Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

aibu sana
 
...Kafulila apelekwe mahakamani....au Werema?....sorry namaanisha aliyesema UONGO Bungeni

:ban:

I am confused eti kati ya viroba na wigiiiii kipi kinalewesha?
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu
.
Hapo kwenye red ndo nspata homa miye, na kipindu pindu kabisaaaa!
Yale yale ya Waziri Mkuu mstaafu " aliyejiuzulu".
 
Wakatii mwingine Mr. president kukaa kimya kunakujengea heshima, haya mambo ya kuropoka ropoka yanakukushushia hadhi zaidi. Hivi hiyo kauli ya kusema "Unamshukuru AG kwa utumishi uliotukuka" kwa aliyoyafanya Werema hivi nani anakuelewa kwa kauli hiyo?

Mheshimiwa rais kauli zako zina-reflect mengi juu yako, kauli hiyo haikubaliki hata kidogo!
 
wabongo bhana!! Mtu ameshastaafu kwa mujibu wa sheria leo ndo mnapumbazwa nanyi mnapumbazika na kushangilia halafu mnajiita gts.kweli?

naomba soma vizuri sana hapo kwenye nyekundu. Werema anatakiwa kustaafu october 9, 2015

attachment.php
 
Mr Dhaifu ni Rais wa hovyo kabisa na ni dhaifu kuliko hata keki , yaani hana ubavu wa kuwawajibisha wezi wenzake anasubiria usanii wa kujiuzulu na kusifiana kipuuzi puuzi.
Nazidi kumdharau sana.

Yeye ni miongoni mwao. Umewahi kuona captain wa timu anasaliti timu wakati lengo lao ni ushindi.
 
Kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema ni wazi sasa nafasi hiyo inabaki wazi.

Kwa walio wadau wa tasnia hii ya sheria nadhani wataungana nami pasina shaka lolote kuwa kutokana na nafasi hiyo kuwa nyeti kwa ustawi wa Taifa lolote lile duniani, inahitaji kushikiliwa na mtu mwenye nidhamu, weredi na mwenye uadilifu wa hali ya juu.

Kwa wasomi na wanataaluma wa sheria nchini wenye sifa hitajika ni adimu sasa kwa taifa letu hili kwa sasa, binafsi namfahamu vyema Mhe. Jaji Feleshi licha ya kufanya nae kazi kwa muda wa miaka michache lakini ni mtu ambaye ukimweka na viongozi waandamizi wenye hadhi yake ni kama mtu aliyeshushwa toka peponi.

Hakuna mtu wa kada yeyote anaeza ongea swala la hongo kwa Mhe. Jaji Feleshi, kwa kipindi chote nlichofanya kazi pale Sukari sijawahi ona mfanyakazi wa kawaida akimtangulia kufika ofisini na akimuwahi kutoka ofisini, sikuelewa nia ya Mhe Rais kumtoa kwenye uDPP lakini huenda alikuwa akiandaliwa kushika nyazifa za juu katika muhimili huo muhimu ili kuusuka upya lakini kutokana na ombwe hili katika nafasi ya AG bado sijaona mtu mbadala.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Na Picha ndio limeishia hapa!!
 
Uaminifu na uadilifu kwa mtu kama Wererma?
"Only in Tanzania"
 
huyu Prof Busha inabidi achukue hatua kali sio kuchekacheka

Mtu anajiudhuru kwa wizi Prof Dr Busha anasema anamshukuru kwa uadirifu

HUU NI UPUUZI IT IS ONLY IN TANZANIA
 
Back
Top Bottom