mhuogomkavu
Senior Member
- Jun 23, 2017
- 116
- 102
Huyu jamaa alikuwa uhasibu jana asbh anazurura zake, kama amekamatwa basi leo itakuwa siku ya piliMwenyekiti wa CHASO - UDOM bwana Henry Mang’era yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na CHADEMA chuoni hapo.
Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.
Kwa mujibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.
Viongozi wa CHADEMA na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.