Mwenyekiti wa CHASO - UDOM yuko mahabusu wiki ya pili sasa kwa kosa la kuwashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunga na CHADEMA

mhuogomkavu

Senior Member
Jun 23, 2017
116
250
Mwenyekiti wa CHASO - UDOM bwana Henry Mang’era yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na CHADEMA chuoni hapo.

Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.

Kwa mujibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.

Viongozi wa CHADEMA na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.

Huyu jamaa alikuwa uhasibu jana asbh anazurura zake, kama amekamatwa basi leo itakuwa siku ya pili
 
divide and rule

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
265
250
Ajifunze na kuelewa kuwa ukiwa unaelekea Udom, Geti la Chimwaga kuna nembo ya CCM, atafute chuo kilichojengwa na Chadema ili akafanye siasa
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,544
2,000
Mwenyekiti wa CHASO-UDOM bwana HENRY MANG’ERA yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na Chadema chuoni hapo.

Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.
Kwamjibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.

Viongozi wa Chadema na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.

View attachment 1278057

Huko alipo ndio kuzuri akawashawishi mahabusu sasa
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,342
2,000
Kama taarifa hii ni ya kweli, ningependa kujua CHADEMA wamemsaidia vipi huyu kijana wao. Hili ndilo la msingi zaidi.

Kama hawajafanya lolote kwa wiki zote hizi kumsaidia kijana wao, basi chama hikikitakuwa na walakini.

Walishakuwa na utaratibu mzuri wa kuyashughulikia maswala kama haya yanapotokea kwa wananchama wao. Kama huo utaratibu haupo tena, chama kinapoteza mwelekeo.
 
Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,571
2,000
Na G malisa

FB_IMG_1575169855941.jpg

Tukitaka nchi hii iendelee tuondoe ubaguzi huu wa KIPUMBAVU unaopandikizwa na wanasiasa kwa kutumia vyombo vya dola. Kumbagua mtanzania mwenzio kwa sababu ya itikadi za kisiasa haina tofauti na ubaguzi wa rangi, au ubaguzi mwingine wowote ule. Ni UPUMBAVU kufikiri kuwa ukiwa CCM unakuwa binadamu zaidi kuliko mwenzio asiye CCM.

Tar.03/11/2019 Chama cha mapinduzi tawi la UDOM, kilitoa taarifa ya kuwakaribisha chuoni wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Taarifa hiyo ilibandikwa ktk mbao za matangazo (kwa ruhusa ya uongozi wa chuo), kwenye miti, kuta za mabweni, na maeneo mbalimbali ya chuo. Pia ilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Hakuna aliyehoji, aliyekemea, wala aliyesema CCM wanaingiza siasa vyuoni.

Siku chache baadae, Shirikisho la wanafunzi ambao ni wanachama wa CHADEMA chuoni hapo (CHASO UDOM) nao wakatoa tangazo kama lile la CCM la kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni. Walipoenda kwa Dean of students kuomba kibali cha kubandika tangazo hilo kwenye mbao za matangazo wakanyimwa, na kukaripiwa vikali.

Kwa ustaarabu hawakutaka kuchafua kuta za mabweni (kama wenzao walivyofanya), badala yake wakaamua kusambaza taarifa yao kupitia mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa tawi hilo Bw.Henry Mang'era ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 akatuma taarifa hiyo kwenye magroup mbalimbali ya whatsapp. Kesho yake akakamatwa na kupelekwa mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga. Kosa lake ni kusambaza taarifa inayoleta taharuki na kushawishi wanafunzi kufanya siasa chuoni kinyume cha sheria.

Kwa muda wa wiki mbili sasa polisi wamemshikilia, wakimpiga bila kumpeleka mahakamani. Wamekataa kumpatia dhamana licha ya jamaa zake kuwaomba polisi kumpa dhamana au kumpandisha mahakamani ili akajibu mashtaka yanayomkabili.

Waliomtembelea kituoni juzi wanasema alikua anachechemea na kushindwa kusimama vizuri. Inadaiwa alipigwa na kupata majeraha sehemu za goti.

Polisi wanafanya haya wakijua kabisa ni kinyume cha sheria, kwa sababu mtuhumiwa hapaswi kukaa kituoni masaa 48 bila kupandishwa kizimbani. This is detention without trial, ambayo haina tofauti na waliyofanya makaburu kule SA. Mang'era apelekwe mahakani, kama kuna kosa mahakama itaamua.

#Justice4Mangera

FB_IMG_1575207501897.jpg
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
3,087
2,000
Happy ndipo wananchi wale ambao hawajui kua CCM ina nguvu,wajue.
 
Manyovumpya

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
688
500
Naunga mkono atendewe haki, ila nawasisitiza watoto wetu wote unaobahatika kupata nafasi kujiunga na vyuo kupata elimu ya juu, nendeni vyuoni mkasome mpate elimu na sio kufanya siasa!.

Hamjifunzi kwa Abdul Nondo?. Baada ya kukubaliwa kurudi chuo kukamilisha masomo yake, sasa yuko busy kusoma.

Mshika mawili, moja humponyoka. Kama umekwenda shule kusoma, kasome. Ukimaliza njoo kwenye siasa.

P
Sahihi kabisa mkuu yan wasipokuelewa hapa hawakuelewi tenaaaa
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
18,540
2,000
Mwenyekiti wa CHASO - UDOM bwana Henry Mang’era yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na CHADEMA chuoni hapo.

Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.

Kwa mujibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.

Viongozi wa CHADEMA na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.

Kadiri wanavyoipiga vita Chadema ndio kwanza inazidi kushamiri
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
18,540
2,000
Acheni ushabiki wa ajabu..wapi uliona pameandikwa ni kosa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa?? Tatizo ni kua unatumiaje uanachama wako wa siasa na maeneo gani. Lakini ndio ajifunze kua chama kinakutumia kwa faida yao..hapo kakamatwa chama kimemnawa mapemaaa
Kawaulize mapoliccm
 
Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,496
2,000
Boss Mwanahabari Huru Ningeshauri kwenye Katiba yetu ya Nchi na Sheria na Kanuni zetu, kupiga marufuku SIASA Mashuleni, Vyuoni na kwenye jambo lolote linalohusu ELIMU. Kama ilivyo Serikalini kwa Watumishi wa Umma.

Ndio maana Elimu yetu inayumba. Ndio maana Wasomi wetu, Elimu waliyosomea wengi wao hawaitumii ipasavyo.

Mwenyekiti wa CHASO - UDOM bwana Henry Mang’era yuko mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga kwa wiki ya pili sasa kwa kosa la yeye kuwa Chadema na kwamba anawashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunge na CHADEMA chuoni hapo.

Polisi wamemnyima dhamana kwa madai kuwa kosa hilo ni kuhatarisha usalama wa Chuo, yaani kwamba kuwa mwanachadema katika Chuo cha Dodoma ni kuhatarisha amani ya chuo.

Kwa mujibu wa polisi kituoni hapo, inaelezwa kuwa hayo ni maelekezo toka Utawala Mkuu wa Chuo kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi ambao ni Tawi la Mbogamboga.

Viongozi wa CHADEMA na Wanasheria mliokaribu hapo Dodoma saidieni kamanda huyu apate haki yake ya dhamana na mambo mengine ya kisheria.

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,770
2,000
Naunga mkono atendewe haki, ila nawasisitiza watoto wetu wote unaobahatika kupata nafasi kujiunga na vyuo kupata elimu ya juu, nendeni vyuoni mkasome mpate elimu na sio kufanya siasa!.

Hamjifunzi kwa Abdul Nondo?. Baada ya kukubaliwa kurudi chuo kukamilisha masomo yake, sasa yuko busy kusoma.

Mshika mawili, moja humponyoka. Kama umekwenda shule kusoma, kasome. Ukimaliza njoo kwenye siasa.

P
Acha hizo
Mbn wakina sitta walifanya siasa wakiwa vyuoni
Kwann kila kitu Mnataka kufanya nyie maccm

Ova
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Naunga mkono atendewe haki, ila nawasisitiza watoto wetu wote unaobahatika kupata nafasi kujiunga na vyuo kupata elimu ya juu, nendeni vyuoni mkasome mpate elimu na sio kufanya siasa!.

Hamjifunzi kwa Abdul Nondo?. Baada ya kukubaliwa kurudi chuo kukamilisha masomo yake, sasa yuko busy kusoma.

Mshika mawili, moja humponyoka. Kama umekwenda shule kusoma, kasome. Ukimaliza njoo kwenye siasa.

P
Ni vigumu mno kwa mtu anayejielewa kusoma bila kuijua na kuifahamu siasa ukiwa chuo kikuu, na kwa wenye interests na siasa ni muda muafaka.

Ni upuuzi kuzuia vijana kufanya politics wakiwa vyuoni. Eneo/mazingira ya chuo ndiyo siasa hairuhusiwi hasa kufanya mihadhara na mikutano ya siasa ila si kwamba mtu akiwa chuoni haruhusiwi kufanya siasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom