Mwanadamu, ujasiri wa kumnyang'anya godoro masikini unayemdai umeupata wapi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,187
22,713
Salaam,Shalom!!

(Mithali 19:17)
Amhurumiaye maskini, humkopesha BWANA.

Mungu anachukia sana Umaskini, lakini anawapenda sana maskini,

Mungu ndiye hufukarisha, na ndiye hutajirisha!!

Maskini wa Leo ni tajiri kesho, maana Mungu ndiye huwapandisha maskini na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwashusha wenye viburi.

Mungu amekuwa akikemea sana kuwaonea maskini, hapendi waonewe Wala kuvunjiwa Heshima Yao, kuwachokoza maskini na wajane na yatima ni kugusa mboni ya jicho la Mungu.

Hivi unawezaje kumnyang'anya godoro pekee analolalia maskini baada ya kukopa pesa ya kununulia chakula Kwa ajili ya familia yake,Ujasiri huo umeutoa wapi, watoto wa maskini watajisikiaje kuona baba Yao ananyanganywa godoro pekee la kulalia?

Ujasiri wa kwenda kumpora kanga au kitenge alichojifunika Jirani Yako Kwa sababu ameshindwa kukulipa deni lako unautoa wapi?

Maskini amekuja kwako anakuomba umkopeshe unga Ili akampikie mgeni wake aliyefika usiku huo, unampa Kwa masharti ya kukulipa siku mbili zijazo, Kwa Bahati mbaya, anashindwa kutimiza AHADI yake, ujasiri wa kwenda nyumbani kwake na kuchukua sufuria pekee analotumia kupikia chakula umeutoa wapi?

Mungu Toka juu, anakuangalia, anakudai pesa kiasi Gani Kwa kutolipa ZAKA, mbona hajawahi kukudhalilisha?

Tangu Leo, jifunze kubariki maskini,

Ukimkopesha maskini na akashindwa kulipa, mpe Muda atakulipa atakapopata, kamwe usimdhalilishe. Mungu atakufungulia mlango wa kupata pesa bila kudhalilisha binadamu mwenzio.

Mungu na awabarikie wote wasaidiao binadamu wenziwe, hiyo ndiyo IBADA na DINI ya KWELI.

Aamen
 
Mtu mmoja akanifuata amejaa bashasha usoni, nikamuuliza vipi Kuna nini?

Akaniambia, nimepata Bahati Leo, nimekutana na Jirani yangu ana mgonjwa hospitali baada ya kushindwa kulipa deni, ameniomba nimsaidie laki 7, alipe gharama za matibabu, nikamuuliza ukishindwa kunilipa rehani Yako nini nifanye? Anayeuguliwa akasema, nikishindwa kulipa, chukua shamba LANGU.

Mtu yule baada ya kusikia vile, akatafuta laki Saba haraka na kumpa Kisha akapewa nyaraka za shamba la Jirani, tamaa ilishamwingia kuwa amepata shamba kirahisi, akajiapiza kuwa atafanya Kila Mbinu kuhakikisha analipata shamba lile.

Nilifadhaika sana kusikia maneno Yale.

Kwa kufanya vile, mtu yule alikuwa anajichumia LAANA mbeleni,sababu malipo ni hapa hapa duniani.
 
Hata bank ukishindwa kulipa wanauza nyumba.
Mwingine amemkopesha maskini laki Moja,

Baada ya wiki mbili kupita anaenda kuchukua friji ya laki 6 na kuona amepata.

Mungu juu Huwa anaangalia, na mabaya lazima yaje kumpata mtu yule mbelen
 
Kuna mtu alishaenda kudai kwa staili hii na biti kibao , hivi tunavyozungumza mdai ni marehemu aliuliwa na mdaiwa. Ameacha na familia.
 
Salaam,Shalom!!

(Mithali 19:17)
Akopeshaye maskini, humkopesha BWANA.

Mungu anachukia sana Umaskini, lakini anawapenda sana maskini,

Maskini wa Leo ni tajiri kesho, maana Mungu ndiye huwapandisha maskini na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwashusha wenye viburi.

Mungu amekuwa akikemea sana kuwaonea maskini, hapendi waonewe Wala kuvunjiwa Heshima Yao, kuwachokoza maskini na wajane na yatima ni kugusa mboni ya jicho la Mungu.

Hivi unawezaje kumnyang'anya godoro pekee analolalia maskini baada ya kukopa pesa ya kununulia chakula Kwa ajili ya familia yake,Ujasiri huo umeutoa wapi, watoto wa maskini watajisikiaje kuona baba Yao ananyanganywa godoro pekee la kulalia?

Ujasiri wa kwenda kumpora kanga au kitenge alichojifunika Jirani Yako Kwa sababu ameshindwa kukulipa deni lako unautoa wapi?

Maskini amekuja kwako anakuomba umkopeshe unga Ili akampikie mgeni wake aliyefika usiku huo, unampa Kwa masharti ya kukulipa siku mbili zijazo, Kwa Bahati mbaya, anashindwa kutimiza AHADI yake, ujasiri wa kwenda nyumbani kwake na kuchukua sufuria pekee analotumia kupikia chakula umeutoa wapi?

Mungu Toka juu, anakuangalia, anakudai pesa kiasi Gani Kwa kutolipa ZAKA, mbona hajawahi kukushalilisha?

Tangu Leo, jifunze kubariki maskini,

Ukimkopesha maskini na akashindwa kulipa, mpe Muda atakulipa atakapopata, kamwe usimdhalilishe. Mungu atakufungulia mlango wa kupata pesa bila kudhalilisha binadamu mwenzio.

Mungu na awabarikie wote wasaidiao binadamu wenziwe, hiyo ndiyo IBADA na DINI ya KWELI.

Aamen
Maskini unakopaje? Acha ujinga maskini hakopi anaomba huyo anayekopa lazima alipe
 
Hata bank ukishindwa kulipa wanauza nyumba.
Hiyo mifumo ya kuwafanya wakopaji wapoteze hata kidogo walichonacho,

Mfumo huo ni WA kishetani,

Afisa mkopo amefanya Utafiti na kugundua biashara ya mkopaji kamwe haitoweza kulipa mkopo, lakini Kwa kuwa ameona mkopaji ana nyumba, anampa mkopo fasta Ili waje kupata faida kuuza nyumba.

So sad!!
 
Maskini unakopaje? Acha ujinga maskini hakopi anaomba huyo anayekopa lazima alipe
Mtu aliyeuguliwa na ana mtoto amelazwa hospitali,

Akija kwako kuomba utampa pesa?

Huwa wanakopa baada ya kugomewa kupewa msaada.

Tuwe na ubinadamu.
 
Kuna mtu alishaenda kudai kwa staili hii na biti kibao , hivi tunavyozungumza mdai ni marehemu aliuliwa na mdaiwa. Ameacha na familia.
Wengine Huwa wanadhalilisha yaani baba anakabwa kama Mwizi, Kila sababu aitoayo hasikizwi.

Mungu atusaidie.
 
Mfanyakazi wako anakujia, anakwambia amefiwa, anaomba Ruhusa aende kuzika,

Mwajiri anamruhusu aende, hampi hata mia, ila anampa sharti kuwa siku atakazokaa msibani zitakatwa kwenye mshahara ujao.

Hiyo wanayo sana wahindi.

Huu SI ubinadamu!!
 
Kuna mtu alishaenda kudai kwa staili hii na biti kibao , hivi tunavyozungumza mdai ni marehemu aliuliwa na mdaiwa. Ameacha na familia.
Ulitaka kuwa salama acha kukopesha kabisa,mtu ankuja na shida zake zimembana unajinyima kukopesha tena bila riba matatizo yake yakiisha ukimdai linakuwa tatizo Tena...
 
Ulitaka kuwa salama acha kukopesha kabisa,mtu ankuja na shida zake zimembana unajinyima kukopesha tena bila riba matatizo yake yakiisha ukimdai linakuwa tatizo Tena...
Hapo Imani Inatakiwa.

Ukitoa Kwa Imani, na usiiwazie pesa Ile, Mungu atajazia ulipotoa,

Kama huna Imani, Bora kutomkopesha ikiwa hutokuwa na uvumilivu au kushindwa kuhimili HISIA zako time unaaubiria kulipwa.

Mengine Mungu huyaleta kutujaribu WANADAMU.

Ubarikiwe.
 
Niliwahi kuona Rafiki amemtendea WEMA Jirani yake,

Jirani huyo alikopa pesa bank na kuweka nyumba pekee ya familia rehani,

Aliposhindwa kulipa, Bank walitangaza mnada, Rafiki wa Jirani aliyekopa alivyosikia hivyo, alimpigia kaka yake aliyekuwa na uwezo na kumwomba amsitiri Jirani yake na fedheha Kwa kununua nyumba Ili analizane na bank Kisha aje kumrudisha nyumba Jirani yake akimaliza kulipa Polepole.

Siku ya mnada ulipofika, jamaa akanunua nyumba kimya kimya bila mkopaji kujua,

Baada ya bank kulipwa pesa Yao,

Jamaa Akaenda Kwa Jirani yake na kumwambia sisi ndio tulinunua nyumba Yako, tunakupa muda ulipe pesa Ile tuliyowalipa bank, Kisha nyumba Yako tutakurudishia.

Jamaa alilipa Polepole mkopo Ule Kwa miaka zaidi ya kumi na kufanikiwa kurudisha nyumba yake.

Niliona ubinadamu wa mtu yule Kwa UKWELI.

Na huo ndio unaitwa urafiki wa Kweli

Ni kumfaa mtu wakati wa DHIKI.

Ubarikiwe kama pia umewahi kumfaa ndugu, jamaa au hata mtu usiyemfahamu wakati wa DHIKI yake.

Aamen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom