Jiji la Mwanza kuna kitu hakiko sawa

Dig the EA

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
279
270
Habari Wana jamvi?

Naomba kutoa mawazo yangu kuwa Kuna jambo haliko sawa jijini Mwanza hususani swala la miundombinu. Jijini Mwanza hakuna miundombinu au barabara za kiwango cha jiji Kama ilivyo kwa majiji mengine. Barabara ndani ya jiji la Mwanza ni ndogo, na za zamani.

Ukiangalia barabara ya kutoka Usagara hadi mjini ni ndogo Kama njia moja tu. Barabara Ile husababisha foleni sana, barabara Ile inafaa njia nne. Pia barabara ya kutoka mjini kwenda Igoma/Kisesa nayo inafaa njia nne lkn ni njia mbili kama moja tu kutaja kwa uchache barabara za Mwanza.

Swali; ni kwa nini serikali na viongozi wa jiji hawaoni umhimu wa barabara hizo au barabara zilizopo Mwanza. Jiji la DSM, Arusha na Dodoma kuna barabara nyingi nzuri. Lakini siyo Mwanza. Kwa nini siyo Mwanza?

Cha ajabu, Bukoba ambayo ni Manispaa imepewa mradi wa barabara njia nne. Watu na magari yaliyopo Bukoba ni kidogo sana lkn wanapewa barabara hizo, Mwanza wananyimwa. Unadhani hilo ni sawa? Nina wasiwasi Kuna kitu hakiko sawa Mwanza kwenye miundombinu. Kwa nini Mwanza haizingatiwi, shida ni nini? Shida ni Serikali kuu? Shida ni madiwani na wabunge au shida iko wapi?
 
Tatizo wanaona awamu ya 5 ilipendelea sana huko.... Hakuna jipya litakalofanyika tena hadi labda awamu ingine... Kinachofanyika ni kumalizia miradi iliyoachwa basi...na mengine imetelekeywa mfano uwanja wa ndege pasiasi..
 
Bukoba Kuna Barabara ya
Habari Wana jamvi?

Naomba kutoa mawazo yangu kuwa Kuna jambo haliko sawa jijini Mwanza hususani swala la miundombinu. Jijini Mwanza hakuna miundombinu au barabara za kiwango cha jiji Kama ilivyo kwa majiji mengine. Barabara ndani ya jiji la Mwanza ni ndogo, na za zamani.

Ukiangalia barabara ya kutoka Usagara hadi mjini ni ndogo Kama njia moja tu. Barabara Ile husababisha foleni sana, barabara Ile inafaa njia nne. Pia barabara ya kutoka mjini kwenda Igoma/Kisesa nayo inafaa njia nne lkn ni njia mbili kama moja tu kutaja kwa uchache barabara za Mwanza.

Swali; ni kwa nini serikali na viongozi wa jiji hawaoni umhimu wa barabara hizo au barabara zilizopo Mwanza. Jiji la DSM, Arusha na Dodoma kuna barabara nyingi nzuri. Lakini siyo Mwanza. Kwa nini siyo Mwanza?

Cha ajabu, Bukoba ambayo ni Manispaa imepewa mradi wa barabara njia nne. Watu na magari yaliyopo Bukoba ni kidogo sana lkn wanapewa barabara hizo, Mwanza wananyimwa. Unadhani hilo ni sawa? Nina wasiwasi Kuna kitu hakiko sawa Mwanza kwenye miundombinu. Kwa nini Mwanza haizingatiwi, shida ni nini? Shida ni Serikali kuu? Shida ni madiwani na wabunge au shida iko wapi?
Bukoba wanajenga Barabara ya njia nne sababu kuu ikiwa Kona Kali, mteremko na ajali nyingi katika Barabara kuu ya kuingia Bukoba.
Ile sekenke na kitonga ndo Barabara kuu ya kuingia mjini Bukoba ilivyokuwa, ukikosea kidogo unajikuta kwenye paa LA mtu na zimekuwepo ajali za namna hii karibu Kila mwezi. Bukoba ni mji uliopo kwenye valley au basin.
Serikali umeanza kutengeneza Barabara kuu hiyo ya Uganda kwa kuifumua kabisa na kupasua mlima kuondoa mteremko( sasa imefungwa kabisa) kuwa ya njia nne Hadi bandari ya Bukoba km 5.1. Lengo ni kupunguza hizo ajali.
Sasa magari yote ya kuingia Bukoba yanapitia kashura road...ni kweli Bukoba Kuna foleni

Kuhusu Mwanza Barabara ya kenyata na Igoma road wazipanue kuwa njia nne hata kwa awamu kama wanavyofanya Bukoba
 
Ebu imagine lile daraja likamilike, magari yaanze kumwagika yakitoka huku na kule, unadhani foleni ya Usagara hadi mjini itakuwaje ?
 
Mwanza haina chake tena mfano Kiwanja cha ndege propoganda zinaendelea hakuna kitu sembuse hizo barabara kisingizio wanajificha kwenye kichaka cha Mwanza ilipendelewa,mbona Dar na Dodoma zilipendelewa zaidi kipindi cha awamu ya 5 kama ndivyo hivyo.
 
Hakuna jiji lolote Tanzania lenye miundombinu ya kisasa au inayoendana na mahitaji ya jiji husika,kote ni ovyo. Hiyo miji iliyoitaja haina miundombinu mizuri kama unayosema inayo. Yote haya yanasababishwa na upumbavu wa wananchi na viongozi wao.
 
Back
Top Bottom