Mwanza jiji zima hakuna Brown Bread?

Mwanza jiji zima hakuna Brown Bread?

Kuto kujua kwao, haimaanishi bidhaa hiyo hamna, wao huenda Dukani kununua mkate, lakini hawajaulizia mkate wa namna hiyo.

Mimi nipo Dar, ukiniuliza swali la wapi utapata mkate wa namna hiyo, sina jibu, kwa sababu haijawahi kuwa hitaji langu.
Uko sahihi. Inaweza ikawepo sema haijulikani kwa jina hilo. Sehemu nyingine wanaita “mikate ya wenye kisukari”😄. Yani ukiulizia brown bread hawafahamu.
 
Uko sahihi. Inaweza ikawepo sema haijulikani kwa jina hilo. Sehemu nyingine wanaita “mikate ya wenye kisukari”😄. Yani ukiulizia brown bread hawafahamu.
Kweli wengi wanaijua kwa mikate ya wagonjwa wa sukari
 
Juzi kati nilikuwa Mwanza, sasa huwa mimi sipatani sana na hivi vitu vilivyo kobolewa aunatakaga kupunguza, kwamba vingine basi viwe ni vile havijakobolewa kama ngano.

Nikauliza wenyeji wangu kwamba nitapata brown bread Mwanza? Wakaniambia ndio nini hio nikawaambia mikate ambayo ngano yake haijakobolewa, wakaniambia hawajawahi ziona na hawazijui, Ikabidi sasa nianze kuzunguka kwenye Super Market ndogo ndogo zote hakuna, nikapata wazo la kwenda Rock city Mall, Kufika kule yaani ndio kabisa hata staff hawaijui, nilichoka sana fikiria Jiji kubwa kama lile hakuna products kama zile.

Ikabidi ninunue unga wa ngano wa Atta nikapike Chapati nyumbani.

Nikakumbuka Arusha au Dar mikate kama ile unakuta nayo maduka ya mitaani kabisa ukiachana na Super Markets.

Mwanza ni ukubwa tu ila ni jiji la kishamba sana huwezi compare na Arusha au Dar, tuiacha Dar ni kubwa sana ila huwezi ilinganisha na Arusha kamwe.
Huoni kuwa kwa Arusha bidhaa kama hizo lazma zipatikane kwa sababu ya utalii?unamuuzia msukima.brown bread aupeleke wap?ni kama na wao walivyo na vya kwao ila Arusha havipo...ni nadra sana kuipata michembe au kichuri ukiwa Arusha
 
Upatikanaji wa bidhaa fulani hutegemea demand ya bidhaa hiyo kwenye soko.

Ikiwa mji wa Mwanzo, wenyeji wake sio watumiaji wa Brown bread basi hakuna bakery itakayokubali kutengeneza aina hiyo ya mikate na kuingia hasara ya kukosa wanunuzi.

Arusha na Dar, kuna walaji wengi wa brown bread hivyo upatikanaji wake ni rahisi. Na hiyo ni sababu ya wingi wa wageni kutoka mataifa ya Ulaya ambao wengi wao hupendelea sana aina hiyo ya mikate.

Jiji la Mwanzo limejaa Wasukuma ambao hawajui kabisa brown bread ni kitu gani.
 
Mkuu ujatafta tu ila ipo kibao mimi mzee wngu anaumwa kisukari na kila siku anatumia brown au hujatafta mwanza mjini
Yawezekana mkuu ipo sema jina ndo kaliweka k malkia zaid likawachanganya wasukuma...yawezkana inatambulika kama mikate ya ku.........mayo....ila yeye katumia neno la ushuani
 
Juzi kati nilikuwa Mwanza, sasa huwa mimi sipatani sana na hivi vitu vilivyo kobolewa aunatakaga kupunguza, kwamba vingine basi viwe ni vile havijakobolewa kama ngano.

Nikauliza wenyeji wangu kwamba nitapata brown bread Mwanza? Wakaniambia ndio nini hio nikawaambia mikate ambayo ngano yake haijakobolewa, wakaniambia hawajawahi ziona na hawazijui, Ikabidi sasa nianze kuzunguka kwenye Super Market ndogo ndogo zote hakuna, nikapata wazo la kwenda Rock city Mall, Kufika kule yaani ndio kabisa hata staff hawaijui, nilichoka sana fikiria Jiji kubwa kama lile hakuna products kama zile.

Ikabidi ninunue unga wa ngano wa Atta nikapike Chapati nyumbani.

Nikakumbuka Arusha au Dar mikate kama ile unakuta nayo maduka ya mitaani kabisa ukiachana na Super Markets.

Mwanza ni ukubwa tu ila ni jiji la kishamba sana huwezi compare na Arusha au Dar, tuiacha Dar ni kubwa sana ila huwezi ilinganisha na Arusha kamwe.
Mimi nilitaka kununua Pound sterling ilinichukua siku tatu kuzipata,Mwanza naipenda sana ukiondoa issue ndogondogo kama za Brown bread Mwanza patamu alafu bata bei poaaaaa tu.
 
Wakati wewe unaona hiyo mikate ni mizuri kwa afya wao wanaona supu ya samaki, ugali n.k ni vyakula vizuri kwa afya zao.

Alafu unakulaje mkate Mwanza nawewe, Yani unazunguka mji mzima unatafuta mkate???

Ukija huku kula ugali wa mtama na samaki, ukirudi Dar Shemeji atakushukuru sana 😂😂
Mwanza breakfast nI viazi vitamu +karanga ...ndo maana majitu ya huku kwel ni miraba minne
 
Mwanza breakfast nI viazi vitamu +karanga ...ndo maana majitu ya huku kwel ni miraba minne
Na hakuna vitambi vya ovyo ovyo maana wanakula wanga na samaki lakini wanachoma mafuta kwa kazi ngumu.Wanaume wa Mwanza na waheshimiwe
 
Na pia afya zao zipo njema,wanakula fresh Samaki kutoka ziwani tena wa kuchemsha au kuchoma na ugali wa dona uliochanganywa na unga wa muhogo.Saa ngapi wapate magonjwa ya uhitaji hata kuchagua vyakula.
Nakubaliana na wewe
 
Back
Top Bottom