Wakubwa zangu shikamooni!
Peopleeeeeeees!
Kama kawa kama dawa nimeletakwenu Mada dume, mada champions league!
Lazima pachimbike hapa! Hii ni kazi chafu ila lazima mtu aifanye, na
huyo mtu ndo nimejitoa muhanga!!!!!
1. Kutoka na mtu anaejiweza kuna sifa bwana asikwambie mtu!!!!!! Kila
mtu anaona umeukata (Japo kiukweli sina lolote) ila tu jamii kukukubali
kiaina na kukuwazia positive jst because ni Demu wa flani kuna raha yake
wajameni!
2.Self esteem na comfidence level approaching 1000% Dah! Yaani among all
choices alizoweza kumake kanichagua mie!!!!!!!! Bonge ya achievement na
accomplishment hiyo!!!! Kwenye hierachy of Needs self satisfaction iko
juu mbayaaa!
3. Its always about him!!!! Kila saa anajiongelea yeye na mikakati yake!
Sasa kwa mtu kama mie mwenye past ya kuficha ficha si manajua every
Saint has a past na every sinner has a future!!! inakuwa afazali nageuka
msikilizaji na msapotiji tu! ! Ila mlalahoi lazima akujue in
details!!!!!
4.Tittle! Unatoka kuwa little Miss No Body hadi Demu wa Flani! Si mchezo
atiii! You share his glory! Hata wanawake wenzio wanaanza kukunotice
Kubwa lao ukikatiza!
5.Gifts na Shopping!!!!!! Daaaaaah! Kwa raha zako unajimwaga! Sio
anakupa coz anakupenda sanaaa, nooo! Coz kwake ni mambo madogo sanaaaa!
He can afford! I dont care! Japo mlalahoi akikupa ujue amekuthamini
sanaaa!
6.Networking na Exposure! Na wewe unaanza kukutana na watu wa maana,
kwenda sehemu za maana na kuwa wa maana! Si yule chausiku wa mtaa wa
pili, ila ni Madam Chau!
7. Social approval unaipata fastaaa! Jamii haiweki vikwazo visivyo na
tija! Kila mtu busy kujikomba komba nae aponee hapo hapo! Mashosti hata
kama Iddi Amini Dadar watamsifu handsome tena baby face!
8.Pressure na wogawoga wa kuishiwa na kurudi kijijini unakuisha! Mambo
ya kuhesabu tarehe yanakuisha! Kila siku kwako mwisho wa mwezi!
9. Watoto ukizaa huna stress kabisaaa, insurance za kumwaga unajua kesho
yao iko guaranteed!
10.Dreams come true! Kama mwenyewe ulikuwa na ndoto zako kuzitekeleza
njenje!!!!!!!!
Wewe wapenda nini?