Unampakaza kwa kumpakaza kwa kuwachomeni sindano ya moto sio, yaweza kuwa dawa msimpuuzeni🤔.David James McAllister, aliyezaliwa January 12 mwaka 1971, ni mtu wa kutiliwa mashaka makubwa anayehudumu katika Bunge la Ulaya (European Parliament) kutokea Ujerumani.
McAllsiter ambaye ana doa kubwa la kuwa mbaguzi wa rangi ana mtetezi mkubwa wa ndoa za jinsi moja (Ushoga) ameonekana kwenye macho ya wachache hapa Tanzania, kupitia video yake wakati akizungumza hoja za uongo zenye lengo ya kuichafua Tanzania.
Pamoja na kwamba hoja zake zilipingwa vikali ndani ya Bunge la Ulaya baada ya kuwepo kwa wabunge wanaofahamu sifa njema za Tanzania, wajuzi wa Diplomasia wanaweka ‘alert’ juu ya McAllister kulingana na historia yake.
Moja kubwa ni kwamba Dvaid MacAllister ni mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Ujerumani, ambalo kihistoria lilijaa ubabe na uonevu dhidi ya mataifa mengi ya Afrika, bila kusahau ujuzi wao wa kutengeneza migogoro katika mataifa ya Afrika kwa maslahi ya vyama vyao.
David MacAllsiter ambaye pia ni mjuzi wa sheria, ni mfano wa Wanajeshi wa mataifa ya kibeberu ambao wametumika kuleta uchonganishi katika nchi nyingi za Afrika, baadae wakaingiza mauaji, mapinduzi ya haramu, machafuko makubwa ya kisiasa, kisha wakateka na kuiba mali.
Katika kufanya hivyo, Wanajeshi wenye hila mbaya kama McAllister, hutumia wanasiasa wa upinzani katika Mataifa ya Afrika ambao mara nyingi wanakuwa wamekosa madaraka. Hujenga nao ukaribu ili wawe chambo ya kuleta uharibifu katika nchi zao.
Ni jambo la kutia shaka, pale ambapo David ameanza kuitupia macho Tanzania. Aanataka nini Tanzania? Ametumwa na nani na watanufaikaje iwapo Tanzania itatatetereka?
Hata hivyo, jambo jema Kwa Tanzania na baya kwa David McAllister, ni kwamba hoja zake za uongo dhidi ya Tanzania, zilipatiwa majibu ya haraka ndani ya Bunge la Ulaya, na sifa njema za Tanzania na kazi njema inayofanywa na Rais Samia Suluhu zikaelezwa ndani ya Bunge hilo.
View attachment 2030928