Mwenyekiti wa CHASO - UDOM yuko mahabusu wiki ya pili sasa kwa kosa la kuwashawishi wanafunzi wa mwaka wa kwanza kujiunga na CHADEMA

Naunga mkono atendewe haki, ila nawasisitiza watoto wetu wote unaobahatika kupata nafasi kujiunga na vyuo kupata elimu ya juu, nendeni vyuoni mkasome mpate elimu na sio kufanya siasa!.

Hamjifunzi kwa Abdul Nondo?. Baada ya kukubaliwa kurudi chuo kukamilisha masomo yake, sasa yuko busy kusoma.

Mshika mawili, moja humponyoka. Kama umekwenda shule kusoma, kasome. Ukimaliza njoo kwenye siasa.

P
Hivi ccm haina wanachama udom..????
 
Hivi ccm haina wanachama udom..????
Tunajenga taifa la hovyo kwa kuharibu umoja ustawi wa taifa letu.Siasa hata enzi za mwalimu tulisoma katiba ya ccm, Mwanafunzi wa chuo iwe haramu?. Sina hakika ni maagizo ya JPM ,mnamharibia sana mkuu kwa kufanya ujinga huu.Huyo kijana aachiliwe haraka bila mashariti.Vinginevyo kama ana hatia afikishwe mahakamani.
 
Hapana bwana, ni siku ya pili na sio wiki mbili. Amekamatwa jana tu. Unawekaje taarifa ya kuforwadiwa bila kupata ukweli wake?? Siku nyingine taarifa kama hizi unapiga simu kwa sisi wanafunzi tulio kwenye eneo lenyewe kuconfirm
Chumvi kidogo muhimu kwenye umbea ili kuongeza mizuka ya wachangiaji
 
Na G malisa

View attachment 1278327

Tukitaka nchi hii iendelee tuondoe ubaguzi huu wa KIPUMBAVU unaopandikizwa na wanasiasa kwa kutumia vyombo vya dola. Kumbagua mtanzania mwenzio kwa sababu ya itikadi za kisiasa haina tofauti na ubaguzi wa rangi, au ubaguzi mwingine wowote ule. Ni UPUMBAVU kufikiri kuwa ukiwa CCM unakuwa binadamu zaidi kuliko mwenzio asiye CCM.

Tar.03/11/2019 Chama cha mapinduzi tawi la UDOM, kilitoa taarifa ya kuwakaribisha chuoni wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Taarifa hiyo ilibandikwa ktk mbao za matangazo (kwa ruhusa ya uongozi wa chuo), kwenye miti, kuta za mabweni, na maeneo mbalimbali ya chuo. Pia ilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Hakuna aliyehoji, aliyekemea, wala aliyesema CCM wanaingiza siasa vyuoni.

Siku chache baadae, Shirikisho la wanafunzi ambao ni wanachama wa CHADEMA chuoni hapo (CHASO UDOM) nao wakatoa tangazo kama lile la CCM la kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni. Walipoenda kwa Dean of students kuomba kibali cha kubandika tangazo hilo kwenye mbao za matangazo wakanyimwa, na kukaripiwa vikali.

Kwa ustaarabu hawakutaka kuchafua kuta za mabweni (kama wenzao walivyofanya), badala yake wakaamua kusambaza taarifa yao kupitia mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa tawi hilo Bw.Henry Mang'era ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 akatuma taarifa hiyo kwenye magroup mbalimbali ya whatsapp. Kesho yake akakamatwa na kupelekwa mahabusu kituo cha Polisi Chimwaga. Kosa lake ni kusambaza taarifa inayoleta taharuki na kushawishi wanafunzi kufanya siasa chuoni kinyume cha sheria.

Kwa muda wa wiki mbili sasa polisi wamemshikilia, wakimpiga bila kumpeleka mahakamani. Wamekataa kumpatia dhamana licha ya jamaa zake kuwaomba polisi kumpa dhamana au kumpandisha mahakamani ili akajibu mashtaka yanayomkabili.

Waliomtembelea kituoni juzi wanasema alikua anachechemea na kushindwa kusimama vizuri. Inadaiwa alipigwa na kupata majeraha sehemu za goti.

Polisi wanafanya haya wakijua kabisa ni kinyume cha sheria, kwa sababu mtuhumiwa hapaswi kukaa kituoni masaa 48 bila kupandishwa kizimbani. This is detention without trial, ambayo haina tofauti na waliyofanya makaburu kule SA. Mang'era apelekwe mahakani, kama kuna kosa mahakama itaamua.

#Justice4Mangera

View attachment 1278326
IGP SIRO watanzania sio wajinga,matukio ya uonevu na upendeleo wanayarekodi siku hazigandi yatakuja kufufuliwa tu.
 
Hivi tunaweza kujinasibu kuwa taifa lina Mungu kweli?
Mungu yupi wa unyamaunyama?
Mungu yupi wa maovu kama haya?
Mungu yupi wa udhalilishaji kama huu?
Yule aliye kinyume na Mungu ametamalaki!
 
Polisi wiki ya pili anafanywa nini huko?

Yaani kweli mlinzi wa sheria anavunja sheria!!

Ndio maana makesi yao mengi kama sio yote wanashindwa.

Aibu toka juu mpaka chini
 
You cannot just comment on a thread without knowing the facts. Is there any member of this forum who can bring the facts about this case? We cannot discuss rumours.
 
Back
Top Bottom