Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,913
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu wakati vita vikiendelea,mori wa vita sasa umepanda kwa Iran na kusema iwapo vita havitasimama basi dunia ijitayarishe kuona taifa hilo likiuziba mfereji wa Gibraltar.
Mfereji huo kama ilivyo kwa mfereji wa Sueza na bahari nyekundu nao ni njia kubwa ya baharini inayounganisha mabara na nchi nyingi katika usafiri wa baharini.Mfereji huo uko baina ya kaskazini ya Afrika eneo la Morocco na Spain na ndipo meli zote zinazoelekea Ulaya kaskazini na Marekani zinapopita baada ya kupita mfereji wa Suez
Tamko hilo limetolewa na Brigedia Mohammad Reza Naqdi wa Iran.Japo Iran haipakani moja kwa moja na mfereji huo lakini washirika wake wa Lebanon na Syria wanapakana na bahari ya Medeteranean.
Kuonesha kuwa chagizo hilo linawezekana pindi washirika hao wakikusudia,leo meli nyengine yenye uhusiano na Israel ikitokea Saudi Arabia kuelekea India imepigwa na droni na kushika moto pamoja na kwamba eneo hilo tayari lina ulinzi wa nchi 20 zikiongozwa na Marekani.