Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Baada ya memba wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna changamoto ya Wadudu aina ya Kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi wa Chuo Kukuu cha Dodoma (UDOM), ufafanuzi umetolewa kutoka kwenye mamlaka ya chuo hicho.
Taarifa ya awali ya Kunguni hii hapa - Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami anajibu madai hayo kwa kusema:
“Ukweli ni kwamba suala hilo halina kweli japokuwa sisi kama Chuo tunaelewa kunapokuwa na wingi wa watu kunakuwa na tishio la magonjwa mbalimbali ikiwemo uwepo wadudu hao aina ya Kunguni, ndio maana kila Wanafunzi wanapotoka Chuo tunaingia gharama kubwa ya kupuliza dawa ili kuhakikisha kila kitu kipo sawa.
“Ukija chuoni hata sasa utaona tumefanya kazi kubwa na kila kitu kipo sawa lakini changamoto kubwa tunayoipata ni suala la kusisitiza usafi kwa Wanafunzi wetu, wanapokuja wanakuta mazingira masafi, wanapoanza kuweka vyakula kwenye mabweni ndipo wanapoanza kufuga hao wadudu.
“Uchafu unapokithiri ndipo Kunguni nao wanavyopata nafasi, sisi hatufugi Kunguni ila wanatokana na uchafu.
“Chuo tumeweka watu wanafanya usafi kila kukicha kupitia kampuni, suala la kufanya usafi binafsi ni la mtu binafsi kama kwenye chumba chake anacholala atashindwa kuwa msafi itakuwa sio sawa kwa mtu kwenda kumtandikia kitanda.
“Suala la kunguni ni letu sote, ni wajibu wa Wanafunzi kuwajibika na kuchukia kuwa na hao wadudu, tunatimiza wajibu wetu kwa kupuliza dawa upande wetu kama tulivyofanya, wanapokuja Wanafunzi waendeleze kwa kila mmoja kuchua tahadhari binafsi.
“Tunaomba Wanafunzi wanapokuta mazingira safi waendelee kuyatunza kama walivyoyakuta.”