Mwanza jiji zima hakuna Brown Bread?

Mwanza jiji zima hakuna Brown Bread?

Haya mambo sijui ya brown bread, brown sugar, low fat milk etc Tanzania bado sana. Wengi tumeyajua tulipoenda majuu hivyo wengi ambao hawatoka yanawatesa. Kwa mfano ukienda dukani unasema nipe sukari na unapewa sukari yoyote.
Mimi nimejua brown bread hapa hapa bongo tena nikiwa mdogo sana
 
Upatikanaji wa bidhaa ni kulingana na uhitaji wake/matumizi. Kwa Mwanza mikate hiyo haina soka kabisa na inauzwa bei ndogo kulinganisha na white bread. Sasa ukizingatia na kua mikate haina shelf life kubwa kwanini wafanya biashara wahangaike nayo?

Ukweli ni kua mikate hiyo ipo lakini haipatikani kila mahali sana sana kwenye supermarkets za wahindi utakuta tele.
Royal oven ipo, cafeteria ipo
 
Mimi ni mchaga biashara zangu nafanyia mwanza kusema ukweli hii bidhaa hipo tena ni nyingi tu na auwezi linganisha mwanza na arusha hata kidogo mwanza ni baada ya dar, wingi wa watu, ukubwa wa city centre, mzunguko wa hela nk.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
SAUT imehamishia wachaga wengi sana Mwanza luchelele, buhongwa, mkolani, nyegezi mmepateka
 
Upatikanaji wa bidhaa fulani hutegemea demand ya bidhaa hiyo kwenye soko.

Ikiwa mji wa Mwanzo, wenyeji wake sio watumiaji wa Brown bread basi hakuna bakery itakayokubali kutengeneza aina hiyo ya mikate na kuingia hasara ya kukosa wanunuzi.

Arusha na Dar, kuna walaji wengi wa brown bread hivyo upatikanaji wake ni rahisi. Na hiyo ni sababu ya wingi wa wageni kutoka mataifa ya Ulaya ambao wengi wao hupendelea sana aina hiyo ya mikate.

Jiji la Mwanzo limejaa Wasukuma ambao hawajui kabisa brown bread ni kitu gani.
Hakuna mgeni atapendelea brown bread unless awe na kisukari, ni mikate isio na ladha kabisa hata upake jam na peanut butter bado haina taste.
 
Hiyo ni fursa fungua kiwanda cha mikate ya brown
 
Ipo mingi,nikiwa Mwanza nishatumia iyo mikate mara kwa mara.
Kerla beckery.
Mwanza beckery.
Buswelu beckery.
War same beckery.
izo👆ni baadhi ya beckery ambazo nimeshatumia mikate yao ya brown.
 
Mwanza kuna wapika vitumbua wengi sana kuliko mkoa wowote Tanzania,Mwanza kuna mbwa koko wengi sana wanaozurura ovyo kuliko mkoa wowote Tanzania mpaka mjini Kati mfano Posta au kariakoo upishane na mbwa koko hii imenishangaza sana.

Chapati ni adimu sana mtaani inasemekana wanawake wa Mwanza kuchoma chapati ni kipengele ila hayo ya mkate wa brown ni mambo ya kizungu.
Nilipoenda Mara ya kwanza Mwanza, nilishangazwa sana na uwingi wa Mbwa
 
Mwanza kuna wapika vitumbua wengi sana kuliko mkoa wowote Tanzania,Mwanza kuna mbwa koko wengi sana wanaozurura ovyo kuliko mkoa wowote Tanzania mpaka mjini Kati mfano Posta au kariakoo upishane na mbwa koko hii imenishangaza sana.

Chapati ni adimu sana mtaani inasemekana wanawake wa Mwanza kuchoma chapati ni kipengele ila hayo ya mkate wa brown ni mambo ya kizungu.
Kuna kule Kiseke jamani hupigi hatua 2 bila kukutana na mbwa koko 15. Yaani nahisi kiseke mbwa koko ni wengi kuliko watu wanaoishi. Jioni pale mjini wapika vitumbuka kila baada ya hatua moja.

All in all mwanza ni mji mzuri sana kuishi hata kama unaanza maisha kila kitu kipo affordable kuanzia vyakula, usafiri mpaka nyumba za kupanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi kati nilikuwa Mwanza, sasa huwa mimi sipatani sana na hivi vitu vilivyo kobolewa aunatakaga kupunguza, kwamba vingine basi viwe ni vile havijakobolewa kama ngano.

Nikauliza wenyeji wangu kwamba nitapata brown bread Mwanza? Wakaniambia ndio nini hio nikawaambia mikate ambayo ngano yake haijakobolewa, wakaniambia hawajawahi ziona na hawazijui, Ikabidi sasa nianze kuzunguka kwenye Super Market ndogo ndogo zote hakuna, nikapata wazo la kwenda Rock city Mall, Kufika kule yaani ndio kabisa hata staff hawaijui, nilichoka sana fikiria Jiji kubwa kama lile hakuna products kama zile.

Ikabidi ninunue unga wa ngano wa Atta nikapike Chapati nyumbani.

Nikakumbuka Arusha au Dar mikate kama ile unakuta nayo maduka ya mitaani kabisa ukiachana na Super Markets.

Mwanza ni ukubwa tu ila ni jiji la kishamba sana huwezi compare na Arusha au Dar, tuiacha Dar ni kubwa sana ila huwezi ilinganisha na Arusha kamwe.
Mwanza ni ukubwa tu ila ni jiji la kishamba sana huwezi compare na Arusha au Dar, tuiacha Dar ni kubwa sana ila huwezi ilinganisha na Arusha kamwe.
Hakuna cha mkate wala nini kiini cha mada yako ni hayo maneno👆👆👆
Wivu na chuki dhidi ya mwanza vitawauwa, wewe endelea kutibu kisukari chako tena pole sana, hizo mikate ya brown inapatikana sehemu nyingi tu mwanza lakini watu hawapendelei na bei yake ipo chini kulinganisha na white bread.
 
Hoyo mikate mingi sana royal oven isifie tu Arusha
 
Back
Top Bottom