Ajaye
JF-Expert Member
- Sep 25, 2020
- 319
- 595
Wakuu Habari za muda huu.
Wiki kadhaa zilizopita University of Dodoma iliripotiwa kuwa na matatizo ya kunguni wakajitetea haikuishia hapo kuna mwenzetu mmoja alitoa mada juu ya uchafu wa vyoo na miundombinu ya maji taka.
Sasa leo hii wakuu, College of Business Studies and Law CBSL, wanafunzi wanalala 10 au zaidi kwenye chumba kimoja, wanafunzi wanahamishwa usiku kutoka hosteli moja kwenda nyingine.
Sababu yao ni ya msingi sana kuwa wanaanza ukarabati wa miundombinu wakati huu, sasa katika hili nina maswali kwenu UDOM;
Mosi, Miezi zaidi ya mitatu wanafunzi walikuwa wamefunga vyuo kwenda kwenye field practical, katika kipindi chote hicho mlishindwa kufanya ukarabati wa vyoo na moundombinu ya majitaka mpaka muanze ukarabati kipindi wanafunzi wamefungua chuo tena wiki hii?
Mbili, kama mlishindwa kufanya wakati huo tajwa hapo juu kwanini msitafute suluhu ya malazi kwanza kwa wanafunzi kisha muanze kuwaondoa? Kuliko kuwabananisha kwenye chumba kimoja wanafunzi zaidi ya 10? Serikali ya wanafunzi mpo wapi?
Professor Mkenda Wasaidie wanafunzi wa UDOM maana ukaguzi wako uliofanyika miezi kadhaa iliyopita pale UDOM haujazaa matunda yoyote yale.
Tuwasaidie kupaza sauti.