Mind control (udhibiti wa akili)

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,526
14,399
🤜 NA Olyme Songo III

Maisha yamekua fumbo pale utakapojiuliza baadhi ya maswali mbali mbali kuhusu wewe, haswa utakapo jiuliza "mimi ni nani ?", Nimetokea wapi ?, nipo hapa kwa kusudi gani?

Na pale akili yako ikianza kupata majibu baadhi ndipo utajiuliza ni nani chanzo cha haya yote. Ukiwa mtu wa dini huwezi kufika hata hatua ya kujiuliza maswali hayo sababu imani haitaki maswali, hata ukiuliza mnapewa majibu yasiyo na fact yoyote ila yatazidi kukufanya uendelee kuamini.

Kwa wengi maisha yanaonekana ni fumbo lakini kiuhalisia sio fumbo kwa maana tafsiri ya maisha hutokana na Intelijensia(/intelligence) yako, uwezo na upeo wako wa kuelewa.

Sababu inayofanya maisha kuwa fumbo ni kwa sababu baadhi ya vitu muhimu havipo wazi kwako na vitu visivyo halisi vimefanyika halisi kwako.

Uwezo wa kuelewa kuhusu maisha hutofautinana kwa mtu mmoja hadi mwingine kutokana namna gani mtu huyo amefanikiwa kuyajua yale aliyofichwa na kutambua yote yasio halisi.

Wengi wetu humu, tunamjua adui wa nje, tunajua Mfumo maisha usio halisi(Matrix) ndio unaofanya hali inakua hivyo, mfumo fake unaongozwa na watu wachache ambao wanacontrol nyanja zote muhimu, nao wameishika dunia.

Kizazi cha reptilia ndio kinadidimiza safari yako ya utambuzi kwa mbinu za hali ya juu (tricknology) kwa kutumia mbinu zinazowawezesha kuikamata akili yako.

Lakini yupo adui mwingine aliye ndani yako mwenyewe ambaye ametengenezwa na huyo adui wa nje unayemjua(reptilia bloodline).

Kwa kutumia tricknology watawala wa dunia hii wamefanikiwa kuigeuza akili yako kuwa adui yako na kukusababishia uharibifu , ingawa akili ikitumiwa kwa usahihi ni kitu kizuri mno sana. Kwa maana akili ni kakitu kadogo sana katika ufahamu/intelijensia kanakotusaidia kutufanya tusiwe kama wanyama, maana bila ya akili nasi tungekua ng'ombe kama ng'ombe wengine.

Amin amin nakuambia, akili (mind) yako ni moja ya adui yako mkubwa katika safari yako , na ndio maana adui wa nje hufanya kila kitu ili kudhibiti utendaji kazi wa akili(Mind) yako.

Kwenye maandiko ya wanubia ya holy tablets wa viumbe jamii ya satanist ndio viumbe wabaya wanaotafuta control minds(akili) wakishiriiana na wa lucifeians ambao hukontrol energy(nishati) na hao ndo wanaohusika na udanganyifu.

Umefanyika mtumwa wa akili yako mwenyewe, tena usipotaka kuamka, utakua mtumwa wa kifungo cha maisha, mpaka unapokufa. Badala ya kuiongoza akili yako, akili ndo inakuongoza wewe.

Muda wote akili (mind) hukupigia kelele na kushindwa kuisikia ujumbe kutoka utu wako wa ndani ulio uhalisia wako. Muda wote akili inawaza, inawaza hili haijamaliza hili inawaza jambo lingine.

Najua umeshawahi kumwona kichaa, kichaa muda wote huongea kwa sauti maneno mengi bila kuongeleshwa na mtu au kumwambia mtu.

Kusema kweli hivyo ndivyo na sisi tulivyo isipokuwa sisi hatuyaongei kwa mdomo yakasikika.

Sauti usikiazo kutoka kwa kichaa hayo ndiyo mawazo yake yatokayo katika akili(mind).

Akili hutuwezesha kufikiri, kuwaza lakini ubongo ndio unaowezesha majukumu yote ya akili
Mawazo yetu hutoa maoni, kasoro, kommenti, hukumu, ufanano, sometimes hupenda au kuchukia n.k.

Na wakati mwingine mawazo huja katika mfumo wa picha, yaani "imagination" lakini cha ajabu mawazo hayo huwa hayahusiani na muda au mazingira uliyopo, bali kila kitu unachowaza hutokana na wakati uliopita.

Hata kama mawazo yako yatahusiana na kinachoendelea muda huo ni lazima yatatafsiri kinachoendelea kutokana na mambo kadhaa yaliyopita.

Unaweza ukawa unakula na ukasema chakula ni kitamu, lakini tafsiri ya utamu inatokana na ladha mbali mbali za hapo awali.

In short mind haijawahi kukaa katika hali iliyopo(present moment)

Kwa wanaofanya meditation nadhani tunaelewana, dakika chache za mwanzo mawazo hukatiza sana katika ufahamu wako, na lengo kuu la meditation ni kukuwezesha kutuliza mawazo yote ambayo ni kelele kwenye utu wako wa ndani (higher self), na kuacha ukimya, Na pale unapokuwa tuliza akili yako kuwa kimya unakua umejiunganisha na uhalisia wako, utu wako, present only neither past nor future.

Hapo unakua haubughuziwi na FUTURE(wakati ujao) wala PAST (wakati wako uliopita) maana yake unakuwa katika PRESENT (wakati uliopo).

Ukiichunguza akili(mind) yako, utagundua muda wote hukuletea mawazo yanayohusu wakati uliopita au wakati ujao.

Mara mpenzi wangu kaniacha mara nitajenga nyumba, mala baadae nitakula nini, yaani ni kelele mwanzo mwisho.

Naam hiyo ndio kazi ya akili(mind), akili hupenda kufikiri.
Kamwe huwezi kujiunganisha na utu wako wa ndani au kui experience hali iliyopo(NOW/PRESENT) kama utakua unatumia akili.

Kufikiri/akili sio sawa na ufahamu(consciousness) au fikra haiendani na ufahamu , fikra haziwezi kuwepo bila ya ufahamu, ila ufahamu unaweza kuwepo bila ya kufikiri(/akili)
Hata ukiwa unafikiri na kutafakari ili kutatua tatizo unaweza kujihisi unatumia akili kutatua matatizo yako, my brothers and sisters you are completely wrong, Akili hupenda kufikiri, kuwaza na kuwazua yaani ni kama vile mbwa apendavyo kutafuna mifupa. Na kamwe ufanyavyo hivyo hautumii akili, bali akili ndiyo hukutumia wewe, yes it Uses you, sababu umefanyika mtumwa wa akili yako mwenyewe, mfano rahisi ni mtu aliye athirika na pornography, yaani huyo akili inamtumia nje nje bila kificho naye kwa utiifu humtumikia Master wake.

Bila akili unapoteza utambulisho wako(identity) sababu akili ndio iliyokupa utambulisho, na utambulisho huo ni fake sio halisi(delusions-maluweluwe) utambulisho wako halisi utautambua pale utakapoizuia akili iache kufikiri. Na ndo maana wataalamu husema kiwango cha juu cha meditation ni kutofikiri kuhusu chochote.

"The highest level of meditation is to think nothing"
Akili hupenda kufikiri kuhusu yaliyopita na yajayo, na ukiona inakuwia vigumu kuzuia kuwaza yaliyopita au yajayo, hapo sasa ndo unielewe nilivyosema kuwa " huwa hautumii akili bali akili ndo huwa inakutumia wewe", Unajua kwa nini? Kwasababu identify yako, utambulisho wako uliupata baada ya kuiruhusu akili yako ikutumie kwa sababu wewe u mtumwa wa akili yako, nayo akili, ikakuambia wewe ni mariamu, wewe ni masikini, wewe ni mrembo, wewe unapendwa sana n.k kwa sababu yenyewe imefanyika bwana wako(slave master).

Lazima uone kama haiwezekani kukaa bila kufikiri chochote, sasa ukiizuia akili yako wewe utakuwa nani? maana yake utakuwa si chochote, ukuu wako, cheo, title yako hapo mtaani na identify zako zote ulizopewa na akili zitapotea. Je ukiizuia akili wewe utabakia nani?

Without mind, who are you?

Bado akili itapenda kuwaza yajayo, future ili kujihakikishia maisha.

Amini amini nakuambia , ukizuia mawazo yako (-ya nyuma na yajayo-) hapo ndipo mwanzo wa kujitambua wewe ni nani, Na hiyo ndio huitwa ENLIGHTENMENT na wanadini ya kibudha.

Na ndo maana Wabudha husema kwamba, "kuangaziwa ni mwisho wa masumbuko yote"
"Enlightenment is the end of all suffering"

Kwa sababu mateso na masumbuko yote yanatokana na Mawazo yetu,fake identity tulizopewa na akii zetu.

Maisha sio fumbo hata kidogo, watu wanaoshindwa kuishi PRESENT, kamwe hawajawahi kupata furaha ya kweli, amani ya kweli, upendo wa kweli. Yaani wamejawa na maumivu kila sahemu, pain every where, ndoa hazina raha, ndoa hazina upendo. Hata kile mnachoita upendo sio upendo huo ni delusion, baada ya muda (euphoria period) penzi linakufa, why?

Upendo, furaha, amani vyote vipo ndani yako mwenyewe, tatizo lenu mko bize kutafuta upendo kwenye mahusiano, furaha kwenye mali na pesa na kamwe hamjawahi kuupata huo upendo,furaha na amani yaani pain everywhere.

Nimesema yote yapo ndani yako nami nipo hapa kama mjumbe kukuonesheni Njia, yes I'M SONGO, i am showing you the way.

Stay connected with me till the end, chief are cooking delicious 😋 food for you

Scribed by👇
Olyme Songo III
 
🤜 NA Olyme Songo III

Maisha yamekua fumbo pale utakapojiuliza baadhi ya maswali mbali mbali kuhusu wewe, haswa utakapo jiuliza "mimi ni nani ?", Nimetokea wapi ?, nipo hapa kwa kusudi gani ? Na pale akili yako ikianza kupata majibu baadhi ndipo utajiuliza ni nani chanzo cha haya yote. Ukiwa mtu wa dini huwezi kufika hata hatua ya kujiuliza maswali hayo sababu imani haitaki
Vizuri
 
Dokta umeona nondo hizo!

Halafu madokta ndio wako mstari wa mbele kuwa brainwashed na mind-controlled.

Hizi nondo zinaanza kutikisa kidogo ile brainwashing kwa mbali.

Hata kuvaa STETHESCOPE nayo ni brainwashing pia.
HYa ndo mambo Yangu BICHWA KOMWE - sema tu Muda mwingi huwa siyazungunzii kwa sababu nitawatisha watu na kuwakatisha tamaa ya kuishi..

Ukweli unatisha ,Ukweli unaumiza,Ukweli unaogopesha Na huwa natamani kuusema ila nahofia watu kuupokea..

Watu wamedanganywa kwenye Dini,Maisha ya kawaida wamewekewa Uongo wanaouona wao ni ukweli, Wametishwa sana..
Kuwaondoa huko Inakubidi kufanya Jitihada kubwa sana
 
HYa ndo mambo Yangu BICHWA KOMWE - sema tu Muda mwingi huwa siyazungunzii kwa sababu nitawatisha watu na kuwakatisha tamaa ya kuishi..

Ukweli unatisha ,Ukweli unaumiza,Ukweli unaogopesha Na huwa natamani kuusema ila nahofia watu kuupokea..

Watu wamedanganywa kwenye Dini,Maisha ya kawaida wamewekewa Uongo wanaouona wao ni ukweli, Wametishwa sana..
Kuwaondoa huko Inakubidi kufanya Jitihada kubwa sana
Tuambie Dr ili tujitambue
 
Great post! Very interesting. Sasa nifahamishe kidogo kuhusu akili. Umesema aikili ndio inatutumia na sio sisi binadamu kuitumia akili. Yaani we are controlled by our minds. That means we can not tell our minds what to do. Sasa shida yangu ni vipi wale tunasema wana akili sana kama wazungu na wachina? Na tunawasifia kwamba gunduzi zao na higher technologies?? Na vipi mwanafunzi darasani anaposhindwa kujibu maswali na hata kufeli mitihani na akaambiwa hana akili? Je ni kweli kuna akili nyingi na kidogo?
 
HYa ndo mambo Yangu BICHWA KOMWE - sema tu Muda mwingi huwa siyazungunzii kwa sababu nitawatisha watu na kuwakatisha tamaa ya kuishi..

Ukweli unatisha ,Ukweli unaumiza,Ukweli unaogopesha Na huwa natamani kuusema ila nahofia watu kuupokea..

Watu wamedanganywa kwenye Dini,Maisha ya kawaida wamewekewa Uongo wanaouona wao ni ukweli, Wametishwa sana..
Kuwaondoa huko Inakubidi kufanya Jitihada kubwa sana
Ukweli unatisha sana.

Shida yangu kwako dokta ni yale madonge unayowapa watu kule hospitali, hivi unaona ni sawa au unatuchezea akili dokta wangu?
 
hivo ulivyoandika na kupangilia uandishi wako pamoja na mawazo ni akili au ufahamu?kujua baya na jema ni ufahamu ndiyo je kufanya maamuzi ni akili au ufahamu?
 
Back
Top Bottom