Unadhani kwanini CHADEMA wamekubali kupokea Ruzuku lakini Wameshindwa kutetea nafasi zao 19 za Ubunge wa Viti Maalum?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,979
141,996
Kimsingi miongoni mwa mambo yanayosababisha chama cha siasa kipate Ruzuku ni kura za mgombea Urais na kura za Wabunge wa majimbo

Ndio sababu wakati Wabunge wa Chadema wanaunga Juhudi za shujaa Magufuli Ruzuku ya CCM ilikuwa inaongezeka na ya Chadema inapungua

Ikumbukwe Halina Mdee, Makamba, Bulaya, Mwaifunga, Mwakagenda nk waligombea Ubunge majimboni hivyo kura zao zimechangia Ruzuku ya Chadema kuwa nono

Nirudi kwenye Hoja, kama Chadema wameshindwa kutetea nafasi zao 19 za Ubunge wa Viti Maalum watawezaje kuusimamisha Uchaguzi mkuu wa 2025 pasipopatikana Katiba Mpya?

Kama umemshindwa Sungura utamuweza Simba?

Mlale Unono 😀😀
 
Tarehe 14 December 2023 hukumu ya COVID-19 itatolewa. Tuwe wavumilivu.
 
Tatizo la Covid-19 wao ni Kabila zao - linganisha na vitimaalum hapo zamani walikuwa wanatoka mkoa mmoja. Aidha, Mbunge pekee wa CHADEMA (alishinda kihalali) si Kabila hilo, nalo lilimuudhi mbowe na ruling clan.

Ni juzi tu - literary - ndiyo imebidi mbowe na CHADEMA wafyate mkia wamkubali Mbunge Aida (nadhani ni Msukuma).

Ukichunguza vizuri Covid-19 hawana kosa, walitii matokeo ya Uchaguzi huku kina tundulissu wana chuki ya kushindwa na kina mbowe wana chuki ya kikabila.

Kuna uvumi pia kuwa washikaji wa Mchungaji Msigwa na Nyalandu na tundulissu walitakiwa wawemo.

Watu husahau kuwa vitimaalum hipangwa hata KABLA ya uchaguzi, kilichotokea they took No. 1 to No. 20 baada ya No. 8 (Aida) kupita kikwelikweli Jimboni kwake.
 
Sababu kuu ni kuwa hawara zao na ndugu zao hawamo

Hamna cha zaidi ya hapo.Walizoea viti maalumu kujaza hawara na ndugu zao
 
Kimsingi miongoni mwa mambo yanayosababisha chama cha siasa kipate Ruzuku ni kura za mgombea Urais na kura za Wabunge wa majimbo

Ndio sababu wakati Wabunge wa Chadema wanaunga Juhudi za shujaa Magufuli Ruzuku ya CCM ilikuwa inaongezeka na ya Chadema inapungua

Ikumbukwe Halina Mdee, Makamba, Bulaya, Mwaifunga, Mwakagenda nk waligombea Ubunge majimboni hivyo kura zao zimechangia Ruzuku ya Chadema kuwa nono

Nirudi kwenye Hoja, kama Chadema wameshindwa kutetea nafasi zao 19 za Ubunge wa Viti Maalum watawezaje kuusimamisha Uchaguzi mkuu wa 2025 pasipopatikana Katiba Mpya?

Kama umemshindwa Sungura utamuweza Simba?

Mlale Unono 😀😀

Akili mtu wangu ujajaliwa
 
Back
Top Bottom