Mabaki ya miili ya Watanzania iliyopo Ujerumani kurejeshwa Tanzania

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Imechukua zaidi ya karne tangu mabaki ya miili ya Watanzania yahifadhiwe katika makumbusho mbalimbali nchini Ujerumani na sasa uamuzi wa kuyarejesha umefikia hatua nzuri.

Baadhi ya mabaki hayo ni yake ya miili ya machifu na viongozi mbalimbali waliokuwa vinara katika vita vya Tanganyika dhidi ya Ujerumani (Majimaji), mwaka 1905/07.

Hatua ya kurejeshwa kwa mabaki hayo, imedokezwa leo Jumanne Oktoba 31, 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan alipozungumza na waandishi wa habari baada mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom