Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Uaminifu na uadilifu?
"Dunia bila unafiki haiwezekani"
 
Kama yeye kajiuzulu wanaofuata wote wanastahili kunyongwa
 
The worst that could happen to him is step down and keep his money.

The dog and pony show continues.....
 
Sisi bado tunajadili jinsi ya kugawana majimbo 2015 ajiuzulu asijiuzulu sisi wana nchi wa mtaani watatujuwa 2015 kama sisi ni wajinga tutagawana mitaa na majimbo kama wao walivyo gawana kwa rumbesa pesa
 
Ila uturudishie fedha zetu. Kujiuzulu hakusaidii
 
Werema alisema makosa ya Maswi atayabeba yeye mbona kamwachia mwenzake mzigo.
 
Nyerere alisema cheo ni dhamana!,,,,,huyu atakuwa amejiuzulu kwa shinikizo la ikulu.Naamini kabla ya ijumaa tutasikia mengine.
 
JK acha sound bana.
Mpige deal na AG then leo unamwambia ajifanye anajiuzulu, mlipiga deal longtime so AG ana kesi ya kujibu.

Hahahahaha mkuu Tanzania ni zaidi ya ukionacho posta au kariakoo....kuna mengi sana nyuma ya pazia chief
 
Sisi wapenda maendeleo tunamhitaji muhongo abaki siyo vinginevyo tunataka maendeleo.
 
Tumbili anapowafundisha binadam jinsi ya kuishi
 
Back
Top Bottom