Molembe, Ukioa hayo yatapungua, maana mnaelewana ratiba zenu na majukumu yalio mbele. Tatizo ni kuwa unajaribu kumfikiria mwanamke kupitia tabia za kiume, ukitaka kuwaelewa elewa wanawazaje, wanawake wanaenda kwa kusikia, kila kitu umtumie message, umpigie au email inatosha. Wanaume inanoga kwa macho, kama kasafiri atataka video call au picha inatosha. Tofauti ya wanawake na wanaume ingine iko katika kujiamini, wanawake hawana kujiamini kama anapendwa au anamisiwa hata kama alishaambiwa anataka kuhakikishiwa. Mwanaume yeye ni tofauti akishajua huyu ni wangu, hana wasiwasi. Tumeumbwa tofauti, ukiimaster hiyo mkuu wala haikupi shida, tatizo hauko wazi ungekuwa free naye unamwambia tu mapema baby niko busy tuwe tunaongea baada ya kazi jioni, na lunch time unamrushia message yeyote nzuri. Yeye mwenzio anazani anaonyesha upendo kumbe anakuboa.....