Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Nisome vizuri, linahusu sana Uislam, huwezi ukajipachika jina ambalo linaleta maana tofauti na isiyotahiki katika Uislam.

Unajuwa nyinyi dini zenu mnachukulia kama zipo zipo tu, sisi tupo very serious na mfumo wetu wa maisha, hatutaki utani na Uislam na Mtume yeyote wa Mwenyeezi Mungu. Kumbuka hilo.

kwa hiyo unamkana muislam mwenzako?
 
Daah..........eti kwa uadilifu na uaminifu........aisee sikujua kama sijui kiswahili kiasi hiki.
 
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali dalili zote zilianza kuonekana mapema tangu alipochaguliwa kwa tabia yake ya ubabe, kauli chafu/ dharau na kuchanganya taaluma ya sheria, ufisadi pamoja na siasa. Tulio wengi tulijua tu mzee wetu hata fika mbali atatumbukia tu kwenye shimo. Na ndivyo ilivyokuwa kwani hata baada ya kujiuzulu haiondoi ukweli kuwa jambo hili lilikuwa kweli, kubwa na hatima yake ameng'ooka. Afadhali aliyekuwa mwanasheria za Zanzibar ambaye aliamua kufa kiume kwa kutokubaliana na upuuzi uliokuwa unafanywa na Bunge Maalum la Katiba. Neno tumbili sasa limegeuka kuwa shujaa.
 
Kumshukuru Mtu kwa uaminifu wake na uadilifu wake kwa sakata lake la kuisababishia serikali hasara hadi kufikia bunge kuibua mjadala mkubwa kuwahi kutokea ni ISHARA YA USHIRIKI WA IKULU KATIKA WIZI HUO TENA KWA USHAHID WA WAZI KABISA

HUYO ANA UADILIFU NA UAMINIFU GANI?

KUMBE WIZI HUU MMESHIRIKIANA WOTE KABISA

Du wewe jamaa bwana. Jaya acha nikupe tu like.

Controler like your post
 
Chakushangaza na kusikitisha ni kwamba uchaguzi s/mitaa ulifanyika jpil ghasia kazungumza jtatu ma DED wametimuliwa jtano haina maana coz wao ni wasimamizi wa uchaguzi hata km karatasi zimekosewa ni wizara ndiyo concerned mambo ya werema tumeshayamaliza tunasubiri kumfilisi kupitia ripoti ya takukuru
 
Tumbili jizi limejiuzulu ,,,basi vizuri na yule mkulima nae vipi,,,
 
Acha ujinga wewe, uhoro uandike wewe, halafu unasema hatujaelewa. Inaelekea hata ulichoandika hukijui. Nahisi ule mkito wa usiku umekupa ganzi. Hayo ndo madhara ya kushika ukuta

Hahahaa haaaa
Uwiii
 
Wewe nilikwambia siku nyingi badili hiyo ID, haikufai. Usifikiri Waislam ni wajinga, hakuna kitu kama "Abdul Mohamed".

Kujibandika majina muonekane Waislaam huku hamjuwi kuwa hayo majina yana maana zake na watu hawakurupuki tu.

Mjinga takaesoma id yako atasema aaah, huyu ni Muislaam, kumbe?????/ kafata ujinga. Ni hayo hayo, mnakurupuka na jina la nyuzi bila kuisoma nyuzi. Poleni sana.

Kasome vizuri, wote mnakurupuka na kichwa cha habari, maudhui hamjaisoma.

Tatizo ni shule, mlienda kusomea ujinga.


FaizaFoxy

Haya yalikuwa maneno yako katika Thread yako uliyoianzisha; Usikikimbie kivuli chako, kipokee na kukiri kuwa unahitaji muda wa kutafakari na siyo kuweka ushabiki kwa jambo usilolifahamu,

Taifa kwanza Vyama baadaye>>>>>>>>>>>

===========================================================================

Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow
Baada ya kusikiliza ripoti rasmi ya PAC iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nnadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.

Ni drama tu lakini hakuna kipengele chochote cha sheria ambacho hakijibiki au kilichooneshwa kuwa kimekiukwa.

Hukumu ya Mahakama ni ya halali na haina utata na Zitto wala CAG wala TAKUKURU hawajaonesha kuwa ilikuwa ni batili au ya kughushi.

Zitto kapiga porojo nyingi sana kuliko ukweli, na mwanasheria yoyote mahiri anazisambaratisha hoja zake zote ndani ya nusu saa.

Zitto ametetea sana BoT lakini alichoshindwa kuelewa ni kuwa Bot kama wakala ndiye alitakiwa aridhike na vielelezo vyote kabla hajalipa na kama havijakamilika hawezi kutoa fedha. Zitto anasema eti Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye alimuamuru Gavana hizo fedha zitolewe, toka lini Gavana wa benki anatoa fedha kwa amri ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Utata wa IPTL na Standard Chartered ni huko-huko kwao si IPTL iliyokopa, iliyokopa ni Mechmar na Mechmar haiwezi jitokeza kwani imeshafilisika kisheria, Standard Chartered karata yao ya mwisho ni hii na hapa wamepata mwanya.

Nnasikitika kusema na nnaliona linakuja la Serikali kuingia gharama kubwa ya kulipa zaidi ya mara mbili au tatu hizi fedha ikiwa watafata akili za akina Zitto.

Nnashauri, wajadili hili suala bungeni lakini shauri liwachwe kesi kumi zilizopo mahakamani zinazoihusu IPTL zikamilike.

Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.

Isitoshe, fedha zilizolipwa escrow si kamili, hizo zilizobaki zilizuiliwa kwanini? Jibu tutalipata kesho na ndilo litakalosambaratisha hoja ya kodi ya Zitto.

Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri kesho, tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu. Na hapo ndipo mtamjuwa Chenge ni kichwa.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Watanzania tubadilike, Mafisadi wanakula sisi tunashabikia umasikini wetu.

Tuwe kitu kimoja kulitetea Taifa letu kwa manufaa ya kizazi cha watoto wetu.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!
 
Mbona JK anazidi kulikologa?Kwa mtaji huu Wazungu hawatampa pesa za misaada.Yeye anasifu badala ya kuchukua hatua za kisheria?Pole sana JK Tanzania itafungiwa misaada mpaka mwisho wa utawala wako.
 
Mbona JK anazidi kulikologa?Kwa mtaji huu Wazungu hawatampa pesa za misaada.Yeye anasifu badala ya kuchukua hatua za kisheria?Pole sana JK Tanzania itafungiwa misaada mpaka mwisho wa utawala wako.

Mtu anaiba mabilion ya hela AF anaenda kuomba vyandarua na dawa ya mseto nonsense kabisa
 
Ndio maana wezi hawaishi TZ, yani mtu anakwiba wee. halafu akikamatwa anajiuzulu. EBO..

Kuanzia sasa hakuna haja ya mahakama kupeleka watu segerea kwa kesi za wizi..,Wanaokamatwa wote waandike barua za kujiuuzulu.wakatumbue matunda ya ujambazi wao.

Imagine mwizi anakamatwa halafu kabla mahakama haijamhukumu anaandika barua ya kujiuzulu ujambazi huo kwani aliowaibia hawakumuelewa.
 
Ccm imepeta wapi? Kwenye mapingamizi? Hivi wenzetu mpo nchi gani? Wewe ni mmoja ya wasiojitambuwa kwa kulishwa takwimu uchwara na Nape.

Na kweli mkuu nimetumia takwimu za Nape. Hebu tupeni matokeo kamili ili tusimuamini Nape.
 
Ccm imepeta wapi? Kwenye mapingamizi? Hivi wenzetu mpo nchi gani? Wewe ni mmoja ya wasiojitambuwa kwa kulishwa takwimu uchwara na Nape.
Nilitarajia kwa kashfa kubwa kama escrow watu wanaojitambua wangeamua kuipiga chini ccm kwenye uchaguzi (mfano ingepaswa iwe UKAWA kashinda kwa silimia 97 na ccm 3%) lakini si umeona matokeo mwenyewe?
 
Back
Top Bottom