Uchaguzi 2020 Mwanamke ajitokeza kuwania Urais kupitia CHADEMA. Ni Msomi, Mwanamke wa Shoka, Ana uwezo na Jembe Kweli, ila...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,497
113,592
Wanabodi,

Baada ya kutulia kwa tishio ugonjwa wa Corona, sasa watu hawana uoga tena, hivyo sasa Vuguvugu la kugombea urais wa JMT uchaguzi Mkuu wa October, limeanza kupanda joto, kwa moto wa urais kuwashwa na mwanadada, msomi wa Ph.D, Dr. Mayrose Majinge, amekuwa ndie mwanamke wa kwanza kujitokeza kutangaza nia ya kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais wa JMT kwa tiketi ya kupitia Chadema.

images (15).jpeg
images (17).jpeg
images (18).jpeg


Kwa vile mimi nimetokea kumfahamu huyu mwanamke msomi huyu, kwanza ni msomi, pili ni mwanamke wa shoka, na anauwezo, yaani kama ni jembe, huyu mdada ni jembe kweli, na ni mwanaharakati wa ukweli ila kuna swali moja tuu najiuliza kumhusu huyu dada, ili ku save space, kwa vile niliwahi kum profile humu mwaka 2013 alipokuwa anagombea uenyekiti wa UWT, naomba uipitie CV kwenye bandiko hili
Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili! - JamiiForums

Kama Chadema ina watu wazuri kama hawa tena wana CV nzito kama hii, walikuwa wapi siku zote hizi hadi mtu kama huyu asiteuliwe ubunge viti maalum Chadema, na badala yake Chadema ikatujazia baadhi ya yale makorokocho kule Bungeni?!.

Jibu langu ni moja tuu, kuna uwezekano ni kweli ubunge wa viti maalum Chadema unapatikana kwa namna fulani, ambayo kwa jinsi ninavyomfahamu huyu dada alivyo ni mtu wa msimamo, ni mcha Mungu, hivyo hizo namna za kumpatia ubunge wa viti maalum Chadema zilimshinda akaamua kutulia, sasa kama ubunge tuu wa viti maalum alishindwa kupewa Chadema, kutokana na misimamo ya kukataa mambo fulani, jee sasa kwenye urais ndio atapitishwa?!

Kwa vile mimi namfahamu vizuri huyu dada na niliwahi kumzungumza humu,

Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili! - JamiiForums
Huko nilichangia hivi
Mkuu Wa Ukenyenge, sina CV yake rasmi ila ni msomi mwenye masters. Sifa yake kuu ni kitabu fulani alichoandika kuhusu vita dhidi ya umasikini!.

Huyu Mayrose she is real good ambaye anaweza kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya CCM kwa ku invoke changes from within!.

Kwa vile huyu ni mdada wa ukweli, bado anaamini a dying CCM can be revived kupitia UWT!. Kumbe bado hajajua, uwongo, fitna na majungu ni mtaji mkubwa wa ushindi kwenye uchaguzi wowote wa ndani ya CCM.

Huyu Mayrose ana tatizo moja kibwa, she is too genuine hivyo kuwa too good kwa CCM, I hope baada ya uchaguzi huu wa UWT, she'll realize she is in a wrong party, anapoteza bure time, money na her very promising potentials to try reviveing a dying CCM!.

I wish her all the best!.
Haya niliyasema tarehe 3 Agust, 2012, leo nimeiona hii picha
Sunday, July 14, 2013
slaa.jpg

Aliyekuwa mgombea UWT Taifa, Maryrose Magige akionyesha kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi Manzese Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao

Kiukweli Chadema imevuna Jembe!. Hata BAWACHA itafufuka na itasimama na kuipuku UWT!.
Hongera Mayrose kwa kuukubali ukweli. Nakukumbusha mane yangu haya
Huyu Mayrose she is real good ambaye anaweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa ku invoke changes from within!.
CCM.

Huyu Mayrose ana tatizo moja kibwa, she is too genuine hivyo kuwa too good kwa CCM, I hope baada ya uchaguzi huu wa UWT, she'll realize she is in a wrong party, anapoteza bure time, money na her very promising potentials to try reviveing a dying CCM!.

I wish her all the best!.

Hivyo naamini, mimi ni miongoni mwa waliomshawishi huyu dada kujiunga Chadema ya enzi ile, na kama amedumu Chadema muda wote huu, bila any recognition ya aina yoyote, then ile Chadema niliyomshauri kujiunga ni Chadema ile, ila kwa Chadema hii...
IMG-20200526-WA0002.jpg

Kwa wale mtakaopata nafasi, tumsikilize hapa asubuhi hii.

Ushauri wangu kwake ni saa hizi hajachelewa, ajirudie tuu nyumbani kumenoga, Chadema is a sinking ship, asipoamua mapema, ana zama nayo.

All the best Dada Dr. Mayrose Majinge.

Mimi ni Kaka yako Mkubwa
Paskali.
 
Salam wanabodi,

Naona joto la propaganda na uratibu wa visa vya kuandaa "watu fulani" wajitokeze kwenye mambo fulani umeanza kwa kasi!!!

Uzi huu hapa chini umenisukuma kutaka kumjua zaidi mmama huyu aliejitokeza mapema kabisaa kuliko vyama vyote vya upinzani!!

Mwanamke Ajitokeza Kuwania Urais Kupitia Chadema, Ni Msomi, Mwanamke wa Shoka, Anauwezo na Jembe Kweli, ila... - JamiiForums


Najua ni haki yake kikatiba,je kwenye siasa,jamii na kimataifa amefanya nini?!! Wote walau tuanze na picha ambatanishi!!!

Salam kwa mwana mama wa 2015 kwenye uraisi,Anna Mghwira!!

EY4idfXWkAIqg9P.jpg
 
Kaka paskali wewe ni msomi wa sheria tena umefundishwa na maprof bora sana

Sasa ukisema kuna namna fulani ya kupata viti maalum chadema means una kubaliana na yale mazungumzo yetu ya watu ambao tunaongea vitu ambavyo sio fact

Turudi kwenye topic:

Huyu mama yuko vizuri sana tena sana but kwa mfumo wa Tanzania kumuweka mgombea mwanamke ni kujizika moja kwa moja
 
Paskali, ni lini uliwasiliana na huyu mama akakuambia kuwa aliwahi kuwa na nia ya kuwa mbunge na akanyimwa? Yaani, unatengeneza hitimisho ili kuunga mkono tuhuma za ngono zilizotolewa na wapenda ngono? Kuna wakati unatumika au unajitumikia kiajabu ajabu sana bro.
 
Back
Top Bottom