa nchi ya wazungu siku hizi.

Uzuri tu kuwa wengi wa wakaazi wa huku washazoea tamaduni za huku hata kama Sio wazaliwa. So huwa kuna staha kwa mambo kama hayo pamoja na mavazi.

Binafsi nafanya kazi na wenzetu wakristo wametoka bara wana nguo zao special za kuvaa Ramadhan.

Na wanapohitaji kula wanakula kuna sehemu ndani wanakaa wanakula hata hatuwabughudhi.

Huku ukiskia mtu kapigwa Ramadhan basi labda awe kalewa na kufanya fujo
Mkuu..you have my respect.
 
Uislam pamoja na kufuata kitabu kitakatifu cha Quran na Sunna za Mtume SAW pia kuna nguzo (sharia) tumewekewa ambazo nazo pia zimetajwa kwenye Quran. Na zipo kwa mpangilio kutokana na umuhimu wake wa kuzitekeleza kwa mpangilio huo.

1. Shahada
2. Kuswali
3. Kutoa Zakka
4. Kufunga mwezi wa Ramadhan
5. Kwenda Makka kuhiji kwa mwenye Kuweza

Na kila nguzo hapo imeelekezwa namna ya kuzitekeleza katika Quran.

Turudi kwenye hio ya nne yaani swaum.

Kuna aya inayosema Enyi Mlioamini mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuja kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezimungu.

Faradhi maana yake ni lazima. Hivyo kufunga kwa muislam mtu mzima mwenye akili timamu na mwenye afya nzuri lazima.

Ili mpate kumcha Mwenyezimungu (kwa nini? Kwa sababu Funga Ni kati ya mja na Mola wake) Anaweza mtu akajifanya kufunga mbele ya macho ya watu lakini akala au kunywa maji kwa kujificha. Hio ni khiari yake. Ila kwa mtu mwenye imaan kuwa atarudi kwa Mola wake na ataulizwa juu ya matendo yake na atahukumiwa na Mola wake basi anafunga ili kupata fadhila kama alivyoahidiwa na Mola wake. (Swaum ni baina ya mja na Mola wake)

Na aya hiohio iliendelea kueleza kuwa kwa mtu alie mgonjwa au yupo safafini basi Anaweza kuwacha kufunga na akaja mukamilisha (kulipa alizoziacha wakati ana dharura)

Pia kwa wajawazito, wanaonyonyesha pamoja na vikongwe wanaruhusiwa kutokufunga na kuja kulipa siku za mbele au kutoa fidia.

Faida za swaum kwa binaadam au kwa mwenye kuamini ni pamoja na kumcha MwenyeziMungu kwani unajizuia kula na kunywa pamoja na kulala na mkeo au mumeo wakati wa mcha ilhali una uwezo wa kufanya hayo lkn unaachana nayo kwa kutegemea malipo Ya kheri.

Pia tumeambiwa tufunge tupate afya. Funga inasaidia kuacha kula kula ovyo wakati mwengine pasi na uhitaji Hivyo basi unauepushia mwili na vitu vingi.

Funga pia inaweka usawa wa walio nacho na wasionacho kwani wote hukaa bila kula kwa masaa kadhaa na kufeel how hunger inakuwaje kwa wasio na chakula cha kutosha. Ndio maana inasisitizwa sana pia kutoa sadaka kwa wasiojiweza kwenye mwezi huu zaidi.

Kwa wanaokula kupitiliza linapozama jua hio haifai. Tunashauriwa kula kiasi tu kwani kuna ibada nyengine zinaendelea usiku kama kuswali taraweikh na tahajjud.

Na pia ni thawabu mtu kula daku karibia ya alfajiri japo maji na tende ili usiwe dhaifu kwani dini haimkalifishi mtu.
[emoji120][emoji120]
 
So na sasa mambo yawe yale yale msianze kutupa masharti ya nini cha kupost kwenye mitandao ya kijamii na nini sio cha kupost acha dunia iendelee kama miezi mingine, mambo ya mihemko acheni kabisa.

Pia sitegemei sisi wafanya biashara wa Kitimoto tuathirike kipindi hiki maana watumiaji hatujafunga tukiona mabadiliko yoyote tutajua kuna watu walikuwa wanashirikiana na sisi.
🤣😂😅😆
 
Lakini pia utambue Kuna mambo kwenu nyie wakristo hayawi dhambi lakini kwa wenzenu waislamu ni dhambi

Mfano wenzenu waislamu kitimoto ni haramu kwao lakini nyie wakristo mnaruhusiwa kumla kitimoto,au kusema yesu ni mwana wa mungu ni sahihi kwa ninyi wakristo lakini wenzenu waislamu mungu wao hakuzaa wala hakuzaliwa na hana mwana

Sasa kwanini wewe uwawekee masharti watu wa dini nyingine?

Ushauri wangu kwako kama unatambua ustaarabu na unaheshimu dini ya mwenzio basi kwa nyakati kama hizi huyo kitimoto ni vyema ukawa unamla sirini na mengine ambayo unaona hayawapendezi waislamu hususani kwa nyakati hizi pia uyafanye sirini
Ina maana akimla hadharani atawatamanisha au sio
 
Mleta Hoja mwenye uzi anasema kila mtu afanye ibada zake bila kumshurutisha mwingine

Kwa Muktadha huo wewe funga usimlazimishe yeye ale kwa kujificha
Hawalazimishwi kula kwa kujificha. No wao wenyewe tu nao wanatuheshimu kwa sababu wanaona mwezi wa Ramadhan kuna kuwa kuna hali gani.

Na MashaAllah hata kama tunajua kuwa mchana wamekula inapofika maghrib tunafutari nao pamoja. Mana ofisi yetu sisi ni mpk saa 1 usiku.
 
Una ugonjwa wa akili si bure. Yaani nitoe hela yangu mfukoni ninunue kitimoto halafu Nile kwa siri???

Nile kwa siri kwa sababu ya imani yako ambayo mimi siiamini?

Tusipangiane maisha...Hiyo hela umenitafutia wewe?
😀 😀 😀 😀
 
Lakini pia utambue Kuna mambo kwenu nyie wakristo hayawi dhambi lakini kwa wenzenu waislamu ni dhambi

Mfano wenzenu waislamu kitimoto ni haramu kwao lakini nyie wakristo mnaruhusiwa kumla kitimoto,au kusema yesu ni mwana wa mungu ni sahihi kwa ninyi wakristo lakini wenzenu waislamu mungu wao hakuzaa wala hakuzaliwa na hana mwana

Sasa kwanini wewe uwawekee masharti watu wa dini nyingine?

Ushauri wangu kwako kama unatambua ustaarabu na unaheshimu dini ya mwenzio basi kwa nyakati kama hizi huyo kitimoto ni vyema ukawa unamla sirini na mengine ambayo unaona hayawapendezi waislamu hususani kwa nyakati hizi pia uyafanye sirini
Unasema huyo kitimoto amlie sirini Ili asimtamanishe mwisilamu?
 
Halafu utasikia waislam ni wadini sana mbona kipindi cha kwaresma wao hawakuanzisha thread Kama hizi
Sasa wangeposti nini??. Maana kila wanachokula wao sisi Wakristo tunakula lkn Si kila tunachokula sisi Wakristo na wao wanakula Mfano Kitimoto,Sasa mtoa uzi anawatahadharisha kuwa isije ikatokea biashara yake ikadorora mwezi huu maana wanaofunga sio walaji Sasa kwanini biashara idorore?!!.
 
Lakini pia utambue Kuna mambo kwenu nyie wakristo hayawi dhambi lakini kwa wenzenu waislamu ni dhambi

Mfano wenzenu waislamu kitimoto ni haramu kwao lakini nyie wakristo mnaruhusiwa kumla kitimoto,au kusema yesu ni mwana wa mungu ni sahihi kwa ninyi wakristo lakini wenzenu waislamu mungu wao hakuzaa wala hakuzaliwa na hana mwana

Sasa kwanini wewe uwawekee masharti watu wa dini nyingine?

Ushauri wangu kwako kama unatambua ustaarabu na unaheshimu dini ya mwenzio basi kwa nyakati kama hizi huyo kitimoto ni vyema ukawa unamla sirini na mengine ambayo unaona hayawapendezi waislamu hususani kwa nyakati hizi pia uyafanye sirini
Kwani Waislamu wanaishi Karibu na Vibanda vya kuuzia kitimoto??
 
Back
Top Bottom