Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,504
- 911,249
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?
Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?
Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?
ulipotelea wapi? Nilikumissije
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?
Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?
Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?
Mwanaumme bila kazi hapendeki
Shida akililiwa visingizio kibao
Kumgalagaza mwenzie kitandani haoni kero
Lakini matunda yake kamwe hayali
Mwanaumme ni nini haswa?
Binti alijipanga bila ya zengwe
Yalikuwa matunda ya ushauri nasaha
Mwenzie alimpasha amalizane naye
Naye aliafiki na sasa matunda yapo hadharani
Mwanaumme ni nini haswa?
Rafikiye alimwuuma sikio naye akaafiki
Kisa mkomoe na uja wepesi
Mengineyo yatajipa sasa ni kilio
Kijana kaingia mitini na hataki tena
Mwanaumme ni nini haswa?
asante mkuurutashubanyuma hoja hii ni tatizi,
ni hoja tata vizazi hata vizazi,
siyo hoja ya wajenzi wala wapagazi,
chanzo chake ni nyumbani, aina ya malezi,
umelelewaje?
Kwani kwenu mko vipi, ni kipi cha thamani,
kwenu shujaa ni yupi, yule mnaye thamini
nani kwenu ni kapi, asiyetakiwa nyumbani,
kipi mnachothamini?
Kama nguo ndiyo mali, elimu ni vuvuzela,
basi hata wanawali, wamachinga watawala,
watapenda suruali, elimu kwao jalala
mnakuzwaje?
uanaume ni sifa, si maumbile ya jalali
uanaume si shufaa, au uwe jabali
uanaume ni kufaa, jamii ikukubali,
ni sifa ya uongozi.
siyo kuvunja vitanda, au hodari kufanya,
uanaume sawa sanda,hutunza si kutapanya,
uanaume si kupinda, au tabia za panya
uanaume utu wema
mwanaume huwa kinga, kiongozi familia,
hana sifa za kijinga, masuala hufuatilia,
kama likizuka janga, hawezi kulia lia
ni sifa ya utume.