Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.


Rais alitakiwa amkatalie ombi lake halafu amfukuze kazi kama alivyofanya kwa balali.
 
Wacha tu kaka lkn hivi vitu vinachangia sana sisi kuonekana wajinga ndani na nje ya nchi.
President anakuwa sufuri-a (0) namna hii ?
But yeye kwa ujinga wake anajisifu anapiga deal

Mkuu ninkuunga mkono kabisa. Unajua sasa hivi nasikia nchi zilzoendelea zinasema africans are not serious! Sasa ona mama Grace Mugabe amepata Dr. yake ktk kipindi cha miezi 2 na Mugabe mwenyewe akiwa Chancellor wa hiyo University, sasa tell me ............... Kikwete anayofanya pia ni maajabu ya Musa!
 
tunataka werema afike mahakamani

hii hatua sio kumwajibISHA

images

hili laitwa KARANDINGA
 
Tafadhali sana Mh.Rais katika mabadiliko utakayofanya umuache Muhongo katika wizara hiyo hiyo, ili atunyoshee kile kikundi cha T P S F wakiongozwa na yule babu anayemuowa mjukuu wake.....kamwe hatuwezi kukubali mabebari wachache wawe madalali wa gesi....hiyo ni hapana hapana.......natumaini ombi langu limesikilizwa......
Prof Muhongo ni Mhimili wa Maovu
 
kwa taarifa isiyo rasmi muhongo naye atajiuzulu hivi karibuni
 
Ni Aibu kwa serikali hii kukaa na wahujumu uchumi hadi wanapata nafasi ya kujihudhuru!.Kwani mpaka wao wanajibaini kuwa walifanya makosa! na serikali yenye madaraka kamili, inakaa kimya???.
Kweli hii mnatutendea haki wananchi!? Inamaana hamtaki kuwawajibisha kwasababu gani ya msingi?Ukiangalia walio jiudhuru kwa kashifa ya kukwapua mali za umma ni wengi na hakuna yeyote aliye chukuliwa hatua yoyote!. Hila kama kungekuwa na mtu aliyewajibishwa kwa ufujaji wa mali ya umma, nidhahiri watu wangeogopa, ndiyo maana watendaji wa serikali wanaweza kuchukua rushwa kubwa wakijua anaweza akajiudhuru na ikawa poa!. Sasa wabunge pelekeni mswaada bungeni kwa yeyeote atakayepatika na hatia ya kukwapua mali ya Umma akae maabusu kwa miaka 3 then ndiyo kesi yake itajwe na asiwe na dhamana.
 
... Huyu Kalazimishwa Ajiuzulu. Hajataka Mwenyewe, Kwann Amechelewa Sana?
 
Bora kajiuzulu baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa
 
ishu sio kujiuzulu tuu afilisiwe mali zote za wizi ndo ajiuzulu sas anajiuzulu vipi na mihela yote hiyo
 
Hii ya kumsifu kwa uadilifu na uaminifu bado hainiingii akilini.....!
 
Mkuu ninkuunga mkono kabisa. Unajua sasa hivi nasikia nchi zilzoendelea zinasema africans are not serious! Sasa ona mama Grace Mugabe amepata Dr. yake ktk kipindi cha miezi 2 na Mugabe mwenyewe akiwa Chancellor wa hiyo University, sasa tell me ............... Kikwete anayofanya pia ni maajabu ya Musa!

Hahahahaha ile ya Mugabe ni kali yaani mkewe anatoka from secretary then muda mfupi tu anakuwa Dr....by the way hii nchi ilipofikia ni hatari sana, na anytime soon tutegemee mabadiliko katika baraza la mawaziri.....wahisani na nchi washirika wamebana kila kona, uchaguzi wa mitaa imetoa pigo takatifu, kuna kila dalili zote za kupigwa kura ya maoni ya katiba kuna kula dalili upinzani kufanya vizuri uchaguzi mkuu unless uteuzi wa ccm uwe free and fair.....kwa kifupi hali ni hatari.....
 
Back
Top Bottom