Mwanasheria mkuu wa serikali, jaji Frederick
Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia
leo, jumanne, Desemba 16, 2014 na rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Taarifa kutoka ikulu zimesema katika barua
yake kwa mhe. Rais Kikwete, jaji Werema
amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa
sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya
akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na
umechafua hali ya hewa.
Mhe.Rais Kikwete amemshukuru jaji Werema
kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu
na uadilifu.