Mwanajeshi mstaafu wa Ujerumani na nia mbaya dhidi ya Tanzania

Sep 17, 2021
39
84
David James McAllister, aliyezaliwa January 12 mwaka 1971, ni mtu wa kutiliwa mashaka makubwa anayehudumu katika Bunge la Ulaya (European Parliament) kutokea Ujerumani.

McAllsiter ambaye ana doa kubwa la kuwa mbaguzi wa rangi ana mtetezi mkubwa wa ndoa za jinsi moja (Ushoga) ameonekana kwenye macho ya wachache hapa Tanzania, kupitia video yake wakati akizungumza hoja za uongo zenye lengo ya kuichafua Tanzania.

Pamoja na kwamba hoja zake zilipingwa vikali ndani ya Bunge la Ulaya baada ya kuwepo kwa wabunge wanaofahamu sifa njema za Tanzania, wajuzi wa Diplomasia wanaweka ‘alert’ juu ya McAllister kulingana na historia yake.

Moja kubwa ni kwamba Dvaid MacAllister ni mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Ujerumani, ambalo kihistoria lilijaa ubabe na uonevu dhidi ya mataifa mengi ya Afrika, bila kusahau ujuzi wao wa kutengeneza migogoro katika mataifa ya Afrika kwa maslahi ya vyama vyao.

David MacAllsiter ambaye pia ni mjuzi wa sheria, ni mfano wa Wanajeshi wa mataifa ya kibeberu ambao wametumika kuleta uchonganishi katika nchi nyingi za Afrika, baadae wakaingiza mauaji, mapinduzi ya haramu, machafuko makubwa ya kisiasa, kisha wakateka na kuiba mali.

Katika kufanya hivyo, Wanajeshi wenye hila mbaya kama McAllister, hutumia wanasiasa wa upinzani katika Mataifa ya Afrika ambao mara nyingi wanakuwa wamekosa madaraka. Hujenga nao ukaribu ili wawe chambo ya kuleta uharibifu katika nchi zao.

Ni jambo la kutia shaka, pale ambapo David ameanza kuitupia macho Tanzania. Aanataka nini Tanzania? Ametumwa na nani na watanufaikaje iwapo Tanzania itatatetereka?

Hata hivyo, jambo jema Kwa Tanzania na baya kwa David McAllister, ni kwamba hoja zake za uongo dhidi ya Tanzania, zilipatiwa majibu ya haraka ndani ya Bunge la Ulaya, na sifa njema za Tanzania na kazi njema inayofanywa na Rais Samia Suluhu zikaelezwa ndani ya Bunge hilo.

50MEPS_David-McAllister-714x714.jpg
 
Sijakuelewa unamaanisha nini

Tulipozuia bidhaa kwenda Kenya ulishangilia Leo tumeondoa vizuizi niliona unashangilia.
Tulipowaita mabeberu ulishangilia Leo tumefuta ubeberu niliona umeshangilia
Makomdo walipofutwa KAZI ulishangilia Leo wanasema ukweli unashangilia.

Kama una uchungu na walichofanya wajerumani kwanini pia usijifunze kuwa na uchungu na wanachopitia akina adamoo.

Mwisho unapoandika mada tambua unaandikia wenye akili timamu siyo akili zakushikiwa na maisha yakukariri fikra za mwenyekiti.

Ninyi ndo mnatufanya tusiajiriwe
 
Je unaleta habari za aina gani? Unashindwa kutafuta habari na kuhakikisha habari zako ni sahihi? Nimeshangaa tu kidogo maelezo yako, nikaangalia habari zake.

McAllister kamwe ni mwanajeshi mstaafu. Alipokuwa kijana katika miaka ya 1980s, alipaswa kuingia katika huduma ya kitaifa ya jeshini, kama vijana wote wa kiume huko. Ukitafuta habari hizo, utaoona siku zile walikuwepo vijana mamilioni katika nchi za Ulaya waliopaswa kufanya jeshini kwa miezi kadhaa, hadi miaka 2 . Kufuatana na mantiki yako, Ulaya inajaa "wanajeshi wastaafu"??

Yale mengine kuhusu historia sijui umepata wapi. Ila kama unashindwa kuona tofauti kati ya mwanajeshi mstaafu na kijana anayepaswa kuingia katika huduma ya kitaifa, sidhani kwamba umeweza kufanya utahmini wa habari kwa jumla.
 
Pinga hoja zake. Ukianza na wewe kumchafua kibinafsi basi inamaanisha hoja zake umeshindwa kujibu. Kumuita mtu beberu, shoga, muongo, n.k halafu hoja zake hujibu moja kwa moja hakusaidii kwenye dunia ya leo. Inawezekana kweli huyu mtu ni beberu, shoga aliyejaa uongo lakini hoja aliyotoa bungeni ina mshiko. Ajibiwe kwa hoja naye.
 
Je unaleta habari za aina gani? Unashindwa kutafuta habari na kuhakikisha habari zako ni sahihi? Nimeshangaa tu kidogo maelezo yako, nikaangalia habari zake.
McAllister kamwe ni mwanajeshi mstaafu. Alipokuwa kijana katika miaka ya 1980s, alipaswa kuingia katika huduma ya kitaifa ya jeshini, kama vijana wote wa kiume huko. Ukitafuta habari hizo, utaoona siku zile walikuwepo vijana mamilioni katika nchi za Ulaya waliopaswa kufanya jeshini kwa miezi kadhaa, hadi miaka 2 . Kufuatana na mantiki yako, Ulaya inajaa "wanajeshi wastaafu"??
Yale mengine kuhusu historia sijui umepata wapi. Ila kama unashindwa kuona tofauti kati ya mwanajeshi mstaafu na kijana anayepaswa kuingia katika huduma ya kitaifa, sidhani kwamba umeweza kufanya utahmini wa habari kwa jumla.
Ukiwa CCM na akili zinapukutika Mkuu. Eti wote waliopitia JKT ni wanajeshi wastaafu??
 
wale wa upande ulee, hawawezi kukuelewa , maana walishaaminishwa na viongoz wao(miungu watu) kuwa wazungu na watu weupe ni tegemeo lao na watetez wao,

so unapowaongelea vbaya wadhamini wa hawa majamaa zetu(upinzan) unakuwa kama unawachokoza sana na hawatokuelewa,

Ukwel n kuwa hakuna na kamwe hakutowai kuwepo Upendo kat ya mtu mweupe na mweus, ukwel mchungu hao majamaa wafanyavyo kuwasapot wapnzan tokea afrika, uo si upendo, bali ni mtego wa kuchochea machafuko na mtengano wa kuwachanganya waafrika wasiungane na kuifanya afrika kuwa kitu kimoja.

Ni kwel kuwa Ccm ni chama chakavu na hovyo.
Ni kwel kuwa katiba ya sasa Tz ni chakavu na useless.

Lkn Kwa wapinzan wa Tz pamoja na mambo wanayoyataka ktk katiba, ni wazi kuwa yapo kwa maslahi yao na uroho wa madaraka kuinua chama chao na si waTZ, maana mwafrika wa kwel, hawez kutetea mibeberu wala kuombea mabaya nchi yake kwa hao wafadhiri, kwakuwa waumiao ni raia masikin pale muiombeapo nchi iwekewe vikwazo, wakuumia si hao wanaCcm ni wananchi masikin,

Kwahiyo wapinzan hawana huruma kwa wananchi zaid zaid wakipata madalaka watayatumia kulipiza visasi badala ya kuendeleza nchi.

Hakuna siasa ya kwel nchin Tz zaid ya vituko na upumbavu
 
Umsipoteza muda tunawambia kila siku leteni uhuru wa siasa kama majirani zetu kenya badala ya kutumia nguvu nyingi na kupoteza muda. Mnafikiria Watanzania wa kizazi hiki wana jua mambo ya wajerumani!!!. Wanacho jua uchaguzi ulikuwa fake na mbowe kabambikwa kesi hayo mengine ni kupoteza muda
 
Sijakuelewa unamaanisha nn
Tulipozuia bidhaa kwenda Kenya ulishangilia Leo tumeondoa vizuizi niliona unashangilia.
Tulipowaita mabeberu ulishangilia Leo tumefuta ubeberu niliona umeshangilia
Makomdo walipofutwa KAZI ulishangilia Leo wanasema ukweli unashangilia. Kama una uchungu na walichofanya wajerumani kwanini pia usijifunze kuwa na uchungu na wanachopitia akina adamoo.

Mwisho unapoandika mada tambua unaandikia wenye akili timamu siyo akili zakushikiwa na maisha yakukariri fikra za mwenyekiti.

Ninyi ndo mnatufanya tusiajiriwe
Hawa wanjulikana kwa jina marufu la vinyonga watu
 
Wazungu hawatujui,sasa ngoja tu wachambe ile mbaya.Hatuna shida nao wametuibia madini yetu na hata Magufuli hakuwai kwenda Ulaya kwao.

Hatuhitaji misaada yao na wasidhani sisi kwa kuwa na wabunge wenye kujuwa kusoma na kuandika tu eti ni wajinga.
 
Najaribu kuunganisha doti hapa juzi dada yao Fatuma kaanzisha tena mambo ya ushoga ambayo ni sera ya MaCHADEMA iliyoletwa Na Lissu baada ya kulelewa Ulaya miaka mitatu Na sasa amerudi tena huko. Leo anazuka shoga mwingine huko eti kuhoji haki za binadamu Tanzania. MaCHADEMA janja janja ya kuleta ushoga nchi hii msahahu yaani hata msiote. Kama hamna hoja sambaratikeni tu manaka sasa mmekua kama TLP.
 
Wazungu hawatujui,sasa ngoja tu wachambe ile mbaya.Hatuna shida nao wametuibia madini yetu na hata Magufuli hakuwai kwenda Ulaya kwao.
Hatuhitaji misaada yao na wasidhani sisi kwa kuwa na wabunge wenye kujuwa kusoma na kuandika tu eti ni wajinga.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Alienda nawalimhudumia hadi akaja kupata Urais kwa hisani yao ya Peacemaker.
Ukaidi tu,angekuwa bado Rais wetu.
Tukubali kuishi kwa kuchukuliana kwa mwenye nacho/asiyenacho.
 
Back
Top Bottom