Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, atafanya Ziara ya Kikazi nchini kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 01 Novemba 2023. Ziara hii mbali na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kwenye kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.

Ujumbe wa Rais Steinmeier utakao jumuisha viongozi wengine wa Serikali, pamoja na wawekezaji wa makampuni makubwa 12; utawasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Oktoba 2023 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba.

Sonderthema_10022022_Steinmeier_0.jpg

Akiwa nchini, Rais Steinmeier atafanya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 31 Oktoba 2023. Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao watapata fursa ya kuongea na Waandishi wa Habari kuelezea kuhusu masuala muhimu yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yao.

Kadhalika, Marais watapata fursa ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara, litakalohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo mbili, lililoandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani kwa ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika Hoteli ya Hyatt Regency; ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao watapokea taarifa iliyojadiliwa na Jukwaa hilo.

Siku hiyo hiyo, Rais Steinmeier anatarajiwa kuonana na kuzungumza na vijana wajasiriamali wa Kitanzania wanaojihusisha na uvumbuzi wa teknolojia mpya hususan matumizi ya akili bandia ambao wanafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani. Vilevile, Rais Steinmeier atatembelea Kiwanda cha Twiga Cement Jijini Dar es Salaam kinachoendeshwa kwa ubia na Kampuni ya Scancem International ya Ujerumani.

Siku ya tarehe 01 Novemba 2023, Rais Stenmeier atasafiri kwenda Wilayani Songea Mkoani Ruvuma kutembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji na Shule ya Msingi ya Majimaji. Hii ni makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonesha historia kubwa ya Vita vya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 60. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati hususan biashara na uwekezaji, maji, afya, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake, uhifadhi wa bioanuai, usimamizi wa fedha, utalii pamoja na malikale na utamaduni.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Tanzania imekuwa ikiuzia Ujerumani bidhaa zenye thamani ya wastani wa Dola za Marekani milioni 42.04 kwa mwaka. Bidhaa kuu ambazo Tanzania inaiuzia Ujerumani ni pamoja na Kahawa, Tumbaku, Pamba, Asali, Samaki, Nta na vito vya thamani.

Kadhalika, Tanzania inaagiza bidhaa kutoka Ujerumani zenye wastani wa Dola za Kimarekani milioni 237.43 kwa mwaka na bidhaa kuu zinazoagizwa kutoka Ujerumani ni Dawa, Vifaa Tiba, Mafuta (manukato, vipodozi) Magari, Vifaa na Mashine za Umeme.

Kwa upande wa uwekezaji, Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini. Kwa mujibu wa TIC hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.

Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imefanikiwa kusajili miradi 15 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300.00 ambayo imezalisha ajira 905.

Kampuni za Kijerumani zilizowekeza nchini zinajihusisha zaidi na sekta za kilimo, viwanda, nishati mbadala, ujenzi, utalii sanaa na utamaduni.

Kufanyika kwa ziara hii ni ushahidi tosha kuwa Diplomasia ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inazidi kupaa.
 
Wakati mfalme pamoja na malkia wa uingereza wanazuru Kenya Oct 30. Hadi Nov.4,hii Sasa siyo siasa chafu?
Nini kipo nyuma ya pazia?
 
Jifunzeni kuchukulia mambo positively! mmekalia conspiracy theories tu ndo mana hamuendelei
 
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, atafanya Ziara ya Kikazi nchini kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 01 Novemba 2023. Ziara hii mbali na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kwenye kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.

Ujumbe wa Rais Steinmeier utakao jumuisha viongozi wengine wa Serikali, pamoja na wawekezaji wa makampuni makubwa 12; utawasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Oktoba 2023 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba.

View attachment 2796751

Akiwa nchini, Rais Steinmeier atafanya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 31 Oktoba 2023. Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao watapata fursa ya kuongea na Waandishi wa Habari kuelezea kuhusu masuala muhimu yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yao.

Kadhalika, Marais watapata fursa ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara, litakalohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo mbili, lililoandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani kwa ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika Hoteli ya Hyatt Regency; ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao watapokea taarifa iliyojadiliwa na Jukwaa hilo.

Siku hiyo hiyo, Rais Steinmeier anatarajiwa kuonana na kuzungumza na vijana wajasiriamali wa Kitanzania wanaojihusisha na uvumbuzi wa teknolojia mpya hususan matumizi ya akili bandia ambao wanafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani. Vilevile, Rais Steinmeier atatembelea Kiwanda cha Twiga Cement Jijini Dar es Salaam kinachoendeshwa kwa ubia na Kampuni ya Scancem International ya Ujerumani.

Siku ya tarehe 01 Novemba 2023, Rais Stenmeier atasafiri kwenda Wilayani Songea Mkoani Ruvuma kutembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji na Shule ya Msingi ya Majimaji. Hii ni makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonesha historia kubwa ya Vita vya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 60. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati hususan biashara na uwekezaji, maji, afya, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake, uhifadhi wa bioanuai, usimamizi wa fedha, utalii pamoja na malikale na utamaduni.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Tanzania imekuwa ikiuzia Ujerumani bidhaa zenye thamani ya wastani wa Dola za Marekani milioni 42.04 kwa mwaka. Bidhaa kuu ambazo Tanzania inaiuzia Ujerumani ni pamoja na Kahawa, Tumbaku, Pamba, Asali, Samaki, Nta na vito vya thamani.

Kadhalika, Tanzania inaagiza bidhaa kutoka Ujerumani zenye wastani wa Dola za Kimarekani milioni 237.43 kwa mwaka na bidhaa kuu zinazoagizwa kutoka Ujerumani ni Dawa, Vifaa Tiba, Mafuta (manukato, vipodozi) Magari, Vifaa na Mashine za Umeme.

Kwa upande wa uwekezaji, Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini. Kwa mujibu wa TIC hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.

Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imefanikiwa kusajili miradi 15 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300.00 ambayo imezalisha ajira 905.

Kampuni za Kijerumani zilizowekeza nchini zinajihusisha zaidi na sekta za kilimo, viwanda, nishati mbadala, ujenzi, utalii sanaa na utamaduni.

Kufanyika kwa ziara hii ni ushahidi tosha kuwa Diplomasia ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inazidi kupaa.
Sasa waache kuomba sijui urejeshwaji wa mafuvu ya Machief.Waongelee mambo ya kimkakati; ukarabati wa Reli ya kati,walete viwanda vya kuunganisha magari,kushirikiana katika utafiti wa gesi,uimarishaji wa Shirika la Umeme,Afya na Elimu.
Ayo mambo ya kina Kinjekitile Ngwale,yasiwepo mezani kwa Rais,atashughulikia January Makamba.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Ziara hii mbali na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Tanzania na Ujerumani, pia imelenga kwenye kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji.

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya 60. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati hususan biashara na uwekezaji, maji, afya, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake, uhifadhi wa bioanuai, usimamizi wa fedha, utalii pamoja na malikale na utamaduni.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Tanzania imekuwa ikiuzia Ujerumani bidhaa zenye thamani ya wastani wa Dola za Marekani milioni 42.04 kwa mwaka. Bidhaa kuu ambazo Tanzania inaiuzia Ujerumani ni pamoja na Kahawa, Tumbaku, Pamba, Asali, Samaki, Nta na vito vya thamani.

Kadhalika, Tanzania inaagiza bidhaa kutoka Ujerumani zenye wastani wa Dola za Kimarekani milioni 237.43 kwa mwaka na bidhaa kuu zinazoagizwa kutoka Ujerumani ni Dawa, Vifaa Tiba, Mafuta (manukato, vipodozi) Magari, Vifaa na Mashine za Umeme.

Kwa upande wa uwekezaji, Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini. Kwa mujibu wa TIC hadi kufikia Agosti 2023, miradi 178 ya Ujerumani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 ilisajiliwa na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.

Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imefanikiwa kusajili miradi 15 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 300.00 ambayo imezalisha ajira 905.

Kampuni za Kijerumani zilizowekeza nchini zinajihusisha zaidi na sekta za kilimo, viwanda, nishati mbadala, ujenzi, utalii sanaa na utamaduni.
Kufanyika kwa ziara hii ni ushahidi tosha kuwa Diplomasia ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inazidi kupaa kimataifa.
 
Sasa waache kuomba sijui urejeshwaji wa mafuvu ya Machief.Waongelee mambo ya kimkakati; ukarabati wa Reli ya kati,walete viwanda vya kuunganisha magari,kushirikiana katika utafiti wa gesi,uimarishaji wa Shirika la Umeme,Afya na Elimu.
Ayo mambo ya kina Kinjekitile Ngwale,yasiwepo mezani kwa Rais,atashughulikia January Makamba.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Sasa waanze kuikarabati tena reli ya mkoloni ( reli ya kati) huoni ,ni gharama wakati Kuna sgr ndo suluhisho la reli ya kati
 
Back
Top Bottom