Verrazanno
JF-Expert Member
- Sep 15, 2021
- 384
- 783
Hakatishi mtu.
Kwa amri na utekelezaji wa wanamgambo wa Houthi wa Yemen.
Nia na madhumuni wamesema ni kuzuia usafirishaji kwenda Israel. Lakini kwa sababu baharini huwa ni vurugu mechi, li meli la Ukraine lina bendera ya Tanzania, wafanyakazi wa Uturuki, waendeshaji wa Ufaransa, na mzigo wa Israeli, Houthi fighters wamesema you ain't fooling nobody, tunapiga chochote kinachokatisha.
Meli inabidi zizunguke dunia kwa Mandela.
Njia ya kuzungukia kwa Mandela inagharamimu ziada ya dola milioni moja kila safari
Lakini kwa meli zinazoendelea ku take chance hapo hapo red sea makampuni ya bima za meli yamewapandishia gharama mara kumi. Meli zimesema isiwe tabu, bora nusu hasara, wameamua kuzungukia kwa Mandela. Kitumbua cha biashara kati ya Europe na Asia kimeingia mchanga, na hakuna la kufanya.
******
Ni furaha iliyoje kuona hatuna mtawala mmoja wa dunia mwenye nguvu ya kuamua kila kitu, awe mzungu au myahudi na vyombo vyao vya ulinzi na ujasusi na zana nzito za kivita. Hata angekuwa ni Mwarabu, au Mchina, au Mrusi, hatutaki unipolar world.
Kumbe penye nia ya mnyonge kusimamia haki yako ukikazana unaweza kuipata. Watu kama hawa huwezi hata kuwaza kuwarubuni wakupe bandari yao, ukijaribu wanamwaga ugali, wanafunga bahari mazima.
Kwa hili la kusimamia maslahi yake namheshimu Mwarabu! Sijali cha dini yake wala dini ya Myahudi wala ya Mzungu.